Wale wa Mgambo JKT mpo?

Duh! Afande Fusi mnamkumbuka na unoko wake? Mie nilikuwa Operation Kambarage. Afande Balua na Omari walivyokuwa wanoko wanatukwepesha ndege. Kablasi na punda wake na alivyokuwa anajitafutia misifa.

kweli mkuu, hapa operation miak 30 ya uhuru, mnakumbuka afande balua, omari, nange na wengineo. kutoroka pale upitie kabuku (kituo cha basi) au gendagenda (kituo cha train), kote pori.
 
Mkuu zile 'lokoo' ulizikwepa vipi? Wako akina dada walikuwa wanalala kwenye mahanga ya wanaume wawahi lokoo, ukichelewa ilikuwa ni kifo. Tulikuwa tunakwenda Kwa Msanga weekend kubadilisha mlo, chakula maarufu ilikuwa mihogo na kuku wa kienyeji kishushio chai ya rangi. Genda Genda the untold stories of migunga..

Wacha uzee unichote sasa. Enzi hizo nilikuwa mtemi sana kwa wale mavoluntia. Niliwahi kumkwida mmoja wao aliyenikuta natafuta madafu ya kutelemshia baada ya kula mihogo ya kuchoma, jina lake simkumbuki ila alikuwa jamaa fulani wa kigogo; akataka kuniletea mkwara nikamwambia nitampa kichapo cha heshima kule porini asipate msaada wowote. Alitetetemeka sana na kunisihi nimwache yaishe. Kambini akawaeleza wenzake kuwa du, kile kichuguu siyo mchezo; basi wote wakawa wananiogopa kama ada; nikifanya kosa lolote wao wanajifanya hawakuliona. Kwenye adhabu za jumla za kuruka kichura, push up na kukimbia kwa kunyanua bunduki nilikuwa nayeya kama vile siyo kitu.
 
Nilipita Mgambo Mwaka 78. Nilikuwa miongoni mwa wale vijana waliokuwa wamejificha wanakula machungwa na Mtono akatokea kwenye kichaka - tukarushwa kichura mpaka quater guard kwa MP afande Dick. DD Kaganga

It sounds like ndie huyo, atakuwa alihamia Oljoro baada ya kuondoka Mgambo. Nikiwa mgambo kuna kuruta walikuwa wanaletwa toka Oljoro kuja Mgambo JKT kama adhabu. Jamaa alisomea Israeli na alikuwa anatembeza ukomandoo kikosini. Kuna stori moja pale mgambo kuruta walitoroka shamba wakajichimbia kwenye kichaka wanakula machungwa jamaa akawazukia na kuwarusha kichura hadi kikosini.
 
Ukweli wale tulikuwa nao Mgambo 1978 - 79 (Operation "USHINDI") tuwasiliane. Mimi nilikuwa Kombania "B" nawakumbuka afande Anthony, Mkombozi, nk.
 
Mimi sikuwa Mgambo ila hili jina la Mtono linanikumbusha afande mmoja kule Oljoro JKT alikuwa anaitwa Ali Mtono, kama ndo huyo basi jamaa alikuwa nuksi kishenzi miaka hiyo ya 1989/90 operation Program ya chama.
Mimi nilikutana na Mtono Malale JKT, dash we acha tu!

Sent from my TECNO-L8Plus using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom