Wale wa Mgambo JKT mpo?

MNDEE

JF-Expert Member
Jul 10, 2009
491
68
Wale mliopitia Mgambo JKT Kabuku Tanga mko wapi na mnafanya nini?

Nilikuwa operation Okoa kombania D ya Afande Tito. Nakumbuka kasheshe za afande Mtono (RIP) na migunga. Wachache tumeendelea kuwasilina na wengine hatunao tena, Saidi Usi (RIP), Masele Madalali (RIP), Macline Ndembeka yuko Dar, kuna wengine wapo BOT na jamaa mmoja ni mtangazaji ITV simkumbuki jina.
 
Mimi sikuwa Mgambo ila hili jina la Mtono linanikumbusha afande mmoja kule Oljoro JKT alikuwa anaitwa Ali Mtono, kama ndo huyo basi jamaa alikuwa nuksi kishenzi miaka hiyo ya 1989/90 operation Program ya chama.
 
It sounds like ndie huyo, atakuwa alihamia Oljoro baada ya kuondoka Mgambo. Nikiwa mgambo kuna kuruta walikuwa wanaletwa toka Oljoro kuja Mgambo JKT kama adhabu. Jamaa alisomea Israeli na alikuwa anatembeza ukomandoo kikosini. Kuna stori moja pale mgambo kuruta walitoroka shamba wakajichimbia kwenye kichaka wanakula machungwa jamaa akawazukia na kuwarusha kichura hadi kikosini.
 
Nakumba kuna kijana aliliwa na simba kipindi cha utawala wake.
 
Last edited:
Mie sikuwepo huko ila nimepita kambi nyingine. Nikiangalia naona maafande wengi uliowataja hapo umeweka RIP yaani wameshakufa. Nami ninaowakumbuka kule nilikopitia wameshazikwa siku nyingi. Hawa maafande wanapukutika jamani,kulikoni? Ngoma au nature of work/working condtions?
 
Sikuwahi kwenda Jeshini ila My Bro alipitia hiyo kambi miaka ya 90/91 alinisimulia visa vingi sana vikiwa vya maafande kula totoz kwa sana na kusababisha maambukizo ya NGOMA kuwa juu sana.Aliniambia Huyu Rais wa Congo saa hivi Kabila walikuwa naye kombania moja pale Mgambo alikuwa anaweza ondoka saa saba usiku kuna defender ilikuwa inakuja kumchukua na ikimrudisha alikuwa akija na some documents analala nazo yaani anahakikisha hakuna mtu anazipata/kuzisoma. Anasema kuna wakati walikwenda porini wakati wa mazoezi ya kijeshi walikwenda km kilometa kumi hivi na mida ikawa km saa mbiliya usiku hivi kamanda wao akasema sasa tumemkaribia adui sasa kabla hakuja kucha kila pair( mwanamke na mwanamme walichanganywa) iwe imeshachimba handaki la kujificha in case ADUI anawashambulia, palikuwa hapatoshi unaambiwa walitifua udongo ilipofika saa nane wengi walikuwa wamefikia at least kiunoni, basi wakaanza kupumzika wengine wanapiga mbonji kiusanii ilipotimu saa kumi na moja watu walikuwa hoi wanakoroma afande si akapiga risasi hewani kuwashtua my bro anasema yule dada alyekuwa nae alijikojolea pale pale kwa uwoga alikua kweli adui anawashambulia hhahaha.
Kitu kingine anasema ladies walikuwa wakipewa Tshirt na bukta siku za kwanza wakizivaa zilivyo fupi basi wanajitahidi sana kuzivuta kwa chini lakini kwata ikishanoga na wakizoea hahahaha wanajimwaya tuuu kama wamevaa skin tigth zao. Lakini all in All kila MTu aliyepitia Jeshi akitoka huko huwa wanasifia sana nadhani iliweza kuficha sana Tofauti zetu za kimaisha na kuwaweka wa TZ karibu zaidi kuliko ilivyo hivi sasa
 
Argh! ufuska mtupu kule. Usiombee dadako aingie anga zile mkuu.
 
Nakumba kuna kijana aliliwa na simu kipindi cha utawala wake.

Hiyo mikasa ya watu kuliwa na simba hata mimi niliisikia, infact nilikuwa na mpango wa kutoroka baada ya kuelezwa hiyo mikasa nikaachana nao. Kwanza inabidi mtoroke usiku wa manane na mtembee kwa miguu, safari yenyewe ni ndefu na mnapita katikati ya msitu. Mbali na simba pia ilikuwepo hofu ya kudakwa na afande Mtono ambaye alikuwa anatokea mahali when he was least expected.
 
MNDEE inaonekana umekula chumvi nyingbi ni miaka gani hiyo tena ??

Firstlady naona ulikuwa ama hujazaliwa au kinda maana waliopitia jeshini watataka kujua mtu alikuwa operation gani.
 
Last edited:
Argh! ufuska mtupu kule. Usiombee dadako aingie anga zile mkuu.

Kama ilivyo vyuoni, makazini na kwingineko jeshini nako ilikuwa hivyo hivyo ukitaka dezo au mtelemko ndio inabidi uingie kwenye pay to play.
 
Wengi tumepita huko bana na sasa tupo makazini huku uraiani. Kuna tofauti kubwa sana kati ya kule na huku aisee. Kule kumezidi mno kwa ngono mkuu!!
 
Hiyo mikasa ya watu kuliwa na simba hata mimi niliisikia, infact nilikuwa na mpango wa kutoroka baada ya kuelezwa hiyo mikasa nikaachana nao. Kwanza inabidi mtoroke usiku wa manane na mtembee kwa miguu, safari yenyewe ni ndefu na mnapita katikati ya msitu. Mbali na simba pia ilikuwepo hofu ya kudakwa na afande Mtono ambaye alikuwa anatokea mahali when he was least expected.
Mambo ya kwenda kujificha kwenye michungwa (Washington)...! Husisahau lile pori la kuelekea Kabuku mjini lilikuwa na nyoka aina ya chatu pia...!
 
Mkuu lile pori nililipita mara kibao tukipelekwa kabuku hata sikumbuki tulikuwa tunakwenda kuchukua nini.

Nakumbuka kulikuwa na jamaa mmoja mlemavu, kazi yake ilikuwa kugawa vifaa ya kwendea shamba, alikuwa anatutia hasira maana kila tukirudi toka shamba lazima atutolee maneno ya maudhi, mara ohoo kuukata sio lazima uende Ulaya au angalia miguu yenu inavyowatesa, watu walikuwa wanatamani wampe kipigo, akawa anaambiwa asisahau tuko pale muda mfupi tutarudi uraiani huko ndio ataona faida ya kuwa na miguu.
 
Wengi tumepita huko bana na sasa tupo makazini huku uraiani. Kuna tofauti kubwa sana kati ya kule na huku aisee. Kule kumezidi mno kwa ngono mkuu!!

Mkuu wale waliokuwa wanajifanya maselule na kufukuzia 'B' hiyo ndiyo ilikuwa fallback plan yao.
 
Last edited:
Duh! Afande Fusi mnamkumbuka na unoko wake? Mie nilikuwa Operation Kambarage. Afande Balua na Omari walivyokuwa wanoko wanatukwepesha ndege. Kablasi na punda wake na alivyokuwa anajitafutia misifa.
 
Mkuu umenikumbusha mbali, na ile mizigo ya kuni na masharti yake. Afande anakuambia kuni ziwe na urefu kukuzidi, mzunguko usipungue unene wa mguu wako, kuni zisipungue kumi. Mzigo ukija unakaguliwa kama hukufuata masharti unaambiwa kautupe ule kichura, kuni zinafichwa next time mzigo ule ule unaletwa.
 
Duh! Afande Fusi mnamkumbuka na unoko wake? Mie nilikuwa Operation Kambarage. Afande Balua na Omari walivyokuwa wanoko wanatukwepesha ndege. Kablasi na punda wake na alivyokuwa anajitafutia misifa.
Dah hao kina balua, Omari, Cheupe, Kitwee (Alikuwa dereva wa Lile Isuzu jipya) nasikia wengi washaondoka duniani.
 
Dah, sasa hii nini tena.

Mimi nilipitia Mgambo kipindi kifupi sana baada ya vita ya Uganda. Afande Mtono alikuwa Lt Col wakati ule; nimesikitika sana kusikia kuwa sasa ana-RIP; ila alikuwa mtemi sana. Kwenye ile mitaa ya Genda Genda, KwaMsanga KwaLaguru na vitongoji vinginevyo vya jirani nilikuwa mwenyeji sana. Kabuku nilipitia tu wakati nakwenda na kurudi kutoka kambini kwa kuwa singeweza kufika kuke kule kwa mguu kuzurura au kujongo.

Kwa utemi wangu (siku hizo) sikupiga kwata hata siku moja pala Mgambo na wale mavoluntia walikuwa wakinigwaya sana kwa vile niliwahi kumkwida mmoja wao. Nadhani hiyo iliwafanaya wapende niodoke pale haraka sana kwenda kwenye leader's course ambako nilijipatia tepe yangu nikawa voluntia pia.
 
Mkuu zile 'lokoo' ulizikwepa vipi? Wako akina dada walikuwa wanalala kwenye mahanga ya wanaume wawahi lokoo, ukichelewa ilikuwa ni kifo. Tulikuwa tunakwenda Kwa Msanga weekend kubadilisha mlo, chakula maarufu ilikuwa mihogo na kuku wa kienyeji kishushio chai ya rangi. Genda Genda the untold stories of migunga..
 
Back
Top Bottom