Wale wa galanos agriculture sec school miaka ya 1999-2002...tujikumbushe!.

don-oba

JF-Expert Member
Dec 8, 2011
1,387
677
"Galanos school penda watoto....twakupenda twakusifu!.." mnaukumbuka huo wimbo?, Headmaster alikua T. Z. KINALA, namkumbuka sana mwl wa michezo Msocha. Tulikuwa tukitoroka tunaenda disco Club Lacasachika, siku moja walipitisha bed check usk tukakutwa hatupo. Suspension miezi miwili ndo ilikua adhabu kali. Special diet kwa wale wagonjwa tulikua tukivizia sicksheet za uongo tupate mbogamboga. J'4 na j'moc watu walikua wanajaa dinning hall kwasababu ya nyama na ubwabwa. Miogo 'chipc dume' ilikua zetu pale mwisho wa rami kwa ma K. J-DRONE na SOKORO hizo chata zilipigwa hadi kwenye kiti cha headmaster. Daladala zetu za Nguvumali, majani mapana- mjini zilikua full muziki. Patner wetu walikua TANGA tech na St Christina. Mkonge, Chai na pamba dom zilikua poa. Hebu tukumbushane mambo mengine wadau.
 
nakumbuka msocha aliwapa washkaji adhabu ya kukata mbuyu mmoja ulikuwa karibu na msikiti pale...aliwaambia wauchimbe hadi mizizi yake udondoke ..washakaji wakamwambie bora utufukuze shule kuliko kufanya mambo ya ubunuasi
 
Msocha alikua akizungumza kiingereza chake cha nukta.
 
Msocha hajajua kuzungumza kingereza hadi leo,ST wa siku hizi wanazingua mbaya Korogwe girls na Galanos wameunda undugu kuanzia disco mpaka kitaaluma wanakimbiza vibaya,MKONGE imekarabatiwa inashaini kinoma na KAHAWA ndo bweni chafu kuliko yote kwa sasa.
 
Dah msocha alinitesa mbwa yule...alifanya mpaka nisaidi black book..nawakumbuka wakina Mack-master,massawe a.k.a mzee wa mabomba ya english,kinenekejo,akida.
 
Dah msocha alinitesa mbwa yule...alifanya mpaka nisaidi black book..nawakumbuka wakina Mack-master,massawe a.k.a mzee wa mabomba ya english,kinenekejo,akida.

mack master yuko wapi siku hizi ticha wangu wa geography huyu alisababisha nipige A ya geography a-level
 
Zamu za kufuga je? Tulikuwa tunapandisha ng'ombe porini afu hela tunagawana
 
Dah msocha alinitesa mbwa yule...alifanya mpaka nisaidi black book..nawakumbuka wakina Mack-master,massawe a.k.a mzee wa mabomba ya english,kinenekejo,akida.

umenikumbusha mama kinenekejo, akida katufundisha Kiswahl. Nimekaa Mkonge dom, kuna kipindi msocha alianzisha kufanya mazoezi asbh. Watu tukawa tunajificha hatwendi...siku hiyo nikajificha kwenye dust bin nikalifungua nikaingia bana then nikalifunga, iliku ni vigumu kugundua. Yeye alipofika akalifungua, ilikua soo yani sisahau.
 
aha aha aha,mi mwenyewe nilikaa mkonge na mwl wa bweni alikuwa Akida,mwaka 2005 2lifanya bonge la mgomo na kurudishwa hme kisa ng'ombe wa graduation ya form four.
 
aha aha aha,mi mwenyewe nilikaa mkonge na mwl wa bweni alikuwa Akida,mwaka 2005 2lifanya bonge la mgomo na kurudishwa hme kisa ng'ombe wa graduation ya form four.

nakumbuka kuna mwana kutoka kigoma alirusha bonge la jiwe usiku pale tukiwa parade likamkosa kosa head master
 
nakumbuka kuna mwana kutoka kigoma alirusha bonge la jiwe usiku pale tukiwa parade likamkosa kosa head master

aha aha yule dogo alikuwa na sura ngumu jina lake limenitoka...msocha na yule mwalimu mwenye benzi alimchapa karugendo 2kataka kumchapa nae
 
J-DRONE na SOKORO, hizo chata kweli bado zipo au zilishafutwa?. Sintoisahau Galanos, imenipa future. Ila waliniudhi mwaka 2005 nilifwata cheti changu cha O'level wakanambia nadaiwa kitabu cha History, nikawapa buku ten yakaisha.
 
You go pick the want-want- Socha Boy

Nimemuona last year and the guy looks the exact same
 
Socha boy noma sana jamaa alikua na kiingereza cha kubahatisha... mihogo ya mama Kijazi pale nje ilituweka sana mjini.
 
aha aha yule dogo alikuwa na sura ngumu jina lake limenitoka...msocha na yule mwalimu mwenye benzi alimchapa karugendo 2kataka kumchapa nae
unamkumbuak msombwa? second master ..hahaha yule jamaa alikuwa kiboko aise. karugendoyule mwana aliyekuwa anavaa miwani? namkumbuka sana.
 
unamkumbuak msombwa? second master ..hahaha yule jamaa alikuwa kiboko aise. karugendoyule mwana aliyekuwa anavaa miwani? namkumbuka sana.

ha ha ha! Msobwa kuna wakati aliugua aka-pararise mguu akadai kwamba amerogwa!
 
Lori la shule lazima lisukumwe kuwaka nakumbuka form 1 ndo ilikuwa kazi because our classroom was close to where they parked it.
 
Msocha ni mwl. Wa bweni la Mkonge na ni msumbufu kama mbu,Mzee,Kinene,Karia wote wamehama lkn Mzee kawa head master wa Masechu,
 
Back
Top Bottom