Elections 2010 Walaka wa maaskofu na waislamu uko wapi? Wakati wake ni huu

QUALITY

JF-Expert Member
Sep 27, 2010
853
115
Ndugu zangu, mimi ni mgeni katika forum hii lakini kuna jambo moja nimelikumbuka ambalo huu ndio wakati wake muafaka. kuna walaka wa maaskofu waliouzindua mwaka huu ambapo baadaye waislamu nao walizindua walaka wao. sasa nyalaka hizi zililenga kuwafikishia ujumbe wapiga kura ili wasidanganyike mwaka 2010. sasa ziko wapi? Huu ndio wakati muafaka kuzieleza hadharani ili wananchi wafanye maamuzi sahihi.

wafuatao wanawajibu wa kujitokeza hadharani na kuueleza umma wa watanzania kuhusu nyaraka hizo ili watanzania waelewe namna ya kuchagua viongozi bora. Hongera kwa Kabobe kwa kuonesha njia hapo jana. Big Up!

watu hao ni pamopja na
1. Shekhe mkuu wa Tanzania
2. Mkuu wa Bakwata
3. Askofu mkuu Pengo
4. Askogu Gamanywa
5. Maaskofu wote tanzania ambao ni members wa Christian Council of Tanzania (CCT), Christian Social Service Committee (CSSC), Baraza la maskofu katoriki tanzania (TEC) n.k
Tukumbuke viongozi wa dini na madhehebu wanaongoza watu ambao maisha yao yanaathiriwa na maamuzi ya wana siasa. Viongozi hawa wasipoeleza ukweli watakuwa wanafiki. kwa sababu wananchi wataingia kuchagua chama badala ya mtu mwenye uwezo wa kuongoza ambaye ameonesha mfano wa namna ya kutetea maslahi ya Taifa. Hebu amkeni na kufungua vunywa vyenu na kuwajuza watanzania kuhusu ubaya na uzuri wa utawala unaomaliza muda wake. Huu si wakati wa kuendelea kuwaacha waumini gizani huku wengi wenu (viongozi wa dini na madhehebu) mkinung'unikia chini chini.

Kwa wanaoweza pia wekeni link ya kupata nyaraka hizo katika net ili wengine tuzisome pia.
 
Huyu bwana kweli ni mgeni kwa kila kitu. Nyaraka hizi zilishauzwa na kusambazwa nchi nzima kwa wale waliotaka kuzisoma. Sasa wakati huu ni za nini? Wengine wanasubiri kufuata maagizo ya nyaraka hizi na wengine watakuwa kama mbayuwayu!
 
Inawezekana nyaraka ziliuzwa lakini zilikuwa chache na kuhisi kuwa kila mpiga kura amesoma na anasubili kutekeleza inaweza kuwa si kweli. Ninasema huu ndo wakati wake maana waraka ulitolewa mwanzoni mwa mwaka huu. So wakatin kampeni zimekaribia huu ndo wakati muafaka kuweza kuufafanua zaidi na kuwasaidia wapiga kura kuelewa.

Ndugu Bolobi Shekhe sikumweka sababu yeye hakutoa waraka. Najua ni sehemu ya waislamu na wale wenye imani hiyo. Lakini waraka kama ule wa maaskofu, unapinga matendo mengi yanayofanywa na viongozi na serikali ya CCM.
 
katika black hapo.. & Your point Is......>:confused2:
 
Crap
 
Huyu bwana kweli ni mgeni kwa kila kitu. Nyaraka hizi zilishauzwa na kusambazwa nchi nzima kwa wale waliotaka kuzisoma. Sasa wakati huu ni za nini? Wengine wanasubiri kufuata maagizo ya nyaraka hizi na wengine watakuwa kama mbayuwayu!

Nadhani yuko sahihi. Kama zipo zibandikwe tena tuzijadili. Mwenye nazo aziweke
 
Tusisahau kuwa Watanzania ni Wadanganika na wengi ni wasahaulifu. Kilichoandikwa january kinaweza kusahaulika zaidi ya kitakachosemwa leo. So waumini wa dini na madhehebu yote yakikumbushwa sasa by the time tunaingia kwenye uchaguzi, watakuwa bado wanakumbuka na watafanya kweli. Tuna haki ya kuingo'a serikali dharimu inayowanyanyasa watz katika masuala ya afya, elimu na utajiri.
 
Arusha umeandikwa mwingine kwa mazingira ya Arusha - KKKT, TAG na RC. Lakini nakala tunazo ni suala la kuzisoma na kujikumbushia. Kardinali Pengo kesha ongeza juzi kule Pugu na kurudia mle mle kwenye waraka wa wakatoliki, sasa wewe unataka wafanye nini zaidi, kutaja majina?
 
Back
Top Bottom