Walaah muda wa kitimoto umefika

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
55,489
86,005
Wapendwa, Baada ya kufanya kazi kutwa nzima sasa ni muda wa kwenda kupumzika na kuianza weekend kwa furaha, kwani naamini bado tumebakisha vijisenti vya kale ka-salary.

Twendeni pale nanihii tukapate kitimoto kwa afya, hasa kwa wale wagonjwa na wale wanaojihisi ni wagonjwa wakale ka-ugonjwa kaleee.

Just wanted to say Good weekend to you all
 
kweli bana!! sijala mdudu long tyme! leo nita-do ze needful kwa mdudu!
 
Just kwa afya, karibuni si msubiri hadi muandikiwe na Daktari....ni dawa ile ati.
 
Hapana, sema na kajipilipili kwa mbaaali

Kitimoto haungwi kwa nazi ukumbuke, Sio Tanga hapa.

Juma juzi kanambia kaenda Tanga kafika kaungiwa kitimoto ya Nazi.....mmhhh

Kanywa supu yake tu, Walaah, kamkubali yule mtoto wa kitanga kwa kuunga, maudenda yananitoka hapa tu, naenda zangu mie
 
attachment.php
attachment.php
attachment.php
attachment.php
attachment.php
 
Safi, hasa kwa wagonjwa wa Ini, ni dawa kali na nzuri sana
 
Astakafilulah, Una hatari sana, itabidi nitungie shairi la kuhusu mdudu
 
hahaha kabla hamjampa jina la KITimoto kule kwetu Nyumbi hii bombi hii tulikuwa tukimuita MKUU WA MEZA, hahaha Mshawahi kula URUST pale Angoni Arms enzi hizo? hahahahaha Nishafanya sana biashara ya kuuza kitimoto. Songea tunafuga km mbuzi tu kila nyumba wana kamfugo raha ya AJABU
 
Haha!!! Kuanza weekend na chairfire. Mimi sipo bana. Mpaka mniambie kama kale kaugonjwa kameshapatiwa dawa!!!
Mimi nilishasilimu kuepuka matatizo. Ila sasa nasikia ndo wenyewe!!
 
Baadhi ya madoctor wamegudua kuwa nguruwe na vijidudu. vinavyomfanya awe mbishi, hata kama kutakuwa na mti mbele atalazimisha apite hapo*hapo. Na pia wamegundua kuwa hivyo vijidudu hata vikipikwa havifi, kwa hyo yule mlaji atakuwa na ubishi kama wa nguruwe. Au mnabisha, hapo walaji lazma watabisha!!!!
 
nilikula kitimoto songea jamani, jumajosi na jumapili kwangu ilikuwa sherehe kila wiki...jamani, tupigiane pande basi, wapi wanapika vizuri hapo bongo, manake hayo masahani wengine wameonyesha hapo juu, tayari naona nahitaji mdudu mara moja...
 
Mie nashangaa sana hawa wanaojiita madoctor, wamesambaza uzushi eti kale kamdudu kana virusi ambavyo hata ukikaangiza havifi. Waongo wakubwa hawa, hivi wanajua mafuta au wanacheza, hebu tuwachemshe wao kwenye mafuta ya kitimoto kama hawataungua, ni upuuzi;

Lakini unajua imesaidia kupunguza upinzani na kugombewa kwani sasa tutabaki wachache zaidi na bei nayo pengine itashuka; ukizangatia na wale ndugu zetu wasabato wameshatangaza azma ya kuacha kumtumia. heh eheeeeee,
 
kama virusi mbona hata kuku wana virusi, wasitubabaishie mboga yetu hapa...tena leo weekend....
 
Na samaki pia, si wamekunywa mafuta yenye kemikali toka kwenye lile bomba la mafuta la marekani, naskia ma-doctor watatota tamko sasa hivi kupitia WHO, kwa hiyo wadau tukimbilie kitu moto fastaaaaa
 
hasa kwa mwezi mtukufu kunakuwa na oda chache so ni full kujiachia
mix with yours
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom