Wala kitimoto tahadhari: It's not a tumor, It's a brain worm

Wanasanyansi waendelee kuchunguza zaidi. Ingekuwa ni kweli hiyo kitu basi nchi kama China wangepunguza matumizi ya hiyo nyama na hata huku kwetu pia.

Binafsi bado sijaamini ila kukija na evidence za kutosha nitaamini.
Naam; China ndio nchi inayoongoza kwa uzalishaji na ulaji wa nguuwe duniani - more than 70% ya nguruwe duniani wako China.
 
Katika kitabu cha Mambo ya Walawi 11 ndipo utaona katazo la vitu vinavyopaswa kuliwa. (Hili ni agano la kale)
Baada ya kifo cha Yesu na ufufuko wake sheria nyingi za agano la kale ama zilibadilishwa au kufutwa.
Moja wapo ya sheria hizo ni hii ya kula nguruwe.
Na badiliko hili unalipata katika kitabu cha Matendo ya Mitume 10:9-15 (agano jipya)
"..... 12. Ambayo ndani yake walikuwamo aina zote za wanyama wenye miguu minne, na hao watambaao, na ndege wa angani. 13. Kisha sauti ikamjia kusema, ondoka Petro, uchinje ule. 14.Lakini Petro akasema, hasha, Bwana, kwa maana sijakula kamwe kitu kilicho kichafu au najisi. 15. Sauti ikamjia mara ya pili ikimwambia, Vilivyotakaswa na Mungu, usiviite wewe najisi."


Paulo anawadanganya nyinyi.

Yesu anasema hakuja kutenguwa taurati, sasa wewe na huyo Petro na Yesu nani zaidi?
 
“Nguruwe msimle; ana kwato zilizogawanyika lakini hacheui; kwenu ni najisi. Kwa sababu wanyama hao ni najisi msile nyama yao wala msiguse mizoga yao” (Walawi 11: 7 – 8).
Soma na Matendo ya Mitume 10:9-15
 
“Nguruwe msimle; ana kwato zilizogawanyika lakini hacheui; kwenu ni najisi. Kwa sababu wanyama hao ni najisi msile nyama yao wala msiguse mizoga yao” (Walawi 11: 7 – 8).
Sauti ikamjia mara ya pili, ikamwambia, vilivyotakaswa na Mungu, usiviite wewe najisi. Matendo ya Mitume 10:15
 
Kila kiumbe kina magonjwa hata wewe bi Faiza hapo ulizo yawezekana si mzima - acha kuwapotoshaa watu wasile kitu kilichobarikiwa mbinguni na duniani. Ukitaka kula Nguruwe........ (Malizia basi)
images
 
Ni mtanzania gani aliyewahi kupata UGONJWA/ MADHARA kama haya ya kula nyama ya nguruwe....

Nitajieni haraka sana!.....


Nadhani ndio itakuwa njia pekee ya kunifanya niache kula kitimoto.

Sio kusoma habari za wazungu na nijiridhishe kuwa niache kula hii CHAIRFIRE....
 
Wanapoambiwa msile nguruwe ni haramu, hata biblia imeandika hivyo, wao wamo tu.
Kuna haramu ngapi duniani? hujatembea wewe ukutane na hizo haramu utakula tu hata kama na samaki asiyeparuriwa na asiye na magamba. swala la kujudge vyakula wanavyokula binadamu ni gumu sana.

Hii dunia ni kubwa sana na wote ni wa huyo huyo wa kwenye biblia, Quran na vitabu vingine vyote vitakatifu uvijuavyo.

kama ni kukataza kula kwa sababu za kiafya ama kitafiti basi dini isiingie. hata mbuzi, nyoka, vyura, konokono, panya buku watu tunakula tu.
 
Paulo anawadanganya nyinyi.

Yesu anasema hakuja kutenguwa taurati, sasa wewe na huyo Petro na Yesu nani zaidi?
Hahaaa nilifikiri umesema biblia imekataza, sasa mbona mimi nimetoa quotation ya biblia unaniambia tena Paulo anatudanganya!?
Hilo katazo la kwanza lilitolewa na Mungu kupitia Musa na la ruhusa imetolewa na Mungu kupitia kwa Petro sasa kama uliamini ya Musa kwa nini usiami ya Petro!?
 
“Nguruwe msimle; ana kwato zilizogawanyika lakini hacheui; kwenu ni najisi. Kwa sababu wanyama hao ni najisi msile nyama yao wala msiguse mizoga yao” (Walawi 11: 7 – 8).
Kumbuka pia imeandikwa ,amelaaniwa Mtu yule atundikwaye msalabani. Kama tujuavyo, Kristo alitundikwa msalabani.

Je tuseme alilaaniwa ? Hasha, ni ili atimize yaliyoandillkwa. Hivyo andiko hili amelitamka katika agano jipya kuwa hakuna kilicho nje kimtiacho Mtu unajisi.
 
1. Ukimwi upo na watu wanagegedana daily
2. Kansa ipo lakini watu wanavuta sigara daily
3. Ajali zipo, lakini tunasafiri daily.. Kwa mfano timu ya mpira wa miguu ya Zambia kasoro Kalusha yote ilizama na ndege lakini ndege zinaendelea kusafirisha watu
4. Meli zinazama, lakini tunasafiria kila siku
5. Majengo yanabomoka, lakini kila siku tunajenga.. NA DANGOTE KAJA KUTENGENEZA VIJENGEO
6. Watu wanachomana visu kila siku, laikini hatuishi kununua
7. Gesi inauwa, lakini tumezijaza majumbani
8. Umeme unauwa, lakini ngoja ukatike uone malalamiko...
9. SUmu inauwa lakini tunaitengeneza kila siku
10. etc etc

HIVYO UKITAKA USIFE KESHO, KUFA LEO KESHO HUTAKUFA
mwambie tumemsikia ila kitimoto atuache nacho kwa sasa hyo minyoo itafahamika tu.
 
Back
Top Bottom