Wakuu wekeni busara zenu...

maliyamungu

JF-Expert Member
Aug 14, 2011
564
412
Mwanangu wakike mdogo wa miaka 3 namwambia toka nje nivae. Kanijibu Mbona mama nae mwanamke umwambii toka nje.. Na kila siku ndio swali lake yapata wiki sasa nimjibu nini Wakuu? Busara plz!!
 
unategemea na unavyoilea familia yako,kaz hyo c yako anaitakiwa aifanye mkeo wakat we haupo,au mkeo naye tatzo nn?ucje ukawa umeoa msanii kama akna wema sepetu na irene uwoya
 
mwambie yule ni mama.....yeye ni mtoto......
akikuwa mama hutamwambia tena.....
 
unategemea na unavyoilea familia yako,kaz hyo c yako anaitakiwa aifanye mkeo wakat we haupo,au mkeo naye tatzo nn?ucje ukawa umeoa msanii kama akna wema sepetu na irene uwoya

Leo vipi!Toa hii kitu huku wewe moderator
 
Hii thread imeinigiaje huku ipelekeni kwenye joks inatutia kichfuchefu watu tuconcentrate na issuies huku.
 
mnalala na mtoto chumba kimoja? Kama ndiyo miaka 3 ni wakati muafaka wa kumhamisha chumba.

Mtoto anafunzwa maadili angali mdogo, ni wakati wa kumfundisha hata kugonga mlango ili kuingia chumba chenu.

Khs swali lako unaweza mwambia ukweli kuwa mama yake ni mkeo, anaruhusiwa,ila yeye ni mtoto, ni vibaya,hadi akue atakapoolewa!

Si unajua wazee wetu walituambia ukimchungulia mkubwa utapofuka macho? Nayo ilileta utii kwa watoto mkubwa akivaa unaondoka ili usipofuke macho!
 
Hivi hi thread kwanini bado ina survive huku, iondolewe ipelekwe kwenye mapenzi au joke, wengine tukikosea sekunde unakuta imeondolewa
 
mnalala na mtoto chumba kimoja? Kama ndiyo miaka 3 ni wakati muafaka wa kumhamisha chumba.

Mtoto anafunzwa maadili angali mdogo, ni wakati wa kumfundisha hata kugonga mlango ili kuingia chumba chenu.

Khs swali lako unaweza mwambia ukweli kuwa mama yake ni mkeo, anaruhusiwa,ila yeye ni mtoto, ni vibaya,hadi akue atakapoolewa!

Si unajua wazee wetu walituambia ukimchungulia mkubwa utapofuka macho? Nayo ilileta utii kwa watoto mkubwa akivaa unaondoka ili usipofuke macho!
Asante kwa hekima mkuu
 
Ndio tatizo la kuleta "demokrasia" hata kwenye mambo ya msingi yasiyohitaji mijadala. Mwambie aende sebuleni haraka!!

BTW, hamisha hii thread huku. Peleka MMU.
 
Back
Top Bottom