Wakuu wa Wilaya Kutangazwa!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,466
113,551
Wanabodi,
Rais Jakaya Kikwete, ameahidi kuwatangaza wakuu wapya wa wilaya ndani ya kipindi cha mwezi mmoja kuanzia leo!.

Rais Kikwete ametoa tip hiyo wakati wa ufunguzi wa jengo jipya la Ofisi za Ukaguzi za Taifa (National Audit Office) Mkoa wa Morogoro.

Rais Kikwete alitoa tip hiyo kufuatia utambulisho wa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Bi. Halima Dendegu, anakaimu ukuu wa wilaya nyingine tatu, hivyo JK kumshukuru mkuu wa wilaya tatu na kumwambia "nitakutua mzigo huo ndani ya mwezi mmoja!.
 
Kama ameweza kukaimu wilaya tatu kwa muda mrefu na kila kitu kiko sawa kuna haja ya hizi ceremonial post kweli
 
Kuwa DC wa wilaya nne ni sawa kabisa na kuongoza mkoa. Kwanini hamteuwi kuwa RC kwani ameonesha anaweza. Kwa upande wa pili inaonesha hakuna umuhimu wa watu hawa (DCs') iwapo mtu mmoja anaweza kwa wakati mmoja kuongoza wilaya nne na kusiwe na shida.

Nao huu ni Ubazazi.

Ndimi BAZAZI
 
Haaaaa! Bazazi ni wewe?
Uko njema Mkuu?
 
sometime hivi vyeo vya uDC na uRC naviona havina tofauti na status ya machief waliokuwepo wakati wa ukoloni wa mwingereza ni mfumo mbovu saana DAS na RAS wanatosha sana vimekaa ka vifavour Flani hivi..... Ni mfumo wa kichama zaidi na KATIBA isiporekebisha haya hata dola ikishikwa na upinzani nao hawatabadilisha kwani ni mfumo wa kupeana ulaji kwa watu "walio loyal" kwa utawala means vibaraka
 
Duh....kukaimu wilaya Tatu??
Hiyo ni moja kwa moja kuwa hizo nafasi hazina maana yeyote ile, ni kutafutiana ulaji tu.
Bora zifutwe, the present has just disapproved them.
 
Wanabodi,
Rais Jakaya Kikwete, ameahidi kuwatangaza wakuu wapya wa wilaya ndani ya kipindi cha mwezi mmoja kuanzia leo!.

Rais Kikwete ametoa tip hiyo wakati wa ufunguzi wa jengo jipya la Ofisi za Ukaguzi za Taifa (National Audit Office) Mkoa wa Morogoro.

Rais Kikwete alitoa tip hiyo kufuatia utambulisho wa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Bi. Halima Dendegu, anakaimu ukuu wa wilaya nyingine tatu, hivyo JK kumshukuru mkuu wa wilaya tatu na kumwambia "nitakutua mzigo huo ndani ya mwezi mmoja!.

Kutangazwa ma DC, nayo ni issue mkuu?
 
Tegemea jina la huyu tapeli kuwemo, hapo ndio mtajua kweli RAHISI mnaye??? Poor us????

attachment.php

Habari zake gonga hapa

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...m-na-kashfa-ya-utapeli-ahaha-kujisafisha.html
 
How diffult is it to appoint one to be a DC?!, kama ni ngumu kuteua aje aombe msaada humu JF tumtengenezee sofyware ya kuappoint watu kushika ceremonial posts.
 
Mh Raisi uwezo ninao,nipe nafasi,ktk hizo wilaya tatu alizokaimu kana kwamba hakuna watz wenye uwezo wa kushika hizo nafasi,nilikuwa sijui kama unatafuta wa kukusaidia kazi
nipo tayari Mh RAISI kukusaidia kazi,nipe kazi nifanye kazi

kazi ipo jamani
 
Back
Top Bottom