Wakuu wa mikoa inayolima korosho kuandamana kumuona rais Kikwete

POMPO

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
6,690
2,400
Na Steven Augustino

Wakuu wa Mikoa inayolima Korosho nchini wameahidi kupeleka kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete kero ya ubabaishaji wa bei ya soko la zao hilo ili aweze kulitafutia ufumbuzi wa kudumu zikiwa ni juhudi za kuwawezesha Wakulima kupata matunda ya jasho lao.

Hayao yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Saidi Mwambungu wakati akiongea na wadau wa maendeleo waliojitokeza katika kikao cha dharula cha kujadili hatima ya tukio la ubabaisshaji wa soko la Korosho ambalo msimu huu bei yake imeonesha kusuasua kilichofanyika katika ukumbi wa Boma la halmashauri ya Wilaya hiyo mjini hapa .

Sambamba na maamuzi hayo pia Mwambungu na kamati hiyo ikatoka na azimio la kutouza Korosho hizo kwa Makampuni hayo babaishaji vinginevyo wakubali kununua Korosho hizo kwa Bei itakayo kubalika na wakatumia nafasi hiyo kumuomba Meneja wa Benki ya Nmb Omari Mleche kuongeza mkopo kwa vyama vya msingi ili kuwezesha kununua Korosho zote kwa wakulima wakati juhudi za kutafuta Soko la uhakika zikiendelea.

Akifafanua taarifa hiyo Mwambungu alisema kuwa maamuzi hayo yamefikiwa na Wakuu wa Mikoa ya Lindi Ruvuma na Mtwara baada ya kubaini kuwerpo kwa ubabaishaji wa Soko hilo ulio oneshwa na Wanunuzi hao wakubwa Korosho katika Msimu huu hauwezi kufumbiwa macho na Serikali na kuwaacha Wakulima wakiteseka bila msaada wa Serikali yao.

Awali wakitoa taarifa ya ubabaishaji wa Soko la Mazao hayo Meneja wa Chama Kikuu cha Wakulima wa Korosho TAMCU Ltd Imani Kalembo na Mwenyekiti wa Chama hicho Mahamudu Katomondo walisema kuwa ubabaishaji huo umeonekana katika minada mitatu iliyopita ambapo Makampuni ya Abbas Eport Treding Co.Ltd na Olam Co. Ltd awali wote waliomba kununua chini ya Bei ya Tsh. 1500 kwa kilo moja hali iliyo onesha kuwa makampuni hayo yana ajenda ya siri ya kutaka chama hicho kishindwe kuwalipa Wakulima wake malipo yao ya awamu ya pili.

Walisema kinacho watia mashaka zaidi viongozi hao na kuwafanya wabaini uwepo wa mchezo mchafu kutoa katika Makampuni hayo ni kitendo cha Makampuni hayo pekee kati ya Makampuni 70 ambayo yalijiandikisha na kuomba kununua Korosho hizo katika Msimu huu wa Mwaka 2011/2012,

Wakizungumzia taarifa ya ununuzi Korosho hizo kutoka kwa wakulima walisema kuwa hadi sasa vyama vya msingi vya ushirika vime kwisha kusanya jumla ya Kilo 4,554334 kati ya Kilo 7,000,000 zinazotarajiwa kununuliwa katika Mismu huu na chama chao.

Wakitoa maoni yao wabunge wa Wilaya ya Tunduru Eng. Ramo Makani na Alhaji Mtutura Mtutura waliiomba Serikali kutumia Fedha zilizo idhinishwa katika Bajeti iliyopita kwa ajili ya Matumizi ya dhalula ili zitumike kununula Korosho hizo kutoka kwa Wakulima zikiwa ni juhudi za kuwaondolea adha hiyo.

Nao Madiwani Kazembe said wa kata ya Ligunga na Burhani Nakanje wa Kata ya Marumba mbali na kuutuhumu uongozi wa Kiwanda cha Kubangulia Korosho kinacho milikiwa na Kampni ya Korosho Africa Ltd kuto kuwa na msaada kwa wakulima wa Wilaya yao waliiomba Serikali kuwa na macho na Wanunuzi hao vinginevyo watawaangusha na kuwafanya wananchi kukosa imani na Serikali yao.

Wakijibu tuhuma za Kiwanda hicho kuto kuwa na msaada kwa Wakulima wa zao hilo msimamizi wa Kiwanda hicho Dinesh Poojali na Enginia wa Kiwanda hicho Sivan Edayath mbali na kutoa taarifa kuwa kiwanda chao kimefungwa kutokana na kuishiwa Korosho za kubangua walisema kuwa wao hawana maamuzi yoyoyte juu ya ununuzi wa korosho hizo kutoka katika vyama vya ushirika vya msingi vya Wakulima wa Tunduru.

Source:Stephano Mango na Jamii ya Watanzania: WAKUU WA MIKOA INAYOLIMA KOROSHO KUANDAMANA KUMUONA RAIS JAKAYA KIKWETE
 
Hatua yao inaweza leta immediate solutions lakini sio suluhisho ya kudumu sio mara moja unasikia rais anaingilia kati ununuzi wa korosho toka awamu ya tatu kumekuwa na interventions za namna hiyo lakini baada ya misimu kadhaa tatizo linajirudia. Sasa kutatua hilo tunahitaji kuwa na sera ya viwanda vidogo na vya kati ili tuweze kuuza product ambayo tumeiadd value na kwakuwa mkulima atauza kiwandani au kwenye chama cha msingi na chama cha msingi kitauza kiwandani then kiwanda ndo kitatafuta masoko kutakuwepo na bargaining power kubwa kutoka kwa maafisa wa viwanda vivyo kuwanufaisha wakulima kwa kuuza kwa bei nzuri na pia serikali kupata revenue yakutosha. Hii ni njia mojawapo ambayo mi ninaamini inaweza kututoa hapa tulipokwama.
 
Tatizo la serikali yetu ni kuingiza siasa katika mazao yetu makuu ya biashara. Usiniulize kwanini?
 
mikoa hiyo ina mamilioni ya tani za korosho hazijanunuliwa, wewe nenda vijijini then utangaze unanunua kilo 1 kwa 500 utapata korosho ambazo utajaza matela kadhaa ya malori
 
Hatua yao inaweza leta immediate solutions lakini sio suluhisho ya kudumu sio mara moja unasikia rais anaingilia kati ununuzi wa korosho toka awamu ya tatu kumekuwa na interventions za namna hiyo lakini baada ya misimu kadhaa tatizo linajirudia. Sasa kutatua hilo tunahitaji kuwa na sera ya viwanda vidogo na vya kati ili tuweze kuuza product ambayo tumeiadd value na kwakuwa mkulima atauza kiwandani au kwenye chama cha msingi na chama cha msingi kitauza kiwandani then kiwanda ndo kitatafuta masoko kutakuwepo na bargaining power kubwa kutoka kwa maafisa wa viwanda vivyo kuwanufaisha wakulima kwa kuuza kwa bei nzuri na pia serikali kupata revenue yakutosha. Hii ni njia mojawapo ambayo mi ninaamini inaweza kututoa hapa tulipokwama.
Naamini mwaka huu tutapata Suluhisho la kudumu...
Zitto kabwe acheni cheap politics kwa sababu mtaumbuka.
Tatizo la bei ya korosho ni unyonyaji unaofanywa na watu wale wale kwa miaka yote
 
Ndio ujue awamu ya 5 imejaa usaniii...ni ma cornartist msimu mmoja wakukima waliwekwa kwenye Righttrack msimu uliofuata zengwe utapeli CCM isepe tu...tumeichoka mtanzania huwezi kumtawala kwa mtutu kwa muda mrefu fact! fact! fact!
 
Utasepa wewe CCM haisepi ng'o itadumu mpaka wakati usio na kipimo.. Magufuli oyeeeeeeeeeeee.ccm OYEEEEEEEE.tanzania mpya oyeeeeeeeeeee...Mungu wetu oyeeeeeeeeeeeeeee
 
Ndio ujue awamu ya 5 imejaa usaniii...ni ma cornartist msimu mmoja wakukima waliwekwa kwenye Righttrack msimu uliofuata zengwe utapeli CCM isepe tu...tumeichoka mtanzania huwezi kumtawala kwa mtutu kwa muda mrefu fact! fact! fact!
Tumewajua wafanyabiashara wanaodhulumu wakulima kila mwaka
 
Back
Top Bottom