Wakuu okoeni maujanja nianyeje?

Eeka Mangi

JF-Expert Member
Jul 27, 2008
3,173
481
Jambo JF
Mimi bana naomba kwanza mniwie radhi. Najua ni maudhi kwenu ingawa pia kwa wengine inaweza kuwa baraka maana nimewaletea wenza wenu!
Miaka ya ujana wangu nilikuwa si haba jamani. Kama ni enzi hizi wallah nshafungwa!
Nikiwa kidato cha pili nilimpatia binti wa kidato cha kwanza ujauzito. Alifukuzwa shule na pia alijifungua katoto ka kike. Niliwahi kumwona mara moja tu! Then walipotea na mama yake. Sikujua waliko!
Nikiwa kidato cha nne house girl wetu naye likamkuta. Huyu alipata mtoto wa kiume! Akarudi kwao Singida!
Nikiwa namaliza kidato cha sita nikamwambukiza mwingine tena huyu alizaa mapacha. Naye tulipotezana sikujua aliko kwa kipindi kirefu.
Nikiwa pale Lang'ata Nairobi (Eti nilitakiwa niwe padri) nikapata binti mmoja naye hakudumu akaanza kutemea mate pembeni. Hakunivumilia akaja juu nikaachishwa chuo na kuozeshwa toto la Kwa Moi kipindi hicho.
Kwani kunguru mie nilidumu basi baada ya mtoto wa pili nikasepa nikarudi zangu Tanzania.
Nikapumzika kabisa na tangazo kubwa UKIPATA MIMBA URAFIKI WETU UMEKWISHA. So nimekaa hivyo kwa muda sasa.
Miaka 4 iliyopita nikaamua kuoa.
Huyu binti tuna mtoto mmoja naye ila anajua kuwa nina watoto 2 tu niliokuwa nao! Sikuwahi kumpa hadithi za hao wengine kwa kuhofia angeniona kiwembe sana.
Siku za karibuni nimeanza kupata salamu toka kwa watoto wale wa zamani wengine wakitamani kuniona tu. Kuna ambaye natarajia kuolewa siku za karibuni na anahitaji kumtambulisha mchumba wake kwa baba yake.
Naanzaje kumweleza mother house kuwa jeshi laja? Je ataelewa somo?
Najua wataalamu mpo humu! Sadia dugu!
 
kweli wanamme tumebaki wachache.

Ila, mwambie tu, atakasirika lakini ataelewa.
Huwezi mnyima mtoto haki yake ya kukuona, kwanza ulishamnyanyapaa vya kutosha.

Ukizeeka, hao watoto utawakumbuka sana.
 
Dah mkuu kumkana au kutosema ukweli kuwa ni wanao utakuwa hujawatendea haki...ni bora umwambie mama kuwa una kijiji cha watoto then akasirike ila atanyamaza na yataisha kuliko kuitosa damu yako....Mwambie yalikuwa ni mambo ya ujana na hufanyi tena..
na ingekuwa mbaya km ungewazaa wakati uko nae ila kwa kuwa ulikuwa bado hujawa nae hakuna tatizo kabisa
 
Hahahahaah!! Mkuu ulitisha ngoja nikae pembeni nisikilize ushauri utakaopata.
 
mmmh Shemeji kumbe hujatulia namna hii,Vip haka katabia umeacha baada ya kuoa?
Mwambie tu ukweli uwe huru
 
Mh! anzisha timu ya mpira uiite Eeka Mangi Fc.
MAPROSOO.
 
mangi mwenzangu hayo mambo yanaenda hvi, unaita wazee mnaandaa kasherehe na kuchinja ng'ombe mbili tatu na unaita ndugu zako pale na mkeo akiwepo, unatambulisha ukoo mangi, from there hakuna maneno yeyote, tena ukiwaambia huyo anaefunga ndoa ni baraka kabisa hiyo mambo inaisha. Cha muhimu ni hiyo party usiifanye bila wazee wenye heshima ukawaletea mbege na kuchinja mbuzi au ng'ombe kama unaweza. Hayo mambo yanaisha. Inabaki historia tu.
 
Jambo JF
Mimi bana naomba kwanza mniwie radhi. Najua ni maudhi kwenu ingawa pia kwa wengine inaweza kuwa baraka maana nimewaletea wenza wenu!
Miaka ya ujana wangu nilikuwa si haba jamani. Kama ni enzi hizi wallah nshafungwa!
Nikiwa kidato cha pili nilimpatia binti wa kidato cha kwanza ujauzito. Alifukuzwa shule na pia alijifungua katoto ka kike. Niliwahi kumwona mara moja tu! Then walipotea na mama yake. Sikujua waliko!
Nikiwa kidato cha nne house girl wetu naye likamkuta. Huyu alipata mtoto wa kiume! Akarudi kwao Singida!
Nikiwa namaliza kidato cha sita nikamwambukiza mwingine tena huyu alizaa mapacha. Naye tulipotezana sikujua aliko kwa kipindi kirefu.
Nikiwa pale Lang'ata Nairobi (Eti nilitakiwa niwe padri) nikapata binti mmoja naye hakudumu akaanza kutemea mate pembeni. Hakunivumilia akaja juu nikaachishwa chuo na kuozeshwa toto la Kwa Moi kipindi hicho.
Kwani kunguru mie nilidumu basi baada ya mtoto wa pili nikasepa nikarudi zangu Tanzania.
Nikapumzika kabisa na tangazo kubwa UKIPATA MIMBA URAFIKI WETU UMEKWISHA. So nimekaa hivyo kwa muda sasa.
Miaka 4 iliyopita nikaamua kuoa.
Huyu binti tuna mtoto mmoja naye ila anajua kuwa nina watoto 2 tu niliokuwa nao! Sikuwahi kumpa hadithi za hao wengine kwa kuhofia angeniona kiwembe sana.
Siku za karibuni nimeanza kupata salamu toka kwa watoto wale wa zamani wengine wakitamani kuniona tu. Kuna ambaye natarajia kuolewa siku za karibuni na anahitaji kumtambulisha mchumba wake kwa baba yake.
Naanzaje kumweleza mother house kuwa jeshi laja? Je ataelewa somo?
Najua wataalamu mpo humu! Sadia dugu!

Wewe ulikuwa mkareeeeeeeeeeee, mhh haya bana
 
hahahaah!! N'gombe hazeeki maini, huenda unaendeleza ule mchezo wa ujanani.

Kama ungekuwa mche wa sabuni saa hii hata kichema hakionekani! Ila ki ukweli sipo tena huko mkuu! Ingawa bado wananichokoza bana!
 
mangi mwenzangu hayo mambo yanaenda hvi, unaita wazee mnaandaa kasherehe na kuchinja ng'ombe mbili tatu na unaita ndugu zako pale na mkeo akiwepo, unatambulisha ukoo mangi, from there hakuna maneno yeyote, tena ukiwaambia huyo anaefunga ndoa ni baraka kabisa hiyo mambo inaisha. Cha muhimu ni hiyo party usiifanye bila wazee wenye heshima ukawaletea mbege na kuchinja mbuzi au ng'ombe kama unaweza. Hayo mambo yanaisha. Inabaki historia tu.

Don
Natamani nifanye hivyo ila maandalizi ya sherehe nafanya kibubu bubu ama! maana ka ni sherehe huwa tunajadiliana then tunatengeneza budget! Sasa hii ambayo haina kukaa na kuelezana nitaanzaje?
 
mangi labda hii itakusaidia...
hata kukupa confidence tu...
dingi yangu akiwa nje alizaa na mzungu...
mwaka 1982..
juzi mwaka 2010 mtoto anataka kuoa na ameambiwa dingi yake ni mtanzania...
na ana mawe ya kutosha...
dogo kamtafta dingi hakumkataa...wakaendelea kuwasiliana na kupanga kuja tz
huku dingi akalianzisha kwa kuwaambia wadogo zake (baba zangu wado)
akawaita home...na wazee wengine km alivosema don...
mama akasoma mchezo...
mambo yameisha...dogo amekuja bongo...
alala home akaenda zenj then akasepa canada anapoishi...nov mwaka huu anaoa aise..
 
Ha ha ha haaaa!! Wewe umekubhu kabisa mkuu. Kumbe una ukoo kabisa. Hili ni tatizo kubwa sana
 
Back
Top Bottom