Wakuu ni kweli haya yametokea Pemba au mimi naota ? Imekuwaje yametokea ?

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
Mwananchi
Mon 30 Jan 12:47AM
Hamad Rashid atikisa Pemba
BOOKMARK THIS PAGE
Hamad Rashid atikisa Pemba Send to a friend
Monday, 30 January 2012 11:40
0digg
Aziza Masoud, Pemba
MBUNGE wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohamed ambaye alitangazwa kuvuliwa
uanachama na chama chake, jana alipokewa kwa mbwembwe na kuimarishiwa
ulinzi alipowasili Pemba. Msafara wake uliongozwa na magari manne ya
polisi yakiwa na ving'ora na askari takriban 30.

Hamad amefungua kesi Mahakama Kuu akipinga uamuzi wa chama chake
kumvua uanachama huku akiitaka iwatie hatiani viongozi wakuu wa chama
hicho akiwemo Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Seif Sharrif Hamad
kwa tuhuma za kukiuka amri ya Mahakama.

Jana, Hamad aliwasili Uwanja wa Ndege wa Chake Chake, Pemba saa 5:45.
Baada ya kushuka katika Ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL),
alipokewa na mamia ya mashabiki wake waliokuwa wakiimba:
“Anamereta...,”

Wengi wa mashabiki hao walikuwa wamevaa fulana nyeusi zilizoandikwa
‘Anti Virus’ na mara baada ya kuteremka katika ndege hiyo, alitumia
takriban dakika 20 kusubiri kutoka nje ya uwanja katika kile
kilichoelezwa na uongozi wa uwanja huo kuwa ni kuandaa mazingira ya
usalama kutokana na umati mkubwa wa watu uliokuwa umekwenda kumlaki.
Mbali na ulinzi huo wa polisi, mapokezi hayo yalikuwa na zaidi ya
pikipiki 85, magari 30 na umati wa watu. Hata hivyo, katika hali
isiyokuwa ya kawaida wananchi hao waliimba nyimbo mbalimbali bila
kukitaja CUF kama ilivyozoeleka.

Nyimbo zilizokuwa zikiimbwa katika mkusanyiko huo zilikuwa ni za sifa
kwa mbunge huyo... “Hamad anameremeta... tumpambe maua... Hamad ni
nuru ya Wawi... hao vibua macho wanataka kushindana na Hamad hawawezi
haoooo na mwingine ukisema Maalim Seif, Serikali ya mseto haikufanya
kitu, tunataka mabadiliko.”

Ilipotimu saa 6:15, msafara wake ulielekea hadi katika Uwanja wa soka
wa Ditia, ulioko katika Jimbo hilo la Wawi ambako Hamad alihutubia.
Hata hivyo, tofauti na ilivyokuwa siku za awali, hakuna bendera ya CUF
iliyokuwa ikipepea mbali na ile ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.

Akizungumza katika mkutano huo, Hamad alisema alishaambiwa na baba
yake kwamba atapambana na ugumu katika maisha ya kisiasa kwa kuwa
anasimamia haki na ukweli.
“Marehemu baba yangu aliniambia katika siasa yatakukuta mambo manne
ambayo ni kufukuzwa katika chama, fitina na mwenzangu aliyeshika
mpini, kuwekwa ndani na kupigwa risasi katika hayo yote yameshanitokea
kasoro moja la kupigwa risasi,” alisema Hamad.
Alisema Maalim Seif akisema ndiye chanzo cha migogoro yote ndani ya
chama hicho: “Namuheshimu sana Maalim lakini uvumilivu umenishinda
dhambi tuliyoifanya kubwa wanachama wa CUF ni kumfanya Maalim Seif
kama malaika hana dhambi na hakosei kitu chochote na harekebishwi na
wanachama wengine.”

“Kama yeye ni hodari wa kutoa taarifa, aje atoe sababu ya kuweka
mageti ya kuzuia kuingia karafuu katika barabara zote wakati aliahidi
katika kampeni kwamba biashara ya zao la karafuu itakuwa huru.
Anashindwa kupita kwenye njia zake alizoziahidi, anatumia nafasi yake
kuharibu chama na kupandikiza chuki kwa watu.”
Mmoja wa wakazi wa Wawi, Khamis Baharani alisema wakazi wengi wa jimbo
hilo wamestushwa na kufadhaishwa na uamuzi wa Baraza Kuu la Uongozi la
CUF wa kuwafukuza wanachama watatu na wengine wanane kupewa karipio
bila wao kushirikishwa.

Baharani alisema Hamad ni mbunge wao na kwamba wanaamini amefanya
mambo mengi ya maendeleo na mazuri katika utumishi wake jimbo ni kwao
hivyo ingekuwa vyema wakashirikishwa katika hatua hiyo kubwa
iliyochukuliwa dhidi yake.
 
si aje chadema aje kuwa makamu wa raisi mwaka 2015 ila akija ajue anakuja kwa watu wenye nia ya kweli ya ukombozi kwa watanzania
 
si aje chadema aje kuwa makamu wa raisi mwaka 2015 ila akija ajue anakuja kwa watu wenye nia ya kweli ya ukombozi kwa watanzania

Itategemea kama Muungano bado utakuwepo mwaka 2015.
Lakini mleta mada si heri tuu angesema "Hamad Rashid atikisa Pemba".
Maana kichwa cha thread kimekaa kimbea.
 
si aje chadema aje kuwa makamu wa raisi mwaka 2015 ila akija ajue anakuja kwa watu wenye nia ya kweli ya ukombozi kwa watanzania
Mkuu mimi si mwanachama wa Chadema, lkn natumaini kuwa unatania! Hamad aende Chadema kwa sababu ya umati wa wafuasi wake pemba au kwa sababu ni mwadilifu na ana maono na misimamo sawa na Chadema?!
 
Kavinunua vyombo vya habari vimkweze, wewe hujaskiliza Zenj Fm tangu jana ukifungua radio anatajwa yeye tu! Lakini la msingi ieleweke kama 'Ustadh' huyu anajimaliza kisiasa. Ukiona mtu anatumia hadi speed ya mwisho katika kulifanya jambo jua hana hatua atakayoifika tena, hata mgonjwa utakapomuona anatumia punzi nyingi jua kifo hakiko mbali.
 
Kagawa bahasha huyo
 
si aje chadema aje kuwa makamu wa raisi mwaka 2015 ila akija ajue anakuja kwa watu wenye nia ya kweli ya ukombozi kwa watanzania

Hatumtaki HR in mnafiki katakana sera zetu, Hatufai. Labda awe mwanachama tu an Hulu tukiendelea Kim hunguza
 
Hatumtaki HR in mnafiki katakana sera zetu, Hatufai. Labda awe mwanachama tu an Hulu tukiendelea Kim hunguza
.

Mbona unazungumza as if hiyo CDM ni mali yako na umeiweka mfukoni kaka, chunga maneno yako na wakati huo huo kumbuka siasa ni mchezo mchafu.
 
Itategemea kama Muungano bado utakuwepo mwaka 2015.
Lakini mleta mada si heri tuu angesema "Hamad Rashid atikisa Pemba".
Maana kichwa cha thread kimekaa kimbea.

Mkuu EMT nitake radhi mie nimesema hivimaana nimeshangaa na makelele juu ya HR na matukio yaohuko Pemba .Nimeshangaa hata nashangaa .HiviMtatiro uko wapi uje uniweke sawa inawezekanaje huyu apokewe kishujaa ?
 
Tatizo la Hamad Siasa zake ni za kifitina, ni vigumu kumhold na kumcontrol kwahiyo Chama chochote kikimpata itakuwa Vigumu kweli kumuambia mrengo wao wa yeye kuufuata, atabisha au atajiona zaidi ya wao hivyo itakuwa ni Mzigo...

Yeye ni kama Mrema hawezi kuwa Mwanachama wa Kawaida atataka kuwa zaidi the leader or something within the party

Kwahiyo ni Doa jeusi ndani ya chama chochote atakacho ingia Mwache aanzishe chama chake...
 
Mkuu Lunyungu hayo yaliyoandikwa ni kweli yametokea huko Pemba, hivyo usiwe na wasiwasi wa kufikiri kuwa labda unaota, hauoti na yameweza kutokea kwa sababu Hamad Rashid ni mtu wao.

Ushauri wa bure kwenu, mkimrecrut ajoin chama chenu, then mtajipatia angalau jimbo moja la uchaguzi huko Pemba kwenye by election ya jimbo la Wawi!.
 
Tatizo la Hamad Siasa zake ni za kifitina, ni vigumu kumhold na kumcontrol kwahiyo Chama chochote kikimpata itakuwa Vigumu kweli kumuambia mrengo wao wa yeye kuufuata, atabisha au atajiona zaidi ya wao hivyo itakuwa ni Mzigo...

Yeye ni kama Mrema hawezi kuwa Mwanachama wa Kawaida atataka kuwa zaidi the leader or something within the party

Kwahiyo ni Doa jeusi ndani ya chama chochote atakacho ingia Mwache aanzishe chama chake...
Mkuu Nngu007, Hamad Rashid bado ni asset ambayo Chadema wakiweza kui capture wanaibomoa CUF left, right na center pale Wawi!. Siasa za Pemba ni watu sio vyama kama alivyo Mrema kule Vunjo au Ndesa pale Moshi mjini. Mrema na Ndesa wao sasa wameshajichokea hivyo they are spent force na 2015 hawatasimama, ila whoever watakao washika mkono kuwa ndio wanawaletea ndio watakao yatwaa majimbo yao kutokana na goodwill yao!.

Hamad Rashid anakubalika sana Wawi ila Maalim Seif anaabudiwa kama mungu mtu, hivyo ndani ya CUF Wawi kuna wana CUF wengi wanamuunga mkono Hamad ila hawawezi kujionyesha kwa sababu siasa za Pemba ni kama dini!. Ili chama kama Chadema kupenyeza mguu Pemba lazima kutumia karata dume kama Hamad kuwadhihishia wana CUF kuwa Maalim sii mungu ni just a human and can make mistakes!.
 
sisi wapemba tunajuwa tunachofanya na tunachotaka ,huyo Hamad Rashid kaja na wabongo kiyama kachukua maCCM WA PEMBA yote hatubabaishi kaleta CCM kutoka Tanga.MAPALALA ALIPOKEWA NA AKAFANYA MKUTANO MKUBWA ZANZIBAR,Naila Jidawi aliendelea kuwa mbunge wa mahakama,Asha Ngde na wenziwe watatu walikuwa wabunge wa viti maalum walifukuzwa na kubaki wa mahakama,Ramadhan Mzee ,NYARUBA,Mohammed wankwao(hwang kwo),MAREHEMU NAMATA,Salim Msabbah na wengineo mbali na waliokimbiliaCCM hawana mpango wowote wanatamani kurejea CUF ITAKUWA hamad rashid?
 
Hizo tisheti nyeusi za ANTIVIRUS ni zile za Sugu au? Kama ndivyo hongera Mr. II kwa kukuza brand yako naona hadi kwenye politics iko functional.... Lakini mambo ya wapemba hayanihusu..
 
hamad kakumbuka ubaya wa maalim baada ya kumng'oa madaraka yote? alikuwa wapi siku zote?
 
sisi wapemba tunajuwa tunachofanya na tunachotaka ,huyo Hamad Rashid kaja na wabongo kiyama kachukua maCCM WA PEMBA yote hatubabaishi kaleta CCM kutoka Tanga.MAPALALA ALIPOKEWA NA AKAFANYA MKUTANO MKUBWA ZANZIBAR,Naila Jidawi aliendelea kuwa mbunge wa mahakama,Asha Ngde na wenziwe watatu walikuwa wabunge wa viti maalum walifukuzwa na kubaki wa mahakama,Ramadhan Mzee ,NYARUBA,Mohammed wankwao(hwang kwo),MAREHEMU NAMATA,Salim Msabbah na wengineo mbali na waliokimbiliaCCM hawana mpango wowote wanatamani kurejea CUF ITAKUWA hamad rashid?

Si ajabu ukatuambia hata askari polisi waliokjuwa wanalinda msfara wake alitoka nao bara.

Kitu nachoshindwa kuwaelewa wwanacuf sasahivi wanapomzungumzia hamad rashid baada ya hili sakata la kumtimua, ni kujaribu kwa kila namna kumnasibisha na bara, kwamba wapemba wenzake hawamkubali, kila anachokifanya lazima wakihusishe na bara.

Lakini muda si mrefu tutajua mbivu na mbichi, aidha hamad anakubalika wawi ama hakubaliki.
 
Back
Top Bottom