Wakuu kuna umuhimu wowote mume kula chakula cha nyumbani!

Akili Unazo!

JF-Expert Member
Feb 18, 2009
3,930
4,893
Wakuu naomba munisaidie kuhusu hili suala je kuna umuhimu au kuna ulazima wowote wa mume pindi atokapo kazini au safarini kula chakula cha nyumbani hata kama ameshiba au hajisiki kula?

Hapa naongelea kuwa mume anawajibika kuhakikisha kuwa kila kinachohitajika nyumbani kipo na hakuna mapungufu yoyote?
 
...yap!

alichoandaliwa ni muhimu na lazima ale au angalau aonje hata kama watapewa watoto, au itabidi kifunikwe ili kiliwe baadae!
 
umuhimu upo tena sana kwani kuhakikisha kuwa kila kitu nyumbani kipo sio mwisho wa wewe kula nyumbani unapotoka kazini au safari. Maisha yangekuwa hivyo kuwa ukishahakikisha kuwa kila kitu kipo ndani then uwajibiki tena kuvitumia basi maisha yangekuwa na raha sana kwa wale wenye nyumba ndogo manake wangenunua kila kitu huku kwa bi mkubwa halafu mchezo unatoka, yeye akitoka kazini anapitia nyumba ndogo anakula na kuoga kabisa kwa bi mkubwa kunakuwa kama hosteli ni kulala na kubadilisha nguo tu. Umuhimu upo tena sana ndg yangu
 
Hakuna ulazima unapiga cmu tu kuwa wasikuandalie msosi
Ukijilazimisha unaweza kutapika
 
Wakuu naomba munisaidie kuhusu hili suala je kuna umuhimu au kuna ulazima wowote wa mume pindi atokapo kazini au safarini kula chakula cha nyumbani hata kama ameshiba au hajisiki kula?

Hapa naongelea kuwa mume anawajibika kuhakikisha kuwa kila kinachohitajika nyumbani kipo na hakuna mapungufu yoyote?

Inategemea, labda kala wakati yuko safarini, lakini kama katoka kazini na kila siku ana tabia ya kukikacha chakula cha nyumbani basi hapo kuna neno kubwa sana. Au anakula sehemu sehemu au anayakacha mapishi ya mkewe. Siku moja moja kutokula nyumbani si jambo la ajabu.
 
ila bana hata kama umechoka na umekula njiani, ukifika home na kupiga msosi wa wife au shori wako ni muhimu sana, coz inaonyesha furaha kua umerudi home na umepokelewa vizuri, we ukila huko safarini halafu useme umeshiba hapo hautaeleweka, inamaana hukua na hamu na nyjumbani?
 
...yap!

alichoandaliwa ni muhimu na lazima ale au angalau aonje hata kama watapewa watoto, au itabidi kifunikwe ili kiliwe baadae!

mie labda nitoke nae tukirudi huko ndio tunaweza/anaweza acle, akitoka mwenyewe kokote aendako akirudi chakula kinamuhusu.
 
ila bana hata kama umechoka na umekula njiani, ukifika home na kupiga msosi wa wife au shori wako ni muhimu sana, coz inaonyesha furaha kua umerudi home na umepokelewa vizuri, we ukila huko safarini halafu useme umeshiba hapo hautaeleweka, inamaana hukua na hamu na nyjumbani?

kuna wengine kama mie hapa mwanaume akijua upo nyumbani(hujasafiri)anataka umpikie, hataki kula chakula cha houseboy, umetoka job umechoka umpikie acje kula? haaa no way! atakula hata saa 9 ucku.
 
Du, mie nadhani usipokula watasema umekula nyumba ndogo, ni hilo tu. Sidhani kama wanapenda saaaana tulale tukiwa tumeshiba!!
 
Wakuu naomba munisaidie kuhusu hili suala je kuna umuhimu au kuna ulazima wowote wa mume pindi atokapo kazini au safarini kula chakula cha nyumbani hata kama ameshiba au hajisiki kula?

Hapa naongelea kuwa mume anawajibika kuhakikisha kuwa kila kinachohitajika nyumbani kipo na hakuna mapungufu yoyote?

Chakula kipi? maana vyakula vipo vingi ati? :D
 
Wakuu naomba munisaidie kuhusu hili suala je kuna umuhimu au kuna ulazima wowote wa mume pindi atokapo kazini au safarini kula chakula cha nyumbani hata kama ameshiba au hajisiki kula?

Hapa naongelea kuwa mume anawajibika kuhakikisha kuwa kila kinachohitajika nyumbani kipo na hakuna mapungufu yoyote?

Mume akirudi nyumbani anatakiwa kuonja hata kijiko kimoja. Hilo ni somo mume wangu alifundishwa na my father (baba mkwe wake) na alimuambia hiyo ni kwa "heshima ya mpishi". Hata kama umekula ulikotoka kuonja chakula ulichoandaliwa nyumbani ni Heshima, pia kijiko kimoja hakiwezi kuharibu shibe yako.
 
Mimi asipokula kesho yake hatokuta msosi mpaka atakapouulizia tena.
 
Baba ambaye ana mazoea ya kula nyumbani siku akisema ameshiba au hajisikii kula ni rahisi kueleweka. Tatizo ni pale baba anapokuwa na katabia ka kukacha kula nyumbani aidha ana sehemu nyingine anakula iwe nyumba ndogo au kwa mama ntilie (mapishi ya nyumbani hayamaindi). Kama tatizo ni mapishi si vibaya baba akaingia jikoni kuonyesha upikaji au mapishi vile anapenda.
 
Huwezi jua aliko toka kala nini njiani akichanganya na wa home unaweza shangaa mwenzio halali usiku tumbo limefuluga usiku kucha trip kibao WC.

ananijua vizuri, so hata akila wapi kama anataka tulale salama aje ale na home,hata vijiko viwili vitatu kuliko kuacha kabisa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom