Wakurugenzi 73 wa Halmashauri watimuliwa

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
WAKURUGENZI Watendaji (DED) wa Halmashauri mbalimbali nchini 73 wamefukuzwa kazi, 78 wanakabiliwa na kesi mahakamani, 33 wamesimamishwa na mmoja amestaafishwa kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha katika Halmashauri hizo, Bunge limefahamishwa leo.

Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Aggrey Mwanri amesema bungeni kuwa, hatua hizo zinatokana na ripoti za ukaguzi zilizotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG).

Bila kutaja Halmashauri husika, Mwanri alisema Tamisemi haitakuwa na mzaha katika kukabiliana na watumishi wabadhirifu wa fedha zinazokwenda katika Halmashauri nchini.

“Mheshimiwa Spika, tuko tayari kusahihishwa, lakini hatutamvumilia ye yote katika suala hilo kwa sababu Halmashauri zetu haziwezi kuendelea kugeuzwa shamba la bibi. Tamisemi itafanya fujo za kila aina katika Halmashauri ili kurekebisha hali hadi pale waheshimiwa wabunge mtakapotushika mkono kusema inatosha sasa,” ameeleza Mwanri.

Hata hivyo, amesema, ukaguzi wa CAG Ludovick Utouh katika Halmashauri umesaidia kuboresha hali, akitolea mfano kwamba mwaka uliopita, Halmashauri 78 zilipata hati safi isipokuwa moja ya Kilosa iliyopata hati chafu na mwaka huu, nne tu ndizo zimepata hati chafu.

Amezitaja Halmashauri hizo nne kuwa ni Rombo, Kishapu, Kilwa na Mwanga, huku akieleza kuwa CAG ataendelea na kazi ya kusafisha uozo huo na kwamba akigundua kuna ubadhirifu mahali, anayo mamlaka ya kuagiza wahusika wachukuliwe hatua za kinidhamu.

Naibu Waziri alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Regia Mtema (Chadema), aliyetaka kufahamu Serikali inachukua hatua gani kwa Halmashauri zilizopata hati zenye shaka au chafu.

Akijibu swali la nyongeza la Mtema, Naibu Waziri alisema CAG anakaguliwa na mshauri maalumu kwa uteuzi wa Wizara ya Fedha. Kuhusu swali jingine la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu, Diana Chilolo (CCM), Mwanri alisema serikali inazuia fedha za miradi ya maendeleo kwa Halmashauri zilizopata hati chafu kama njia mojawapo ya kuamsha hasira za madiwani ili wasikubali kupata hati hiyo.

“Si nia ya serikali kuwakomoa wananchi wake, lakini tunafanya hivyo ili kuamsha hasira za madiwani wasikubali Halmashauri zao kupata hati chafu,” alisema Mwanri na kutoa mfano wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga iliyozuiwa Sh bilioni moja za maendeleo kwa hati chafu.
 
duh hizi naomba ni kubwa sana kuna tatizo some where
sidhani kama kesi na kuwatimuwa ni suruhisho ila kukata mzizi wa fitina wa haya matatizo
ni kuondoa mamlaka ya mtu moja kuruhusu pesa ya umma atakavyo lakini pia
kuwa na viwango ya kitaifa kuhusu ulipwaji na ilipaji miradi ya maendeleo.
kama mfumo wa computer hautachukua nafasi hizi kesi zitakuwa common very soon
 
Back
Top Bottom