platozoom
JF-Expert Member
- Jan 24, 2012
- 9,366
- 11,154
Mimi sio mzee lakini napenda nyimbo za zamani kupita maelezo kuanzia za akina Mbaraka mwishehe,Marijani,Cuban marimba wengineo utaongezea.Unajua kwa nini nimezikumbuka leo? kuna wimbo umepigwa nikakumbuka kisa cha kama miaka 15 iliyopita.
Kuna mlevi mmoja alikuwa almaarufu mtaani kwa rafiki yangu,kila akilewa hujiimbia nyimbo za zamani anapotoka ulevini halafu hupita anapoishi huyo rafiki yangu(alikuwa amepanga) mida ya saa 3 hadi 5 usiku na kuelekea kwake kwa sababu hapo ilikuwepo njia. Kila anapopita mabinti wa mwenye nyumba ambao umri wao ni zaidi ya miaka 25 na ambao hawana kazi yeyote wanayofanya humcheka huyo mlevi na kumkejeli wakiwa wamekaa barazani kwao (walikuwa hawajaolewa na mapepe fulani hivi).
Siku ya siku yule mlevi akautandika mtindi kama kawaida na kupita huku akiimba wimbo huu wa zamani.............
Msichana wa sura aah nzuri..... nini kimekufanya usiolewe
Elimu unayo ya kutosha lakini bado hujaolewa
Wadogo wa nyuma yako wameolewa wamekuachaa.. ukihangaika
Ooh baby.usionyeshe majivuno kwa vijana,ukionyesha majivuno kwa vijana utabaki ukihangaika
oooh miaka yaenda sana na sura inachujuka......................
***********************************************
Wale mabinti waliposikia anaimba hivyo hawakumkejeli na waliufyata kuanzia siku hiyo.
Nafikiri alikuwa Daudi Kabaka huyu.Sijui nawe unakumbuka nyimbo yeyote ya zamani au bendi inayokukumbusha matukio ya raha na karaha..........................!
[h=1]Daudi Kabaka - Msichana sura Nzuri[/h]

Last edited by a moderator: