Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Baada ya kikundi cha watu wachache kujitengenezea mfumo wa posho kama mastahili ya kujikimu watu pekee ambao hawapokei posho japo ndio wanafanya kazi kubwa zaidi ni wakulima.
a. Mkulima anapolima mazao na kuyahifadhi anapata posho gani ya kufanya kazi yake kama mkulima? - farming allowance? alipwe na nani?
b. Mkulima anapopata upungufu wa mazao kutokana na hali mbaya ya hewa, soko n.k anapewa posho gani ya kujikimu kwa siku? Ili kumsaidia kumudu gharama za maisha? au hizi gharama za maisha zinawagusa watu wenye ajira rasmi tu?
c. Mkulima analeta mahindi, ndizi, nafaka nyingine, matunda hadi kwenye masoko makubwa say Kariako, Tandale n.k au Ngamiani pale Tanga je anapoouza mazao hayo analipwa posho ya kusafirisha (transportation allowance); je anaweza kudai "transportation allowance" au yeye anabeba gharama ya kusafirisha na kuiingiza kwenye bei ya vitu anavyouza? Vipi allowance ya vikao vya majadiliano ya bei (negotiation allowance) kwa muda anaotumia kufanya dili na wanunuzi?
d. Mkulima wetu huyu ambaye tunaambiwa ndiye anayeshikilia nchi kwa jasho lake anapotumia usafiri wake kuleta mazao kutoka shambani hadi sokoni au kwenye sehemu ya mauzo analipwa posho ya mafuta (gas allowance)? Au hatujali mazao hayo yanafikishwaje sokoni?
e. Hakuna kazi ngumu kama ukulima hasa ukulima wetu ambao bado unategemea sana jembe la mkono. Maandalizi ya shamba, kulima, kulinda mazao na hata kuja kuvuna ni kweli ni kazi ya "jasho" la mtu literally. Lakini mbona wanapoenda kuuza hasa wanapoiuzia serikali kwanini pamoja na kununua mazao serikali haiwalipi hardship allowance? Au wao hawastahili?
Ninachouliza hasa ni kuwa kwanini ni watumishi walioajiriwa katika sekta rasmi tu ndio wanalipwa hizi allowance ambazo hawataki kuziachia? Wakulima wetu mbona hata ruzuku hawapati (wenyewe wanapewa vocha! siyo fedha!). Kwanini hatuwapi ruzuku wakulima - ya fedha au allowance kusaidia kumudu maisha yao kama tunavyowapa watumishi wa umma na hata wengine wa sekta binafsi ambao tunaambiwa ati maisha ni magumu kweli kwao? Hivi wakulima wa Tanzania wanapata maisha mazuri kuliko ya watu wengine?
Jamani vipi kuhusu wanakijiji wenzangu wakulima? Tunawapa ahueni ipi katika mapato yao? au ndio yale yale "tutaboresha soko la mazao yetu ili wakulima wapate bei bora za mazao?".. Really? Au ni kwa sababu wao hawana uwezo wa kuiba waziwazi kama hawa wengine?