Wakulima tunaotegemea Mvua msimu ndio huu tukutane hapa tujadiliane

Kwetu mpaka leo mvua hata tone moja halijaonekana
na serikali haitoi chakula cha msaada acha tuisome na sisi tutawasomesha 2020 sio mbali panapo majaaliwa
 
vipi kuhusu viazi vitamu kama mvua ni chache inawezekana?
Viazi vitamu ama mihogo yawezekana ndio chaguo sahihi kulingana na mvua zilizopo. Hofu ni kwamba mazao hayo hasa viazi mara nyingi hulimwa kwa ajili ya chakula na sio biashara. Sasa sifahamu lengo lako ni lipi?
 
Nataka nilime viazi lishe aina ya carroti kibiashara mkuu..
 
Wakulima wenzangu pia kuna kilimo cha mbegu za vitunguu ni kilimo kinachotoa sana kama mtu ukiwa siriazi ila ni kilimo kinacholimwa wakati wa kiangazi kwani ni kilimo cha umwagiliaji ukilima hekari tano tu. tayari ushapata mtaji kwani katika hekari 5 una uhakika wa kupata debe 60 na debe moja huuzwa mpka laki 6, na bei ya chini ni shilingi laki 3. hivyo katika kilimo hua tunapigia bei ya chini. sasa fanya laki 3 mara 300. ni shilingi Milioni 90
ila mtaji wa kilimo hiki kwa hizo hekari 5 sio chini ya milion 10. na upate eneo lisilokua na asili ya chumvi chumvi, na gharama za uendeshaji sio kubwa kwani unamwagilia maji ya kutosha kwa mwezi ni mara 2 mpaka 3 na sio zaidi ya hapo.
 
Mdau,hivi kulima kitunguu wakati wa mvua(sio cha mbegu)inawezekana?na kama inawezekana ni mambo gani ya kuzingatia hasa kulima msimu huo.
 
Kwa shinyanga ni kulima hasa mtama, alizet, pamba, choroko, uwele na mengine yanayositahimili ukame
 
Kweli mvua ilikuwa haba lkn mimi nililima mahindi ya njano ile mbegu ya Thailand niliambulia kidogo nilichojifunza hii mbegu inavumilia ukame.
hyo mbegu inajpatikana wapi na je pato lake likoje kwa eka kukiwa na mvua nakm kuna mvua chache pato lake likoje kwa eka?msda pls,
 
Kweli mvua ilikuwa haba lkn mimi nililima mahindi ya njano ile mbegu ya Thailand niliambulia kidogo nilichojifunza hii mbegu inavumilia ukame.
hyo mbegu inajpatikana wapi na je pato lake likoje kwa eka kukiwa na mvua nakm kuna mvua chache pato lake likoje kwa eka?msda pls,nasoko Lake Lipoje?
 
Kwa kweli sijui bei ikoje?
maana mimi nililima hayo ya njano na meupe lkn meupe nilivuna kidogo kutokana na hali ya ukame mwaka huu.
hayo ya njano ndio nilipata na mengi.
sasa ndio nataka kulima ya biashara.
Vp Pato Lake Kwa Eka Km Kuna Ukame Napia Km Kuna Mvua Yakutosha,
 
Mdau,hivi kulima kitunguu wakati wa mvua(sio cha mbegu)inawezekana?na kama inawezekana ni mambo gani ya kuzingatia hasa kulima msimu huo.

kitunguu cha kawaida nisikufiche mdau mwenzangu ni kilimo kizuri sana, hasa kipandwe maeneo ya mbuga, pia kitunguu hiki kinahitaji mvua lakini sio mvua ya kuzidi hasa kwa mbegu hizi za kisasa kama red cleore, na nyingine kama hizo, kama mvua ni kubwa maeneo yako wataalama wanatushauri tupande kitunguu aina ya kaki, lakini kitunguu hiki mavuno yake sio mengi kama red cleore ambacho kina soko kenye, uganda, na hata comoro na mavuno yake kama utapanda kwa kufuata taratibu na kanuni za upandani kwa hekari utapata mpaka gunia 90 za kilo 100.

mambo ya kuzingatia
japo ni gharama

otesha mbegu zako katika kitalu maalum za kutosha hekari unazohitaji
safisha shamba lako vizuri pia ukitumia dawa ya kukausha nyasi ni vyema kwani pia hurutubisha shamba,
pitisha trekta kwa mara ya kwanza kabla mvua haijanyesha, pia mvua ya kwanza ikinyesha pitisha haro, kwa kutumia ng'ombe au hata trekta ili kuifanya ardhi isiwe katika hali ya ugumu. then tengeneza vitalu na vichimbie mashimo kwa ajili ya kuja kupandikiza mbegu ambazo ushaziotesha kwenye kitalu hapo kabla. then ukimaliza panda, na uanze kuwa unaziangalia maendeleo yake, ni kilimo kina gharama, lakini kupata ni majaaliwa yeke mungu.

pia kuna njia nyingine ya kumwaga mbegu moja kwa moja ila mavuno yake ni gunia 30 mpaka 40 na ikishuka ni 20. yenyewe unapandia ngo'ombe au trekta.

ila ni bora ukalima kitunguu cha kiangazi kama maeneo yako ya karibu kuna maji ya kutosha. kitunguu kinasoko, japo mkulima wa kitunguu ni sawa na mtuhumiwa anayesubiria hukumu mahakamani.

kwa uelewe wangu mchache napenda kuishia hapo
 
hyo mbegu inajpatikana wapi na je pato lake likoje kwa eka kukiwa na mvua nakm kuna mvua chache pato lake likoje kwa eka?msda pls,nasoko Lake Lipoje?
Hiyo mbegu ina mavuno mengi nimewahi lima nilipata 39 gunia kwa heka!! Pili inavumilia sana ukame.
 
Wakulima wenzangu pia kuna kilimo cha mbegu za vitunguu ni kilimo kinachotoa sana kama mtu ukiwa siriazi ila ni kilimo kinacholimwa wakati wa kiangazi kwani ni kilimo cha umwagiliaji ukilima hekari tano tu. tayari ushapata mtaji kwani katika hekari 5 una uhakika wa kupata debe 60 na debe moja huuzwa mpka laki 6, na bei ya chini ni shilingi laki 3. hivyo katika kilimo hua tunapigia bei ya chini. sasa fanya laki 3 mara 300. ni shilingi Milioni 90
ila mtaji wa kilimo hiki kwa hizo hekari 5 sio chini ya milion 10. na upate eneo lisilokua na asili ya chumvi chumvi, na gharama za uendeshaji sio kubwa kwani unamwagilia maji ya kutosha kwa mwezi ni mara 2 mpaka 3 na sio zaidi ya hapo.
Mkuu nimewahi waza hivyo aisee naomba hints zaidi hizo mbegu nazipataje na zinachua muda gani?
 
Kiukweli kilimo cha kuangalia mawingu angani kina presha sana. Nimepanda Mihogo ekari 8 wilaya ya Kisarawe maeneo ya Kisanga, mvua ilinyesha mara moja tu kwa sasa ni jua kali....
 
Back
Top Bottom