Wakubwa wenzangu Tusaidiane mawazo hapa

KGB

Member
Sep 2, 2010
52
6
Card ya Mwaliko wa Harusi ya rafiki yake wife ime kuja kwa Jina lake e.g Rose Sungura Instead ya Ku elekezwa kama ilivyo Desturi MR&MRS Lameck Ngofisi.Sasa Mimi Nimechomoa kwamba siendi kwa kuwa mwaliko ni wa wife peke yake na ndo maana imeelekezwa kwake,Ila wife analalama sitendi haki sababu Rafiki yake hakujua Jina langu na kwasababu haijakatwa popote inamaanisha ni yetu pamoja.......

Nakumbuka kipindi cha harusi yangu wake za watu ambao kwa namna moja ama nyingine ni marafiki ila sifahamu majina ya waume zao nilikuwa nikiwapigia simu kuwauliza ungependa niku address vipi ?

Je wadau kwa Taratibu za kiafrika Hii imekaaje?Kwanini Mtu amadress Mke wa mtu kwa Jina lake,Kwanini kama ulichukua mchango usiulize pia Card iandikweje au tunachojali ni mchango tu?
 
mimi nishaacha kuchangia harusi na wala siendagi! ila mawazo yangu henda alipitiwa, hivyo nenda tu haina noma mkubwa!
 
Nadhani atakua amepitiwa tu. Mimi nakushauli nenda na wala usiwe na kinyongo chochote. Kagonge Bia na Kuku mzee, Usipende kuchunguza kila kitu. Ila maamuzi ya mwisho unayo mwenyewe, hata kama tutakushauli. Kama vipi kuwa Mafia tu.
 
nenda nae usipoenda akichakachuliwa usije lalamika!utashanga kwenye sherehe katoka kabla ya zawadi lakini home kaja saa 7
 
mnh utakuwa na gubu na wewe,
yaani usiende kny harusi kisa jina lako halikuwepo???
how close ulikuwa na huyo mwenye harusi?
hauoni unamlet down?:embarrassed:
 
mmmhhh sijajuaga vitu kama hivi vinawaingia wanaume...
kwa sababu wanaume hawachkuagi notice ya vitu vidogo vidogo kama hivyo...
 
nyie ndo wale wale lazima mpenyeze shingo hata kwenye vitobo ili watu wajue mpo jiamini mwanaume nenda na mkeo kwani kila mtu anayemjua mkeo anakujua au ana interest ya kukufahamu kwa sababu hata mie na mashoga kibao lakini huwa sinaga muda wa kujua waume zao labda kama anatumia jina la mume
 
mimi niliwahi kufanyiwa kitendo km hicho nikamwambia wife kuwa kama hiyo kadi inanihusu na mimi basi airudishe kwa aliyeandika ili ikabadilishwe huko, ili hao watu wajue ameolewa na yuko chini ya mume. Toka hapo sijakumbana na tatizo hilo, wife mwenyewe akiona discrepancy kwenye majina anahangaika nayo kabla ya kuifikisha kwangu...ni kuwa ngangari kidogo tu, kwisha.
 
mimi niliwahi kufanyiwa kitendo km hicho nikamwambia wife kuwa kama hiyo kadi inanihusu na mimi basi airudishe kwa aliyeandika ili ikabadilishwe huko, ili hao watu wajue ameolewa na yuko chini ya mume. Toka hapo sijakumbana na tatizo hilo, wife mwenyewe akiona discrepancy kwenye majina anahangaika nayo kabla ya kuifikisha kwangu...ni kuwa ngangari kidogo tu, kwisha.
Sidai tukul....
 
Back
Top Bottom