Wakubalieni wapenzi wenu wanachotaka.

kakuruvi

JF-Expert Member
Sep 2, 2009
770
256
Ili mapenzi yanoge, kuna wakati tu utalazimika kufanya kile anachopenda Mwandani wako japo kwa kujikosha.
Kuna Kaka mmoja toka Pemba alioa mke huku Bara, Mpemba alianza kunywa pombe lakini haziwezi, kila akinywa vituko. Mke wake alimsihi sana kila mara bila mafanikio. Siku moja jamaa aliutwika, aliporejea nyumbani mkewe kwa hasira akatandika chini alale ili kuepuka bughudha. Jamaa alianza fujo bila sababu kila saa anamwamsha mkewe, ilipofika saa saba usiku...
Mpemba: ''Nke angu, Nke angu''
Mke: (huku akiwa na hasira) ''Sitaki tabu, kila nikikuonya uache pombe hutaki, nami sitaki usumbufu, kwani wataka nini?''
Mpemba: ''Nsindikize nkakhojoe''
Mke: ''Nenda mwenyewe pombe tumekunywa wote kwani?''
Mpemba: (Kwa unyonge akajikongoja kwenda msalani) ''Sawa hunipendi, pombe siachi''
akajisaidia na mara akarejea
Mpemba: (Huku akiwa na furaha yenye mshangao) ''Nke angu, Nke angu"
Mke: (huku akiwa na hasira kuliko mwanzo) ''sitaki kuitwa hebu lala huko pombe huziwezi"
Mpemba: ''si hivyo Nke angu nimekutana na maajabu nsalani"
Mke: (huku akishawishika kujua nini kimempata mumewe mlevi) ''Maajabu gani Mume wangu''
Mpemba: ''Nke angu, ile nnafungua nlango wa choo tu, taa ikawaka, nkajisaidia, ile nnafunga tu nlango, taa ikazima yenyewe''
Mke: (huku akiwa na hasira kuliko mara ya kwanza na ya pili, aligunda jambo na alifoka) ''Nilikuambia mimi, kuwa pombe huziwezi, ndio umeshakojoa kwenye friji hivyo, pumbavu mkubwa wee''
Jamaa angemsikiliza Mkewe yote haya yasingetokea.
 
Back
Top Bottom