Wakongwe wa magari msaada tafadhali

Mi nadhani ulaji wa mafuta wa gari unategemea sana ukandamizaji wako wa accelerator,mfano wakati wa kuondoka kama uondokaji wako ni wa zaidi ya 3000rpm lazima ikulie mafuta tu hata kama unatumia gari zenye engine za VVTi.
 
Hapa ndio nnaposhindwa kuwaelewa watanzania!kipindi napanga kuchukua gx100 napo maneno yalikua mengi tu kuhusu ulaji wa mafuta lakini baada ya kuchukua mpaka sasa nnakaribia mwaka wa pili sasa naliona la kawaida tu!cha msingi ukitaka kufanya kitu fanya kwa manufaa yako ila ukisikiliza waswahili hutofanya lolote
 
ni gari nzuri, confortable, stable on the road so ni nzuri kusafiri pia. engine yake ni 1G-FE VVTI inatumia technology nzuri kwenye uchomaji wa mafuta. ulaji mkubwa wa mafuta unakuwa unavyokua kati ya 80km/hr ma 100 km/hr spidi ya juu ya hapo fuel efficiency inakua nzuri tena. kwa mfano ukijua kubalance mafuta unaweza tumia full tank moja ukasafiri Dar to Arusha. However ukipata nayo ajali hata kama vifaa vya bodi uki replace bado itaonyesha kwa mbali unless upate mechanic mzuri sana. Usipolitunza kimuonekano linapoteza mvuto mapema sana. spares zake za steering system eg rack ends stabilizer links, wishbone bushes etc zinabei average ambazo mtu wa kipato cha kati atazimudu. on safari usipokuwa makini unajistukia tayari ume clock 180 kms/hr speed ambayo ni top speed kwa gx 110. niliwahi kuwa nayo kwa miezi kadhaa mwaka 2010 so naongea kutokana na experience. ni hayo tu mkuu.
 
Hapo kuna mawili hiyo mark grand 110 ina engine ya 1G FE ambayo ni vvti na 2JZ FSE D4 na Vvti.

So sijajua mdau anataka kuchukua yenye engine gani hapo??.

Na kuhusu mafuta watu wengi wanajidanganya na kuongopa sana kila siku wanasema gari flani inakula sana mafuta bila kuwa na ushahidi.

Mfano mazda rx8 ni gari yenye cc ndogo lkn inabwia mafuta kama v8 tuu.

Anayesema kuwa hiyo gari ukiwa nayo inabidi uwe na shell ndani atoe ufafanuzi wauutumiaji wa mafuta na utofauti wa gari nyingine ya four
 
Back
Top Bottom