Wakipinga kuvurugwa Upinzani Bungeni; CHADEMA watoka nje!

Topical,

Nadhani walitoka kuonyesha kuwa wanapinga hoja ya kulazimishwa kuungana na vyama ambavyo si vya upinzani kivitendo. Kurudi kwao ndani ya ukumbi ni kutimiza kazi waliyotumwa na wananchi (waajiri wao). Posho ni haki ya kila mbunge, hata wale wasiohudhuria leo watapewa...

Hii kususa nusu nusu ni dalili ya unafiki

Shika moja susa au pambana kwa hoja period!
 
ndo mana 2najua chademu co chama mana wana2zingua 2uu wewe kila cku wanatoka nje wanamaana gan kama co cfa hakuna chama hapo kuna kuchanganyana 2uu hapo

Just do your home, usiishie hapo mkuu. Jaribu kuangalia mbele zaidi labda uniambie wewe ni CCM A or B hapo nitakuunga mkono.
 
ndo mana 2najua chademu co chama mana wana2zingua 2uu wewe kila cku wanatoka njewanamaana gan kama co cfa hakuna chama hapo kuna kuchanganyana 2uu hapo
Nadhani CDM wanahitaji kiongozi makini na mwenye busara sio huyu Mbowe, mwenye kutawaliwa na hasira, chuki na jazba.
 
..hii kanuni kwanini ilipitishwa wakati wa bunge lililopita?

..kwanini wanaikataa kanuni hiyo wakati wa bunge hili?

..hivi watakuwa wanabadilisha kanuni kila bunge jipya linapoanza kazi?
 
CCM bado inaweweseka na CHADEMA; lengo lau ni kutaka kuudhoofisha upinzani. Kama CCM wanasema kuwa sasa kampeni zimeisha na ushindani uhamie bungeni basi waache kanuni za bunge kama zilivyokuwa na kama upinzani watakubaliana kwa ridhaa yao kama kanuni inavyosema basi wataleta hoja ya mabadiliko hao. Vinginevyo ninaomba Chadema waachane na kambi ya upinzani bungeni wao wawakilishe wananchi wao tu na kambi hiyo ihamie mitaani kwenye kuongoza maandamano na mikutano kila wiki end nchi nzima mpaka 2015.
 
tutaangalia kesho kama hawatahudhuria, tukiwaona tutajua hii ni janja ya kuuma na kupulizia!

nimegundua kuwa wewe ni mshabiki mzuri ambae nadhani una urafiki na Kibonde (au watu wenye akili kama za kibonde) au unatumia muda mwingi kumsikiliza kibonde bila ya kufanya tafakari ya unachokisikia.

sasa naomba nikueleweshe kidogo. umezaliwa umezikuta sheria zinazokuongoza, hukuzitunga wewe lakini kwa kuwa umezikuta huna budi kuzifuata. walichokifanya CHADEMA leo ni kutoshiriki kupitisha kanuni Kandamizi lakini ikipitishwa bila ya wao kuwepo wakija wakaikuta ipo hawana jinsi itabidi waifuate. ugomvi wao haupo kwenye kuunda kambi moja na wenzao ila upo kwenye MISINGI ya KIMTAZAMO wa watu hao wanaotakiwa kushirikiana.na hadi naandika post hii tayari wamesharudi ukumbini.

kwahiyo natumai umenielewa ukiwaona kesho kwenye kikao wala usishangae na kupiga kelele.. Senkyu!
 
Tayari bunge limeshavunja kanuni na kuwaingiza wale wengine rasmi kwenye kambi ya upinzani bungeni...it is a pure sign of MANY DECISIONS AMBAZO ZIMEKUWA ZIKIFANYIKA FOR THE SAKE OF POLITICAL EXPEDIENCY. Hiki kitu ni kibaya sana

Tunafanya maamuzi makubwa kwa ajili ya manufaa ya kisiasa ya muda mfupi kwa maslahi ya watu/kikundi cha watu. Not for the country!!!!!!!!!!!! Nani aliyeturoga. CCM they are taking us to nowhere.

Anne Makinda si ndiye aliyesema hivi karibuni haiwezekani vyama vingine kuingia kuwa na kambi nyingine unless wawaombe CHADEMA!!!!
 
Nasikitika kusema wabunge wa CHADEMA, kwa mlolongo wa matendo yao,hawako kwa maslahi ya nchi hii......wako kwa maslahi yao binafsi na ya chama chao....ni watu wa kukurupuka,wasio heshimu mawazo ya wenzao na waliokosa mikakati sahihi ya ku-deal na wapinzani wao.....zaidi ni waongo kama CCM na CUF,ni wafitini na wachochezi sana.....kwa matendo yao si watu wa kuamini....lolote na liwe mradi wao washinde....hatufiki!!!! Bunge haliwezi kukaa kutimiza mapenzi ya CHADEMA watakalo ndo liwe,nasikitika kusema UPINZANI WENYE MASLAHI NA WATANZANIA HAUJAZALIWA TANZANIA........tuna wenye njaa na tamaa tu katika vyama vya siasa......nazidi kujihurumia na kuwahurumia watanzania,kwakuwa sasa nimeona hakuna mwema.......nakaribisha matusi.......ila sitashabikia nisichokiamini kwa kuogopa kutukanwa JF
 
MTM,
"WAanasiasa wote ni wanafiki"! Nadhani unawajibika kutoa utafiti uliokufikisha kwenye Conclusion hiyo.

Kwasababu matendo ya sirini (hidden) ni tofauti na yaliyo dhahiri

Hata wewe kumbuka siku moja nilikuuliza kwanini hamuungane na CUF ukasema wanasali sana

Nikakwambia does it matter! ukaanza siasa kukwepa hidden agenda zako..lol
 
ndiyo maana walimuweka huyo mama ili iwe lahisi kuwabana chadema . Walishajua ni moto na huyo mama ni lahisi kufuata maelekezo ya mafisadi.
 
MTM,
"WAanasiasa wote ni wanafiki"! Nadhani unawajibika kutoa utafiti uliokufikisha kwenye Conclusion hiyo.

Je, huyu kweli ni Dr. P.W. Slaa? Mbona siioni initial "P" kwenye jina? Any way, let me believe. Hata hivyo MTM ni nani? Kama ni mwenyewe mzee Dr. W. P.Slaa, basi niseme vijana wako watamfanya mama wa watu apate kifafa.....
 
Mbona wakati CUF wanaunda kambi yao ya upinzani hawakubadilishiwa vipengele iweje leo Chadema ndiyo wabadilishiwe kipengele iwe ushirikiano wa wabunge wote wa upinzani halafu what does this have to do with Spika wa Bunge kwanini yuko so concerned hapo ndio naanza kuamini kazi aliyotumwa huyu Mama Spika ameanza kuitekeleza vilivyo.
 
CCM wanataka kutengeua kanuni zote ambazo zinatoa mwelekeo wa kuleta Democrasia ndani ya Bungena ambazo zilikua zimesimamiwa vizuri na S.Sita, kwa minajiri ya kutaka kuonyesha kuwa Sita alikua wrong''
 
Nasikitika kusema wabunge wa CHADEMA, kwa mlolongo wa matendo yao,hawako kwa maslahi ya nchi hii......wako kwa maslahi yao binafsi na ya chama chao....ni watu wa kukurupuka,wasio heshimu mawazo ya wenzao na waliokosa mikakati sahihi ya ku-deal na wapinzani wao.....zaidi ni waongo kama CCM na CUF,ni wafitini na wachochezi sana.....kwa matendo yao si watu wa kuamini....lolote na liwe mradi wao washinde....hatufiki!!!! Bunge haliwezi kukaa kutimiza mapenzi ya CHADEMA watakalo ndo liwe,nasikitika kusema UPINZANI WENYE MASLAHI NA WATANZANIA HAUJAZALIWA TANZANIA........tuna wenye njaa na tamaa tu katika vyama vya siasa......nazidi kujihurumia na kuwahurumia watanzania,kwakuwa sasa nimeona hakuna mwema.......nakaribisha matusi.......ila sitashabikia nisichokiamini kwa kuogopa kutukanwa JF

Well said mkuu

Naanza kukuunga mkono moja kwa moja.
 
Dalili za wazi kuwa Makinda Bunge hataliweza zimeonekana siku ya kwanza tuu.
 
Back
Top Bottom