Wakili maarufu anadaiwa kuponza na ushauri

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,463
911,172
Wakili maarufu anadaiwa kuponza na ushauri
Send to a friend
Sunday, 07 August 2011 21:46


Mwandishi Wetu
IMEBAINIKA kukamatwa kwa wakili maarufu mkoani hapa na makachero wa polisi, kunatokana na ushauri wake wa kisheria aliotoa kwa wateja wake kuhusu utaratibu wa uanzishaji kampuni na kuwatambulisha benki kufungua akaunti.Akizungumza na gazeti hili jana, ofisa mmoja wa polisi alisema wakili huyo alitoa ushauri kwa wateja wake jinsi ya kuanzisha kampuni na aliwatambulisha benki ambako walifungua akaunti.

“Kinachomfanya ashikiliwe polisi ni kwamba wanataka awaonyeshe wale wateja wake aliowatambulisha mpaka benki na yeye anadai hafahamu walipo,” alidai ofisa huyo.Taarifa za awali zilidai wakili huyo alikutwa na kiasi hicho kikubwa cha fedha katika akaunti yake na kwamba, alipokamatwa kwenye gari lake zilikutwa Sh20 milioni.

Chanzo hicho cha habari kilipasha kuwa, akaunti ya kampuni hiyo aliyoshauri kufunguliwa ilikutwa na dola 500 za Marekani sawa Sh800,000, ambazo zilitumika kufungulia akaunti hiyo.Simu za wakili huyo zimekuwa hazipatikani tangu akamatwe na polisi Agosti 2, mwaka huu ingawa habari za uhakika zilisema aliachiwa kwa dhamana juzi jioni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye, alipoulizwa wiki iliyopita kuhusu taarifa za kukamatwa kwa wakili huyo, hakukiri wala kukataa zaidi ya kusema suala hilo liko ngazi za juu, hivyo hawezi kulizungumzia.
“Kwa kweli hilo suala liko juu ya ngazi yangu, siwezi kulizungumzia chochote kwa sasa hadi nipate idhini kutoka kwa wakubwa wangu,” alisema Andengenye.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) tawi la Arusha, Duncan Ooola, alikiri kukamatwa kwa wakili huyo na kwamba, walipofuatilia waliambiwa anachunguzwa na polisi.“Ni kweli wamemkamata Jumanne (wiki iliyopita), lakini sijui saa ngapi, tulikwenda polisi kujua chanzo walitwambia anachunguzwa, hiyo ndiyo taarifa ninayoweza kukupa,” alisema Ooola.
 
hivi huyu mwanasheria maarufu mbona hatajwi jina au hata magazeti yanamwogopa?
 
Alishatajwa jina mara kadhaa anaitwa Mwale...

Tusubiri uchunguzi ukamilike tujue hiyo account ina issue gani, na hayo mabililioni ni ya nini
 
Back
Top Bottom