Wakili: DOWANS itadhoofisha nchi

I agree with you in toatal Jamaa amenichefua hata ham ya gazeti 'tanzania daima' ikanitoka asubuhui asubuhi!!!

but now im begging to belive tanzania daima wamemchomkea huyo jamaa atapike

Kwenye gazeti la Tanzania Daima la Jana Kibanda nae ameongea kitu kama hiki cha Fungamtama, amemponda sana Sitta kwa kumlaumu waziri Ngeleja juu ya uamuzi wa kuwalipa Dowans.

Alimponda sana Sitta kusema kwa nini Ngeleja awe na maamuzi hayo kabla ya kikao cha baraza la mawaziri. Kibanda anamlaumu Sitta kwa kutoa siri za kikao cha baraza la mawaziri na anawaita wajinga wote wanaomsikiliza Sitta.

To me Sitta is not perfect lakini pale anapopigania haki hasa katika swala hili la Dowans namuunga mkono, i was a bit disappointed with Kibanda's rhetoric towards mzee Sitta.

Ntapost hiyo article a bit later.
 
Fungamtama huwa ni wakili wa Rostam soma hii habari

Fungamatama hapa anamtetea Mahanga Makongoro

Rev. Thanks. Nilikuwa nimeanza kuchanganyikiwa kwa tafsiri ya Huyu Fisadi II Wakili Kennedy. Sasa nimempata, anatetea maslahi ya Mteja wake wa Siku nyingi. Yuko kwenye Payroll la Rostam.
 
Kennedy Fungamtama, ameiomba serikali na umma upuuze ushauri wa aliyekuwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta, wa kutaka serikali kukataa kuilipa fidia ya sh bilioni 94 Kampuni ya kuzalisha umeme ya Dowans, kwani ushauri huo unaweza kulidhohofisha taifa kwa kuliingiza katika matatizo makubwa.

Mwanasheria huyo ambaye alimuelezea Sitta kuwa mtu anayejaribu kucheza na akili za Watanzania, kwa sababu ya kutojua kwao undani wa hukumu ya ICC, alisema endapo serikali itakaidi kulipa fidia hiyo ni wazi taifa linaweza kukabiliwa na madhara makubwa mawili:

>>>>Alisema moja ya madhara hayo ni kwa wafadhili kuiweka nchi kwenye orodha ya kunyimwa misaada, kwa sababu ya kutoheshimu sheria na mikataba ya kimataifa ambayo imeridhia.

>>>>Wakili huyo alisema madhara mengini ni pamoja na wawekezaji kuingiwa na hofu ya kuja kuwekeza hapa nchini na kuongeza kuwa hilo likitokea taifa ndilo litakalopata hasara na si Waziri Sitta binafsi.

Fungamtama alisema amefikia uamuzi wa kuzungumzia jambo hilo baada ya kuisoma

NIMEAMUA KUTANGULIZA '' NUKUU'' HIZO ILI WADAU MUONE JINSI NCHI YETU INAVYOLIWA!!!
ILI MPATE UCHUNGU WA KUWANGOA MAFISADI.
ILI MPATE UCHUNGU WA KUDAI HAKI ZENU ZINAZOIBWA
ILI MPATE KUJUA MAFISADI WENGINE WALIOJIFICHA
ILI MUAWATAMBUE MAFISADI WAPYA
ILI UCHUMI UNAPOYUMBA MJUE NANI WANACHANGIA
ILI MUWEZE KUJUA PUMBA NI ZIPI NA MCHELE NI UPI
ILI MUWEZE KUPIGANIA KUIRUDISHA MALI YA NCHI INAYOIBWA

NOTE; SITA SI MSAFI SANA LAKINI PALE ANAPOTETEA MASLAHI YA UMMA TUMUUNGE MKONO KWANI SWALA SI SIASA BALI MASLAHI YA UMMA
 
huyu nae amerukwa na akili na anatumika tu .......halafu huyu kubwa jinga pale magogoni amekalisha wala hasemi kitu...........mpuuzi kweli
 
Jamani mi niko ignorant kidogo na maswala ya TIC na BRELA kwa ujumla kuhusu usajili wa kampuni za nje Tanzania.

Kutokana na list iliyotajwa ya wamiliki wa Dowans kutoka BRELA, kama sijakosea, wote ni watu kutoka nje ya Tanzania.

Hivi inawezekana kweli kampuni ikasajiliwa BRELA ikiwa na wamiliki wote sio watanzania??? au inatakiwa atleast kuwepo na share holder mmoja ambaye ni Mtanzania????

Jamani naomba mnisaidie kwenye hili...
 
Kuna haja ya kufuatilia uraia wa wale wote wanaotetea kuilipa dowans
 
Jamani mi niko ignorant kidogo na maswala ya TIC na BRELA kwa ujumla kuhusu usajili wa kampuni za nje Tanzania.

Kutokana na list iliyotajwa ya wamiliki wa Dowans kutoka BRELA, kama sijakosea, wote ni watu kutoka nje ya Tanzania.

Hivi inawezekana kweli kampuni ikasajiliwa BRELA ikiwa na wamiliki wote sio watanzania??? au inatakiwa atleast kuwepo na share holder mmoja ambaye ni Mtanzania????

Jamani naomba mnisaidie kwenye hili...

Wapo japo Ngeleja kawaficha lakini Sitta alituambia ni wabunge watatu...wale wa Ngeleja ni wakurugenzi tu si lazima wawe wamiliki
 
Ukiaangalia arguments za huyo wakili mbuzi (mchumia tumbo) utagundua kwamba ametumwa kumsema Sitta kwa sababu kila alipokuwa anatoa maelezo hakusita kulitaja jina la sita. Kwa mtililiko huu utaona kuwa kuna kitu kinafichwa hapa. Hii hoja ya kupinga dowans kulipwa inasemwa na watu wengi sasa katika maelezo yake ameona wa kumshambulia ni sitta tu? Hapa ndopo unapokutana na wasomi wanaopaswa kufutiwa shahada zao kwani hawalisaidii taifa zaidi ya kulifilisi.
 
Mbona wazee wetu EAC hawajalipwa mpaka kesho na serikali imepuuzia huyu wakili hili analiona au hilo tu?
 
kwani wajameni nini chaa kushangaza hilo hawa wakina Fungamtama, Mtukama.... na wengineo ni wanafki wala si wa kuskiiza maana wao ndio wamejaa katika nafasi senior katika mawizara na kinachofanyika kila mtu anajua! Upupu tupu hawana credibility ya kukosoa uovu unaoendelea wao ndo wana draft, facilitate na wana-sign mikataba yoote feki! Kwa hiyo si cha ajabu wajameni
 
Ukiaangalia arguments za huyo wakili mbuzi (mchumia tumbo) utagundua kwamba ametumwa kumsema Sitta kwa sababu kila alipokuwa anatoa maelezo hakusita kulitaja jina la sita. Kwa mtililiko huu utaona kuwa kuna kitu kinafichwa hapa. Hii hoja ya kupinga dowans kulipwa inasemwa na watu wengi sasa katika maelezo yake ameona wa kumshambulia ni sitta tu? Hapa ndopo unapokutana na wasomi wanaopaswa kufutiwa shahada zao kwani hawalisaidii taifa zaidi ya kulifilisi.

Huyu wakili uchwala Kenedy kama ni wakili wa Rostam si ni yeye aliyetengeneza huo mkataba. Alijua huo ni mtego alingojea tu ufyatuke. Hebu wanasheria tafuta jinsi ya kuitoa Tanzania katika hili janga la Dowans. Tuwashitaki hawa jamaa kwa kutuingiza kwenye mikataba feki wakijua kuwa mwisho wa siku itabidi tuwalipe. Tutoke usingizini tuungane na Waziri Sitta kupinga huu ujinga. Huyu Bwn anapambana na Sitta kama vile kumnyamzisha!! Lakini wenye uchungu tuko wengi bado hatujalala na hizi fedha zisilipwe mpaka hoja hii ya hukumu ipelekwe Bungeni.
 
Kataeni kuwalipa muone yatayojiri. Mlishinikiza kuvunja mkataba sasa matokeo mnayaona.

Nyerere alijidai kuwataifisha LONRHO, ingawa taifisha yake ya Ma Benki na Mashamba Na Viwanda vya wazungu ilikuwa ya geresha kwani wote alikuwa akiwalipa, wote walilipwa, wasiolipwa ni waIslam tu waliokuwa na mali zao. Akajidai kuwalipa LONRHO anavyotaka yeye, mbona ilimtokea puani! Jee hamkumbuki? Kama wengi wenu hamkuwepo wakati huo, m-google mtazipata data.

Sasa haya ya Dowans tunapiga kelele na madudu tumefanya wenyewe, huwezi kuvunja mkataba na mtu aliyekwisha kuingia hasara ya kukuletea mlivyo ahidiana, labda viwe chini ya kiwango mlichokubaliana au viwe vibovu au awe hajavileta kabisa. Lakini hakuna sababu nyengine yoyote utayoitowa ukashinda, mahakama yoyote duniani labda iwe haifati haki.

Hili La Dowans, tutapiga kelele weee, at the end lazima lilipwe.

Hii imetokea wapi tena? Hivi JF siku hizi bila kujadili mambo haya ya kidini kidini hoja hazijengeki?
 
Hahahaaaaaa! Kumbe Fungamtama anajaribu kuwatishia watanzania ili wafunge mdomo apate % yake??? Masanilo kanifungua macho. Sasa badala ya watanzania kumpuuza 6 tunalazimika kumpuza mwenye kufunga mitama.
 
Fungamtama alichoongea ni siasa tupu. Na mtu mwenye akili atatambua kuwa katumwa na genge la kina Rostam. Hasa ukizingatia kuwa yeye ni wakili wa rostam kama alivyotufunulia Rev masa.
Kama yeye ni mwana sheria kweli angetambua kilio cha watanzania sii zaidi sana kwa hukumu ya kuilipa dowans bali ni jinsi gani tulivyofikishwa dowans kutoka kwenye kampuni hewa ya richmond.
Watanzania tunaiuliza serikali yetu itupe kanuni walizotumia kuhalalisha mkataba kutoka kwenye hewa na ni nani waliofanikisha hilo deal mnalothubutu kuliita mkataba.
Pia tunataka tuwekwe wazi kama kupanda kwa umeme ni kwa ajili ya kuwalipa dowans.
Na kama jibu ni hapana basi tunaomba serikali iweke wazi pesa za kuilipa dowans ambazo imeshatangaza kuzilipa zitatoka wapi na kwa njia ipi.
.
 
Kataeni kuwalipa muone yatayojiri. Mlishinikiza kuvunja mkataba sasa matokeo mnayaona.

Nyerere alijidai kuwataifisha LONRHO, ingawa taifisha yake ya Ma Benki na Mashamba Na Viwanda vya wazungu ilikuwa ya geresha kwani wote alikuwa akiwalipa, wote walilipwa, wasiolipwa ni waIslam tu waliokuwa na mali zao. Akajidai kuwalipa LONRHO anavyotaka yeye, mbona ilimtokea puani! Jee hamkumbuki? Kama wengi wenu hamkuwepo wakati huo, m-google mtazipata data.

Sasa haya ya Dowans tunapiga kelele na madudu tumefanya wenyewe, huwezi kuvunja mkataba na mtu aliyekwisha kuingia hasara ya kukuletea mlivyo ahidiana, labda viwe chini ya kiwango mlichokubaliana au viwe vibovu au awe hajavileta kabisa. Lakini hakuna sababu nyengine yoyote utayoitowa ukashinda, mahakama yoyote duniani labda iwe haifati haki.

Hili La Dowans, tutapiga kelele weee, at the end lazima lilipwe.

Zomba you are talking like one of them! Aren't you?

Mzee hapa huwezi kumshawishi mtu yeyote MWENYE AKILI TIMAMU kuwa ati sisi tulikosea kuvunja mkataba.Upuuzi!
Fuatilia riporti ya Kamati ya Bunge iliyoongozwa na Dk.Harrison Mwakyembe-Mwanasheria aliyebobea. Kamati iliweka mambo yote hadaharani na kila mtu ni shahidi ukiwemo wewe, Kikwete.Lowasa, Rostam na wengineo.

Naomba ujibu maswali rahisi kabisa kuhusiana na kadhia hii ya DOWANS/RICHMOND.

  1. Je, unaweza kutupa sababu kuu iliyomfanya edward LOWASA AKAJIUZULU NA BUNGE LIKAVUNJWA?
  2. Je,unajua ni kwanini RICHMOND waliamua kukabidhi kazi zao(Contract)kwa DOWANS baada ya sakata la kushindwa kuleta umeme kama walivokubaliana kati ya Serikali,Tanesco na Richmond kinyume cha taratibu?
  3. Je, unajua sababu za msingi zilizosababisha mkataba ukavunjwa?
  4. Je, unajua kuwa Kamati ya Bunge ilisafiri mpaka Marekani kwenda kuhakiki kama Richmond ilikuwa ni Kampuni halali iliyosajiliwa na walichokuta huko ni kuwa Ricmond haimo kwenye orodha ya Makampuni yaliyosajiliwaaaaaaaa??
Ukishapata majibu ya maswali haya basi njoo uendelee kutushawishi kuwa Lazimatulipe hizo
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom