Wakenya wanaharibu kiswahili?

Unajiumiza bure, kile ni kiswahili chao na hicho unachokisifia ni kiswahili chako. Lugha zote ziko hivyo hivyo, hutofautiana kwa kutegemea eneo, nchi hadi bara. Kiingereza cha London hakifanani na cha New York na hata vitabu wanavyovitumia kama dictionary ni tofauti. Kiingereza cha Afrika Kusini hakifanani kabisa na cha Nigeria na hivyo hivyo kiingereza cha Kenya hakifanani na cha New Zealand na kote huko Kiingereza ndiyo lugha kuu ya taifa. Kiswahili nacho kinatofautiana - cha Zaire hakifanani na cha Uganda na cha Zanzibar hakifanani na cha Mwanza, sasa kwa nini useme cha Kenya ni kibovu na huku wanaelewana wazungumzaji. Nimeshuhudia wakitucheka kwa kuongea Kiswahili kibovu hasa tunaposema maiti huyu badala ya maiti hii, au ng'ombe huyu badala ya ng'ombe hii - sasa hapo !
Kama hicho wanachoongea ni kiswahili chao, basi huko ndio tunaita kuharibu kiswahili. Huwezi kuweka makosa ya namma hiyo kwenye mitihani eti kisa ni kiswahili cha kikwako..
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom