Wakenya na utamaduni wa kulipa kodi

Mpitagwa

JF-Expert Member
Feb 10, 2012
2,339
1,119
Jamani wiki iliyopita nilitembelea Kenya, kilichoishangaza ni kuwa kila unaponunua kitu lazima upewe risti na usipochukua mtoaji na walio jirani wanakushangaa sana. Na wanakwambia kuwa ni jukumu la kila mkenya kuhakikisha kuwa wafanyabiashara wanalipa kodi. Na hili linatimizwa kwa kuhakikisha kuwa kila unaponunua, unachukua risti yako. Nikawaza na kupata hisia kuwa labda tabia hii imechangia Kenya kujiendesha kwa asilimia 98 kwa bajeti yake yenyewe. Hapa kwetu wanaJF wenzangu mnajua. tunafikia hata hatua ya kujadiliana na mfanyabiashara kuwa hii ni bei ya risti na hii ya bila risti na unajua kabisa kuwa hapa huyu anakwepa ushuru na unashiriki vizuri kabisa bila wasiwasi. Tufanyeje ili nasi tujifunze hili kwa wakenya?
 
Inawezekana wakenya wanapata huduma nzuri za jamii ndio maana wanajiona ni wenye nchi. Hapa kwetu mnalipa kodi halafu zinaenda kugawanwa na kina nkulo na washikaji zake ukienda hospitali unaenda kupewa maandishi badala ya vidonge au sindano na ndio maana maduka ya madawa daily yanaota kama uyoga, mkulua naye daily safarini na jopo la watu sijui mabalozi wana kazi gani maana sio wawakilishi tena wamebaki kugonga viza pekee!
 
Hapa kwetu TZ, ukienda nunua bidhaa za tsh laki moja, muuzaji anakuandikia receipt ya tsh 60000. Maana yake ni kwamba atalipa kodi ndogo sana. Suluhisho ni kwamba wananchi wapewe elimu via media ili waweze kudai risiti zao. Kulipa kodi ni utamaduni mzuri ikiwa kama inatumika kwa maendeleo ya wale wanaolipa kodi, vinginevyo hakuna haja ya kulipa kodi coz haieleti tija zaidi ya kunufaisha akina Mkulo!!
 
Inawezekana wakenya wanapata huduma nzuri za jamii ndio maana wanajiona ni wenye nchi. Hapa kwetu mnalipa kodi halafu zinaenda kugawanwa na kina nkulo na washikaji zake ukienda hospitali unaenda kupewa maandishi badala ya vidonge au sindano na ndio maana maduka ya madawa daily yanaota kama uyoga, mkulua naye daily safarini na jopo la watu sijui mabalozi wana kazi gani maana sio wawakilishi tena wamebaki kugonga viza pekee!

ata mimi naungana na wewe kaka,kama mtu unalipa kodi then haikunufaishi ata kidogo,wanagawana wajanja wachache whilst majority ar toilering in extreme poverty,unafikir mtu anaweza akawa convinced kudai risit ili aisaidie serikal ktk ukusanyaji kodi?lazima serikal ibadilike hasa ktk matumizi yake..yafocus ktk provision of social services to the majority na ndipo hapa watanzania nao watakapoona umuhimu wa kuisaidia serikal yao ktk ukusanyaji kodi otherwise tax evasion itazidi kushika kasi.
 
Kipi kianze sasa, kuwabana wezi au kulipa kodi?maana kweli ili tuwe taifa kodi hazikwepeki kama alivyowahi kusema nyerere kuwa viserikali corrupt havitozi kodi
 
Back
Top Bottom