Wake wa Marais wetu na Mambo yao

Mimi nimeuliza tu kama una uhusiano na Mama Mkapa na ndiyo maana unamtetea hata kwa vitu visivyo kichwa wala mguu.Wewe unaweza kuja na sababu zako murua tu za kumtetea na kuwarudishia imani wana jamiiforums kuwa humtetei mama Anna Mkapa nee Maro kwa sababu ya maslahi ya kifamilia/ kiukoo.

Hujafanya hivyo.

Mchagga mwenzie
Hujui mbinu ya mafisadi?
Angalia alivyofanya Lowassa, Chenge na Ben. Ni kukimbilia nyumbani kwanza
 
Tuandamane, sasa mbona tena unakuja na taarifa za uvumi? Na unatueleza kabisa huo ni Uvumi! Kama huna taarifa za kutosha acha wenye nazo watoe! Hapa uvumi si mahali pake
 
waliozulumika katika zoezi hili wameniomba nilete hili swala hapa jf kuomba msaada wenu wakuu

Safi sana, waambie waliokutuma kuwa taarifa zimefka na JF wamesema waende mahakamani na JF itakuwa macho kufuatilia jinsi mahakama itakavyoendesha kesi. Inawezekana mahakama pia ikatusaidia kuibua mambo mengine yahusianayo na matumizi ya hizo pesa za "pensheni".
 
Hivi Wakati wa Ben Ikulu yalitokea mangapi?
1. Iliungua ( wakadai pasi)
2. Fence ya ukuta(hii ilijengwa wakati wa che nkapa?)
3.
4.
 
Mwikimba !

Tafadhali tupe uthibitisho uliokamilika kuwa:-
1. Hao wahandisi walinunua hizo nyumba
2. Mama Mkapa amemmilikishwa hilo eneo.

Baada ya hapo tutaweza kuwafungulia mbwa wa hatari kwa magazeti na mtandaoni.
 
Watu Muache Kupiga Kelele Hizo Nyumba Zimenunuliwa Kihalali Na Hakuna Hata Chembe Moja Ya Rushwa Au Kudanganyana Na Mkataba Wa Uuzaji Nyumba Hizo Upo Wazi Sema Wahusika Wakuu Ndio Wanao .

Kwa Sasa Hizo Nyumba Pamoja Na Zingine Nyingi Ni Mali Ya Familia Ya Maro Sio Maro Mimi Lakini Maro Huyo

Wewe hebu funga domo lako, tunajua Anna Mkapa ni shangazi yako na ndiye aliyekuingiza huko kwenye u-snitch. Yaani huoni aibu kutetea ufisadi? Au ndio kula kulala bure kwa shangazi? Hebu nyamaza kabla hatujakutoa manundu!
 
Nimesikia mengi sana kuhusu huyu mama kumiliki real estate nchini; nasikia kuna mitaa Dar ukigusa tu unaambiwa imeshanyakuliwa... lakini hadi hivi sasa sijaona karatasi hata moja linalomuunganisha huyu mama na dili lolote la real estate. Kati ya mali hizo zote kuna yoyote yenye jina lake, kampuni, au familia yake ya karibu...?
 
jamani hawa watu sasa wamezidi kuchukua vitu vyetu kwanini tusiwapige mawe na adhabu hiyo ikawekwa kwenye sheria maake wanauzi sana?
 
Huu ni ujambazi wa hali ya juu...:( Watu wanauziwa nyumba na kulipa deni za nyumba hizo mpaka wanamaliza halafu wanaambiwa nyumba hizo kumbe zina mmiliki mwingine!!! Naye ni fisadi mama Mkapa!!!! Hizi title deeds zitolewe haraka sana kwa wanunuzi halali wa nyumba hizo au warudishiwe pesa zao zote pamoja na riba. Hawa majambazi hawana hata aibu!!!! Wanataka kukupua kila kona ya nchi ili kukidhi tamaa yao ya fisi ya kuwa matajiri wa kupindukia!! Hii kitu inasikitisha sana
 
Watu Muache Kupiga Kelele Hizo Nyumba Zimenunuliwa Kihalali Na Hakuna Hata Chembe Moja Ya Rushwa Au Kudanganyana Na Mkataba Wa Uuzaji Nyumba Hizo Upo Wazi Sema Wahusika Wakuu Ndio Wanao .

Kwa Sasa Hizo Nyumba Pamoja Na Zingine Nyingi Ni Mali Ya Familia Ya Maro Sio Maro Mimi Lakini Maro Huyo

Huyo Maro jambazi aliyehusika na kuwaleta makaburu wasiojua chochote kuhusiana na umeme ili waendeshe TANESCO na kuliacha shirika hilo hoi bin taaban.
 
Kwahiyo Unatamka Hazarani Na Kuonyesha Chuki Yako Dhidi Ya Muwekezaji Mzalendo ?

Je Angekuja Andrew Clay ?

Kwenye ujambazi hakuna uzawa. Mbona tunaoibiwa pia ni Watanzania Wazawa?

Huyo mama na bwanake wamejifedhehesha mno. Hivi Mkapa kwasababu anasalimiana na akina Bill Gates na yeye anataka kuwa na pesa kama wao? Tamaa imemzidi mno.
 
Wakuu wenye data watuorodheshee 'tujisenti' twa hawa partners ANBEN maana inaonekana list ni ndefu. Nianze na zinazotajwa sana

1. TanPower/Kiwira
2. Bank M
3. Ikulu ndogo Lushoto
4. Hotel SA
5. ...



Na tunyumba twa Mama hapa Dar na mikoani pia ? Kama tunahitajika kujumuisha kwa kuwa wao ni kitu kimoja then list is long
 
Wakuu wenye data watuorodheshee 'tujisenti' twa hawa partners ANBEN maana inaonekana list ni ndefu. Nianze na zinazotajwa sana

1. TanPower/Kiwira
2. Bank M
3. Ikulu ndogo Lushoto
4. Hotel SA
5. .ANBEN( Anna Benjamin)
6.nasikia Serengeti ana Hotel inayomilikiwa yeye na Thabo Mbeki
 
Huyo Maro jambazi aliyehusika na kuwaleta makaburu wasiojua chochote kuhusiana na umeme ili waendeshe TANESCO na kuliacha shirika hilo hoi bin taaban.

Ulijuaje ? Ulijua lini ? Na una ukweli gani kwamba hao wengine si wenye uhalali ila Maro wa aina yako ndiye mwenye uhalali huo ? Maro ni mtumishi wa Serikali ? Alikaa Mbeya ?
 
wakuu hali iko hivi,

1. NYUMBA 12 zenye utata ziko plot no 2747 block x, along great north road, wanaofahamu mbeya ni maeneo ya nane nane mkoani mbeya

2. mwaka 1987, wizara ya ujenzi iliomba survey ya kiwanja hicho kifanyike, na survey ilifanyika na kuwa approved by director of survey tarehe 29/4/87, kwa jina la zonal garage and hotel, for the ministry of works. reference survey plan no E14/472/37.

3. mwaka 1990 contractor aliyepewa kujenga barabara ya igurusi-kwenda songwe alipewa eneo hilo akajenga nyumba za ma-ex patriates wake, ikiwa ni wale wa kampuni ya renadert na partzank put

4.contrator alipomaliza kazi alirudisha nyumba hizo kwa mwenyewe yaani wizara ya ujenzi, compound ina nyumba 12, ambazo wizara iliwagawia ao ili allocate kwa wafanyakazi wake

5, mpaka hapo kiwanja hicho hakikuwa na hati kwa kuwa serikali huwa haina au haikuwa na utaratibu wa kuwa na hati miliki za viwanja vyake

6. sera ya serikali ya kuuza nyumba zake ilipotangazwa nao hawa wakaomba kuuziwa na wakaukabaliwa, wako 12 na kwa sasa wanakaa na familia zao

7. mwaka 1998, inaonekana mama ana mkapa aliomba apatiwe mahali pa kujenga hiyo inayoitwa shule huko mbeya, na kwa kificho, huyu bwana anayeitwa j.d.zongo, ambaye ana kashfa nyingi sana za uuuzaji maeneo wazi, huko dsm hasa sinza alilietwa hapa mbeya kama afsa ardhi. ni wakati huo huo aliandaa mpango wa siri wakampa mama mkapa hiyo offer na yeye akachemka huko bongo hadi akapata hati miliki.

8. wakati huo anapewa hati, tayari hawa wafanyakazi walishauziwa nyumba na kwa taratibu walitakiwa wakishamaliza kulipa, kufanyike sub-division from hati kubwa ili kila mmoja apewe hati yake. sasa walipoenda huko mbeya city council ndipo wakakikuta hiki kitimtim, kuwa mmiliki ni huyu mama fisadi.

9. wenzetu hawa wakarudi kwa mmiliki yaani wizara kupitia tanzania building agency, wizara na tanzania building agency wakapatwaa na mshangao kuwa kuna mtu anamiliki eneo lao, tena liliko ndani ya eneo lingine la serikali ambalo kuna karakana maarufu ya mbeya roadworkshop, karakana ambayo wizara ilipata msaada toka norway

mpaka sasa wanarushwa danadana, na ndoyo maana wanaomba msaada wenu wana jf

useful contact

manager
tanzania buildng agency
phone 025-2502755
mbeya
 
Jamani mnamsingizia Mama Mkapa... wenyewe wanaishi kwa pensheni tu!! Kama hizo nakala za mauzo zipo si zipenyezwe. Yeye na mke hawakuwa hata tujivisenti vya kusafirisha mizigo...


"Sina uwezo wa fedha ingawa najua mnasikia na kusoma mengi …naishi kwa pensheni yangu kutoka serikalini kutokana na kuwa kiongozi kwa miaka 10 ambayo hata Mzee Mwinyi anaishi hivyo maana sisi sote ni wastaafu. Huo (uvumi) ni uongo …uongo ….uongo ….uongo …uongo….uongo….uongo," alisema Mkapa.

Sawa wewe umejitetea na Mkeo je?



Kabisa, yaani wanaishi kama Mzee Mwinyi.
 
Wewe hebu funga domo lako, tunajua Anna Mkapa ni shangazi yako na ndiye aliyekuingiza huko kwenye u-snitch. Yaani huoni aibu kutetea ufisadi? Au ndio kula kulala bure kwa shangazi? Hebu nyamaza kabla hatujakutoa manundu!

Jamani hebu tusiwe wavivu wa kufikiri tuliojaa wivu na watu wa kulalamika kila wakati.Hoja iko hapo.Haina uthibitisho wowote sisi tunaanza kulalamika na kulaumu watu.Kuna mtu anaweza kututhibitishia madai hayo???Mimi naziona kama chuki binafsi.

Kwa mnaojua sheria,je ni kosa au ni kifungu gani cha sheria kinamkataza mke wa rahisi kuwa mjasiriamali ama kufanya biashara???
Mama Anna Mkapa ni msomi mzuri tu aliyebobea na amekaa katika biashara siku nyingi tuu,je tendo la mmewe kuwa rais linamkataza automatically kuendelea na biashara zake???
Mwenye ushahidi aje mbele aseme labda mchakato wa kununua nyumba hizo ulighubikwa na mazingira ya rushwa.Lakini mimi hadi sasa nayyaona maneno haya kama uzushi tu wa kumsingizia na kumchafua mzee wa watu.

Hebu tuwe makini na matumizi haya ya habari
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom