Wakazi wa UKONGA waapa kuandamana hadi bungeni

Mkuu umesema kweli tupu! Imagine! Jimbo lote la ukonga mbali na kutumia maji taka( maji ya kisima),hakuna hospitali ya maana ukiachilia mbali zahanati zilizopo kama Arafa, na Rugambwa ambazo ndizo tegemeo lako!:flypig:
Ziko kero nyingi kwa wananchi..............

Kulingana na taarifa ya Habari ya Jana ITV inaonyesha wazi mbunge wa Ukonga kupitia CCM amekata tamaa kabisa hana ushawishi, hana uwezo wa kulobby kwenye Serikali za mitaa, hana mvuto, hana ubunifu wa kutatua hata kero ndogo ndogo, hajawahi kukutana na wananchi wake kwa vikao vidogo vidogo kama wabunge wengine kama January Makamba wanavyofanya.

Kwa hiyo basi wana Ukonga wamelalamika sana kuhusu barabara inayotumiwa na Watu wengi ya kuanzia Mombasa mpaka Moshi Bar ilivyo mbaya kupita kiasi, hata leo hii ukienda kuona huwezi kupeleka gari yako ndogo utakoma na service yake maana ni mashimo makubwa ya Ajabu, Je kuchagua mbunge ambaye hana ushawishi ina maana hamuwezi kupata hata greda au kuwekewa kokoto kwa mwaka.

Hii ina maana basi wana ukonga tubadilike mwaka 2015.

La mwisho Namuomba huyu mbunge aje angalau kila kata mara mbili kwa mwaka kutatua kero za wananchi kwa kujadili na kuona mbinu gani zitumike ili kama anaona halmashauri ya Ilala haina jioya basi atuunge mkono tuandamane wiki nzima mfululizo bila kuacha maana hatuma maji ya dawasco hata tone tunatumia ya kuchimba, hatuna masoko mpaka uje buguruni, hatuna huduma nzuri ya mafundi wa Tanesco, Umeme kukatikatika, Mashimo ya taka n.k

CHADEMA MPO JIMBO HALINA KICHWA, KAZI KWENU. ZITTO INGAWA ILIFIKA MAZIZINI, NJOO UKONGA TENA NA DR SLAA
 
poleni wana ukonga ila kupanga ni kuchagua.siku nyingine muwe makini zaidi.muandamane labda hii serikali iliyoachwa na Mungu itawapa haki yenu kama sio kuwapiga mabomu ya machozi.haaaa haha haaaa,kwikwi kwikwi kwiiiiii serikali ipo kifungoni MUNGU AMEIACHA :sleepy:
 
wajifunze kupiga na kulinda kura! sio mnapiga kura kisha mnaenda kusikilizia matokeo baa! matokeo ndio hayo kuchezewa cheusi chekundu!!
 
ndio matokeo ya kuchaguliwa na kukubali. Lazima atimize matakwa ya waliompa kiti kwanza na sio wanaukonga.
 
M4C ikiweka kambi jimboni Ukonga, ubunge mwepesiii kama kusukuma mlevi vile!!! Hili jimbo lipo tupu
 
Mkitaka kumsikia atokee mpinzani aanze kujitangaza jimboni na kumwaga sera atakuja kulalamika.
 
Wacha wafu wazike wafu wenzao!
Inashangaza sana kusikia mtu mzima akisema kwamba watoto wa shule wanadanganyika kwa kubebeshwa mimba. Lakini hatujiulizi kwanini sisi watu wazima (above 18years) tunadanganywa kwa sukari, wali, soda, bia, kangara, key holders, kofia, t-shirts, fedha mamia sifahamu kama kuna anayepewa zaidi ya msimbazi mmoja au la na wengi kiasi gani. Hayo yote aidha mojawapo au kadhaa yanatufanya tundanganyike (tubebe mimba/tupate uchungu/hali mbaya ya maisha) kwa miaka mitano; harakaharaka unaweza kusema bora huyu anayebebeshwa ya miezi tisa kuliko tunaobeba ya miaka 5!!!

Labda kwa kasheshe hizi tulizonazo sasa zitatufanya tukokotoe mahesabu vizuri kati ya kubebeshwa ---- ya miaka 5 au bora ukose raha ya siku moja ambayo itakufanya usijutie miaka mitano itakayofuata!
 
mbona mlivyokuwa mnalishwa wali na kupewa t-shirt hamkutangaza.Pokeeni malipo yenu
Hahahahaha kumbe waliuza kura zao kwaajili ya wali?....wakae kimya mpaka siku watakapoamka na kugundua kuwa KURA zao ni bora kuliko wali na t'shirt.
 
Tena huyo meya mbuz kabisa anahudhuria miss ukonga lakini haitishi hata mkutano wa kutathmini hali ya wananchi,halafu na majitu ya huku yamelala sana,yanapigia kura mafisadi tu na kudanganywa na ngoma za kizaramo,wengine tunajaribu kufanya mabadiliko ,ila kuna wajinga kuliko,hata vijijin wanatushangaa,mimi nipo ukonga-mombasa tangu 2004 hakuna maendeleo yoyote tofauti na upanuzi wa hii barabara kubwa unaoendelea,licha ya kuwa na machinjio ni chakavu na ushuru wake hatujui unafanya nini.
 
Tena huyo meya mbuz kabisa anahudhuria miss ukonga lakini haitishi hata mkutano wa kutathmini hali ya wananchi,halafu na majitu ya huku yamelala sana,yanapigia kura mafisadi tu na kudanganywa na ngoma za kizaramo,wengine tunajaribu kufanya mabadiliko ,ila kuna wajinga kuliko,hata vijijin wanatushangaa,mimi nipo ukonga-mombasa tangu 2004 hakuna maendeleo yoyote tofauti na upanuzi wa hii barabara kubwa unaoendelea,licha ya kuwa na machinjio ni chakavu na ushuru wake hatujui unafanya nini.

Mkuu Mapalmo kwa moto huu Ukongo 2015 ni CDM.
 
Kuna taarifa kwamba mbunge amehama jimbo, amehamia mbezi. Anakuja ukonga mara moja moja kwenye shule zake za Tumaini kwa ajili ya kuchukua makusanyo. Shughuli za maendeleo ya wananchi hana muda nazo.

Diwani wa ukonga yeye ndiye haonekani kabisa na barabara ya mombasa moshi bar ndiyo anayopita lakini kwakuona aibu siku hizi anapanda gari yenye vioo tinted ili wananchi wasimtambue. Hovyo kabisa huyu mwanamke (inasemekana ni chakula ya kirumbe ng'enda, ndiye alifanya uchakachuaji akapitishwa kugombea, hata magamba wenzake hawamkubali hata kidogo).

Tuna meya wa manispaa ya ilala jerry slaa toka jimbo la ukonga hana msaada wowote kwa wananchi. Naye amehamia upanga na kuitelekeza kata yake ya g/mboto pamoja na jimbo la ukonga, na yuko busy kuutafuta ubunge 2015!

Nilishaapa na narudia tena hapa huyu kijana Jerry akigombea Ubunge na mimi tasimama kugombea naye tupambane.Huyu kijana ana majivuno ya hali ya juu na ana dharau kubwa kwa watu.CDM haitakuwa na upinzani wowote dhidi ya huyu kijana asiyejiheshimu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom