Invisible
Robot
- Feb 11, 2006
- 9,075
- 7,878
Na Geofrey Nyang'oro
HATIMAYE kitendawili cha sheria gani itatumika katika kuwalipa fidia wakazi wa Kipawa, jijini Dar es Salaam, kimeteguliwa baada ya serikali kuelezea msimamo wake kuwa itatumia sheria ya ardhi ya mwaka 1967.
Msimamo huo wa serikali, ulitolewa juzi na Afisa Ardhi Mkuu Mwandamizi katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Edgar Japhet, alipokuwa akizungumza na wawakilishi wa wananchi hao, kuhusu sheria itakayotumika katika kuwalipa fidia.
Japhet alisema malipo hayo yanazingatia sheria iliyotumika wakati wa uthamani.
"Serikali ilifanya tathimini mbili moja ikitumia sheria ya zamani na nyingine ikitumia sheria mpya lakini ikamua kutumia sheria ya zamani katika kuwalipa fidia wananchi wa Kipawa," alisema.
Hata hivyo wananchi hao wamekuwa wakiilalamikia sheria hiyo kwa madai kuwa inalenga katika kuwadhulumu.
Katika kikao hicho, wananchi wa Kipawa walimlalamikia Japhet kuwa ndiye chanzo cha kutaka kudhulumiwa.
Hata hivyo Afisa huyo alisistiza kuwa huo ndio msimamo wa serikali na kwamba unatokana na sheria iliyotumika katika tathimini ya eneo hilo.
"Siyo mimi niliyeamua ninyi kulipwa kwa sheria hiyo, maamuzi yaliyotolewa yanawataka mlipwe kwa sheri ya mwaka 1967 sheria iliyokuwa ikitumika wakati wa uthamani"alisema Japhet.
Alisema uamuzi huo, umezingatia ushauri kutoka kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Alisema kutokana na msimamo huo, tayari serikali imetenga Sh 30 bilioni kwa ajili ya malipo ya fidia kwa wananchi wa eneo hilo.
Kwa mujibu wa afisa huyo, fedha hizo ziko tayari wakati wowote wananchi hao wataanza kulipwa haki zao.
Japhet alisema fedha hizo zitatumika kuwalipa fidia wananchi wa maeneo ya Kipawa, Kigilagila na Kipunguni.
Kwa mujibu wa Afisa huyo, watu wa Kipawa, wametengewa Sh18 bilioni katika fedha hizo, taarifa ambazo zilionekana kuwachanganya watu.
Mwenyekiti wa wakazi hao Magnusi Mulisa,alisema kimsingi wananchi wa eneo hilo hawakubaliani na uamuzi huo wa serikali.
"Sisi tupo hapa kuwawasilisha wenzetu hata hivyo hatukubaliani na majibu haya tutakwenda kuonana na wenzetu ili kujua la kufanya,"alisema.
Chanzo: Gazeti la Mwanchi la Sept 13, 2009