Wakazi wa Dar, waliozoea Kinyaa!

Hongera Mwanakijiji kwa makala hii pamoja na wachangiaji mbalimbali kwa maoni yenu. Kwny mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi - Durban - S.A ilisemwa ktk majiji yenye 'USWAZI' slams na miundombinu dhaifu zaidi Africa ni Dar na Maputo. Mm niko Blantyre - Malawi nashuhudia wenze2 walivyopanga mji wao. Huwezi kuona mafuriko, takataka zikizagaa, maji machafu yakitiririka km hapo Dar.

Kazi ya serikali ni kupanga sera na kusimamia na bila shaka yoyote Magamba wameshindwa kabisa.naamini ktk nchi ya TZ wapigakura mbumbumbu ni waDar na pia tuwaite mazuzu wale wote wanaowachagua magamba ambao kwa miaka 50 ya uhuru wameshindwa kulijenga jiji bora la dar km mfano kwa TZ na makao makuu ya dola.

Hakika Bwana wafumbue macho hawa WaTZ wanaodanganyika na magamba maana wanaangalia lakini hawaoni, wanasikiliza lakini hawasikii na wanafundishwa wala hawaelewi.
 
Ni jambo la kusikitisha ya kuwa kiasi cha mvua Dar kinapimwa kwa mafuriko kwny makazi ya watu. Utasikia wakisema "mvua ilikua kubwa sana" je kwanini mnasema mvua ilikua kubwa? "umeona mafuriko ya kule tandale, Mikocheni .." wanasahau kitaalamu mvua hupimwa kwa mililita/sentimeta .

Mathalani ukichukua kiasi cha mvua kinachonyeshaga Mbeya au Moshi na kuileta hapo Dar huenda baadhi ya wa2 wangehama makazi yao kabisa.
na bila shaka ingeonekana ni gharika.
waTZ wasiwe wavivu kufikiria kama magamba na serikali yao hiyo mvua ni kubwa ila siyo ya kupindukia au wa2 wanavyodhani bali tatizo ni MIUNDOMBINU HAFIFU
 
Ni jambo la kusikitisha ya kuwa kiasi cha mvua Dar kinapimwa kwa mafuriko kwny makazi ya watu. Utasikia wakisema "mvua ilikua kubwa sana" je kwanini mnasema mvua ilikua kubwa? "umeona mafuriko ya kule tandale, Mikocheni .." wanasahau kitaalamu mvua hupimwa kwa mililita/sentimeta .

Mathalani ukichukua kiasi cha mvua kinachonyeshaga Mbeya au Moshi na kuileta hapo Dar huenda baadhi ya wa2 wangehama makazi yao kabisa.
na bila shaka ingeonekana ni gharika.
waTZ wasiwe wavivu kufikiria kama magamba na serikali yao hiyo mvua ni kubwa ila siyo ya kupindukia au wa2 wanavyodhani bali tatizo ni MIUNDOMBINU HAFIFU
Umeongea ukweli mkuu...
 
M. M. Mwanakijiji
April 15, 2009 (Tanzania Daima)


WANAENDESHA magari mazuri ya kifahari; wanavaa nguo nzuri za kupendeza na majengo ya ofisi zao yananguruma viyoyozi vya kuwapoza huku madirisha ya majengo hayo yaking’ara kwa vioo vilivyotiwa giza.

Ukiangalia kwa mbali Jiji la Dar linaanza kuonekana kama jiji jingine mashuhuri duniani. Ukiwaona wanasiasa wake wakiendesha magari yao yanayopepewa vibendera vya taifa au yale ambayo tunayaita ya kifahari wakielekea kwenye kona za “kujirusha” mwishoni mwa juma, unaweza ukaamini kabisa kuwa Dar yetu hii ni tambarare! Wenyewe wanaamini ni tambarare!

Tatizo la Dar ni wakazi wake

Kati ya watu wanaonishangaza kila kukicha ni wakazi wa Jiji la Dar. Nikisema wakazi ninamaanisha watu wote ambao wanafanya Jiji la Dar kuwa makazi yao ya msingi. Miongoni mwao ni rais, waziri mkuu, mawaziri, wabunge na watendaji wa vyombo mbalimbali vya serikali kama JWTZ, Polisi, Usalama wa Taifa, Magereza n.k. Pamoja na hao nawajumuisha mabalozi wa nchi mbalimbali, viongozi wa dini zetu (Sheikh Mkuu, Kardinali Pengo n.k ), pia nawajumlisha wasomi wote wa Chuo Kikuu cha Dar, IFM, madaktari wa Muhimbili Aga Khan na wengine wote ambao wanajitaja kuwa waliwahi kupata elimu rasmi yenye uthibitisho wa cheti!

Hawa wakazi najumuisha kina mama ntilie, wauza magazeti, wafanyakazi wa kawaida maofisini, watumishi wa majumbani, wauza nyama na wauza karanga. Ninachotaka kusema ni kuwa ninaposema “wakazi wa Dar” najumuisha watu wote wanaoishi Dar na simpi udhuru yeyote. Ninachosema ni kuwa wakazi hawa wa Dar (Jumuisha wote hao hapo juu na wale walioshuka kwenye mabasi na ndege leo!) ni watu waliozoea kinyaa na uchafu kiasi kwamba hawana fikra za kuishi bila ya vitu hivyo!

Kama wewe ni mmoja wa watu wa Dar unayesoma gazeti hili leo basi wewe ni miongoni mwa watu ninaowazungumzia. Leo sizungumzii mafisadi walioiba fedha Benki Kuu, wala sitaki kuzungumzia hawa wanaotaka kuwaibia watu wetu leo kwa kutumia mradi wa DECI.

Sitaki kuzungumzia mambo ya CCM wala vita ya TLP. Nazungumzia wakati karibu milioni tatu na zaidi wa jiji kubwa zaidi nchini mwetu la Dar. Hawa wamezoea kinyaa na kuvumilia uchafu!

Ndiyo! Uthibitisho wa hoja yangu leo ni jambo moja tu (naweza kuchagua mengine mengi) nalo ni mafuriko ya kijinga, yanayosababishwa na uzembe na ambayo yamekuwa yakiendelezwa miaka nenda miaka rudi na watu wasiozoea mazingira masafi na wasioabudu mazingira bora! Mafuriko yaliyotokea wiki iliyopita kama yale yaliyotokea 2008, 2007, 2006, 2005, 2004, 2003, 2002, 2001 n.k ni matukio yanayothibitisha jambo moja ambalo nataka kulisema, wakazi wa Dar hawachukizwi na mafuriko haya, wameyazoea, wanajua jinsi ya kukabiliana nayo kila yanapokuja.

Wao wamebuni njia mbalimbali za kuyakabili, kubwa ikiwa ni kukunja suruali zao hadi magotini, kushika viatu mikononi, na kuendelea na safari.

Njia nyingine ambayo wasomi wetu wameibuni ni ile ya kuweka matairi mabovu au maboksi ya mbao ili kutengeneza vivuko mahali ambapo maji yamepungua kwa kiasi. Wataalamu wetu wengine wameamua kupendekeza vivuko vya aina ya kisasa katika kukabiliana na mafuriko haya kwa kutumia usafiri wa enzi za kale wa migongo migongo. Njia hii inadaiwa inatoa ajira kwa wakazi wengine 50,000! Wa jiji letu hili.

Katika uchunguzi wangu wa hapa na pale nimegundua pia baadhi ya wasomi wenye usafiri wa magari ya kifahari wameamua kutumia njia ya kuhakikisha kuwa madirisha na milango ya magari yao yamefungwa na kwa hakika kujaribu kupita pembeni pembeni.

Wale wenye piki piki wanajua kuwa baada ya muda maji yatapungua hivyo wanapofika mahali penye maji mengi, basi wanaamua kuzisukuma pikipiki zao hadi mahali watakapoziegesha.

Mafuriko haya ambayo Rais Kikwete, Waziri Mkuu Pinda, Mkuu wa Mkoa Kandoro pamoja na wakuu wa usalama kina Said Mwema, Mwamunyange na Othman wameyazoea yamekuwa ni alama ya umoja na utulivu wa nchi yetu.

Ni marufiko ambayo Waziri wa Miundombinu aliyepo sasa (Kawambwa) na wale waliomtangulia (mzee wa Vijisenti) hawana mpango wa kuondokana nayo kwani kuondokana nayo ni sawa na kuvunja urafiki wa muda mrefu.

Mafuriko haya ambayo baada ya muda yatasababisha mlipuko wa kipindupindu (wilaya za Ilala na Temeke zitashindana nani ataongoza kwa muda mrefu zaidi) yamezoeleka mno kiasi kwamba hakuna mpango wa dhati wa kuachana nayo. Wakati watawala wetu wanajivunia kuinuka kwa majengo makubwa na marefu huku kinachodaiwa kuwa jengo refu kabisa nchini kuanza kujengwa ni wazi kuwa kitu pekee ambacho watawala wetu wameshindwa ni kushughulikia maji ya mvua na maji machafu.

Huku wakiona fahari wanaendelea kubomoa majengo ya kale, wakitoa vibali kwa majengo mapya, lakini wakishindwa kabisa kufikiria na kuanza mradi wa uhakika wa kujenga mitaro ya kisasa ya kusafirisha maji machafu na ya mvua toka kwenye makazi ya watu. Nimesema wameshindwa kwa sababu wameshindwa.

Ukiangalia barabara nyingi zinazojengwa katika kile wanachokiita maendeleo pembeni yake utaona wametengeneza mitaro ya aina ya “V” yaani ile ambayo haina mifuniko juu.

Mitaro hii ni wizi mkubwa wa hela za wananchi kwa sababu kwanza mitaro yenyewe haijaunganishwa, pili kwenye jiji ambalo udongo wake ni wa kichanga kila mvua inaponyesha mitaro hii ndiyo inakuwa ya kwanza kufukiwa.

Matokeo yake baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar ambao wamezoea kinyaa na kuvumilia uchafu wameamua kugeuza mitaro hii kuwa mashimo ya takataka kama alivyolalamika mkazi mmoja kwenye TBC mwishoni mwa juma.

Majiji yote ya kimataifa duniani ambayo yamejijenga na kujiboresha kitu kikubwa na cha kwanza cha msingi ni kuhakikisha maji machafu na maji ya mvua hayatuwami kwa muda mrefu aidha kwenye makazi ya watu maofisini.

Hivyo kwa kutumia mifereji au hata kuchimba mto usio wa asili wamefanya hivyo na kusababisha ukusanyaji wa maji yote machafu na ya mvua kuyaelekeza baharini au kwenye maeneo ya kukusanyia maji hayo.

Miji mikongwe kama London, Paris, na New York yamekuwa yakitumia mifumo mbalimbali ya enzi na enzi na wamekuwa wakiiboresha kwa kadiri ya mahitaji.

Hata hivyo miji mipya hasa kule Marekani ambapo miji mingi bado ni mipya mfumo wa maji taka na ya mvua inapangwa mapema kabisa katika ujenzi wa miji hiyo na pale inapobidi ujenzi wa nyumba na majengo mbalimbali huzingatia kwanza uwepo wa usafirishaji wa maji machafu. Katika nchi yetu na hususan kwa jiji letu la Dar, wazo hili limebakia vitabuni na kwenye hotuba za bajeti!

Ripoti mojawapo ya Timu ya Wanasheria wa Mazingira (LEAT) ya mwaka 2001 ilidokeza hivi kuhusu Jiji la Dar kuwa “ni asilimia 5 tu ya wakazi wa Dar ambao wameunganishwa na mfumo wa maji taka”. Na kwa kiasi kikubwa makazi mengi ya watu bado wanatumia vyoo vya shimo ambavyo uchafu wake hatimaye huishia baharini bila kuwekewa dawa (untreated).

Tatizo kubwa ni kuwa Jiji la Dar halifuati na haliwezi tena kufuata ile “Master Plan” yao ya miaka ile! Jiji letu limekuwa kwa kasi mno na watu wameongeza mno na sasa majengo pia.

Bila kuwa na uongozi wenye maono ya mbali tutajikuta tunakabana makoo hivi hivi.

Wao wenyewe (watawala wetu) wanafikiria kuleta barabara za juu kwa juu na vitambulisho vya smart card! Wakazi wa Dar waliozoea uchafu hawaoni kitu kisicho sawa hapo!

Wao wapo wapo tu; hawaandamani kupinga halmashauri zao na wasomi wao hawapigi kelele kupinga miradi isiyo na kichwa wala miguu!

Matokeo yake tunataka kuendesha magari ya kisasa kwenye barabara za juu kwa juu tukizungukwa na takataka! Katika akili zao watawala wako tayari kutumia bilioni 200 kwenye vitambulisho na hakuna anayefikiria kujenga mitaro ya kisasa ya ukusanyaji na utupaji wa maji machafu na ya mvua.

Hawezi kufanya hivyo kwa sababu wameshazoea. Unajua mtu ukikaa na uchafu muda mrefu hata mwisho husikii harufu yake?

Sasa, ninachosema si kigeni; wao wanajikua na Watanzania wanakijua na wakazi wa Dar wanakijua. Lakini hayuko mtu mwenye kupima gharama ya kiuchumi inayopatikana wakati mvua inasababisha mafuriko.

Watu wangapi wanachelewa kazini? Wangapi hawaendi kabisa? Miradi mingapi inabidi isimame kwa sababu ya mafuriko? Magari mangapi huharibika baada ya mvua hiyo?

Tukiwaambia watasema tunawaonea wivu, na ya kuwa watawahi kuuliza ‘kwanini hamrudi basi kama mnajua sana?’ Tukisema wamezoea uchafu watasema ‘mbona anatutukana huyu?’ tukisema unahitajika uongozi bora ambao haulei uchafu watalia ‘huyu ni mpinzani, CCM nambari wani!’

Wakazi wa Dar kwa kifupi wanastahili uchafu wote wanaoupata na mafuriko yote yanayokuja na yale yatakayokuja. Wanastahili kipindupindu na vingine vinavyowapindua; wanastahili harufu mbaya na mlipuko wa magonjwa ya matumbo na kichocho!

Wanastahili kwa sababu ni wao wenyewe wasiolalamika, wasiondamana kusimama sasa inatosha na ni wao ndiyo wanaendelea kuwachafua watu kutoka chama kile kile wakiamini kuwa siku moja watakumbukwa!

Matokeo yake wamebakia kusoma udaku, kula mahindi ya kuchoma, kwenda kujirusha na kucheza ‘ngwasuma’. Nani anajali?

Kitu pekee wanachokumbuka ni kuwa hii mvua ni ya muda tu na jua litatoka maji yatakauka, majengo yatapendeza tena na magari yatasafishwa na kurembeshwa. Na kila mkazi atasahau mafuriko ya wiki iliyopita na wote watakuwa wanafikiria suala la DECI!

Rais ataendelea na shughuli zake, Waziri Mkuu na safari zake, Meya na mikutano yake na wananchi wa kawaida na shughuli zao. Mpaka yake mafuriko mengine! Kwa sababu wakazi wa Dar wamezoea kinyaa, nani anawashangaa?

This is so touching.......what can I say brother?

hatujarogwa mkuu...tuna mtindio wa akili

Hakuna umeme, hakuna maji, hakuna usafiri, hakuna mafuta........kuna uchafu wa vinyesi, matakataka kila kona na bendera nyingi za CCM.

Seriously..I am leaving the city not after this stunning article..I thought before, there is no life in DSM...not at human standard

Mbeya my beloved city where are you? will you embrace me till I die...najuta kuifahamu DSM
 
...Ukisema jiji linanuka unaweza kushambuliwa kama mpira wa kona, lakini huo ndio ukweli. Huwa wanaanzisha kampeni za kisanii eti za kusafisha jiji na kupigwa mapicha mengi kisha hakuna ufuatiliaji wowote na matokeo yake jiji la Dar na majiji/miji mengine nchini kuendelea kuwepo katika hali ya uchafu uliokithiri na hivyo kuwa chanzo cha magonjwa mbali mbali yakiwemo malaria na kipindupindu.
 
Hahahaaa, imenikumbusha Wimbo wa Faustin Munishi wa "Eti wamerogwa....."

MMM na wengine, sidhani kama TUMEROGWA au tunahitaji KUOKOKA.....

Kila kitu duniani kwa sasa kipo wazi kabisa na hauhitaji Muujiza wowote kulifanya.

Kupanga ni kuchagua? Tumeamua kuishi kwa Minuso, acha tusote.

Mkizidiwa mafuriko, karibuni Sikonge ambako hatuna shida ya foleni wala harufu mbaya.



Najiuliza kama siku ya Uhuru, kuna Bundi walilia :)
 
Last edited by a moderator:
Sijakiona hata kimoja cha maana ulichokiandika.

Hujui kuwa huu mji umechafuliwa na wakuja?

Kweli dunia hii kuna watu na viatu!
Hiki kiatu nadhani kinafaa kuchakaa na kusahauliwa. We cha maana ulichoandika kiko wapi?
 
hii niliandika mwaka 2009. Ooh well! we prophets of doom!
Kuna wakati huwa nakunyoshea mkono mkjj, kuna thread moja ulianzisha baada ya mafuliko ya Kilosa ukauliza serikali imejiandaaje na majanga ya aina hii naitafuta siioni ninadhani ni wakati wa kuiibua ile hoja.
 
tunasubiri 'Mungu atunusuru...'
Tusisubiri Mungu aje kutuzibulia mifereji, kutuambia tusijenge kwenye mkondo wa maji, Mungu ana mambo mengi ya lazima kutusaidi zaidi ya haya.

Mimi naitupia lawama serikali kwa kufumbia macho waliokuwa wanajenga mabondeni kwa kuhofia kunyimwa kura, pale bonde la Jangwani upande wa Muhimbili kama sikosei miaka ya 80 kulikuwa hakuna hata nyumba moja, nyumba zimeanza miaka ya 90, tena nakumbuka mtu mmoja nafikiri alikuwa mganga wa kienyeji yule, baada ya hapo ikaja nyumba ikatundikwa bendera ya CCM tukaambiwa yule ni balozi hiyo nyumba haikuguswa hadi leo ni ofisi ya chama.

Bonde la Jangwani upande wa Yanga ukiacha majengo ya muda ya Kajima lilikuwa ni eneo la viwanja vya michezo lakini leo huwezi amini, watu wamegawana hata rais akipita anachekelea tu huku amri zake zikidharauliwa. Maeneo ya wazi yote yamejaa vibanda na ofisi za CCM hawaguswi. Nani utamlaumu kama si serikali na chama chake.

Kina Tibaijuka, Magufuri wanapojaribu kufuata sheria wanakutana na vikwazo toka juu, maeneo mengi ya wazi yamejengwa vituo vya mafuta mbaya zaidi wanaojenga ni wale tunaotegemea watutungie sheria. Mimi nafikiri tusimlaumu Mungu tujilaumu sisi wenyewe. Hili ni pigo kama alivyowapiga wana Sodoma na kama alivyoleta gharika wakati wa Nuhu kwa viongozi na watu kuifanya mioyo yao migumu.
 
Sijakiona hata kimoja cha maana ulichokiandika.

Hujui kuwa huu mji umechafuliwa na wakuja?

halmashauri yako ya kichwa haiko sawa. Sifa za kijinga. Serikali haijali sehemu zingine, imagine jiji la mwanza kuwa na vyuo vikuu 3.
 
Naangalia TBC hapa kuhusu mafuruko Dar na sehemu nyingine nchini na lazima nikiri I find the whole thing offensive! NI kana kwamba leo ndio watu wamegundua kuwa mvua huwa zinanyesha na kusababisha mafuriko. Watu wanazungumza utadhani wametoka sayari ya Zuhura!
 
Naangalia TBC hapa kuhusu mafuruko Dar na sehemu nyingine nchini na lazima nikiri I find the whole thing offensive! NI kana kwamba leo ndio watu wamegundua kuwa mvua huwa zinanyesha na kusababisha mafuriko. Watu wanazungumza utadhani wametoka sayari ya Zuhura!

Tangu lini misukule ikawa na akili timamu?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Naangalia TBC hapa kuhusu mafuruko Dar na sehemu nyingine nchini na lazima nikiri I find the whole thing offensive! NI kana kwamba leo ndio watu wamegundua kuwa mvua huwa zinanyesha na kusababisha mafuriko. Watu wanazungumza utadhani wametoka sayari ya Zuhura!
MM kuna mtu nimebishana nae sana leo anasema eti mvua kubwa sana imenyesha
nikamuuliza mvua gani kubwa anayozungumzia wakati tatizo limesababishwa na miundombinu nikamwambia akitaka kuzungumzia mvua kubwa aangalie yaliyotokea Thailand na Phillipines...
 
Naangalia TBC hapa kuhusu mafuruko Dar na sehemu nyingine nchini na lazima nikiri I find the whole thing offensive! NI kana kwamba leo ndio watu wamegundua kuwa mvua huwa zinanyesha na kusababisha mafuriko. Watu wanazungumza utadhani wametoka sayari ya Zuhura!

Na bado! Baada ya hapa tutasahau kabisa na ikitokea tena tutajifanya hivyo hivyo kana kwamba tumegundua mvua huwa zinanyesha na kusababusha mafuriko.

Subiri tu utaona.
 
Tangu lini misukule ikawa na akili timamu?
Halafu cha kushangaza eti mbunge wa Kinondoni naye analalamika eti vikosi vya uokoaji havipo halafu anaishia kusema eti tutafanyaje tukae tusubiri tu walahi ningekuwa karibu ningemnasa vibao viwili vya uso ili akili yake ifanye kazi vizuri..
 
Na bado! Baada ya hapa tutasahau kabisa na ikitokea tena tutajifanya hivyo hivyo kana kwamba tumegundua mvua huwa zinanyesha na kusababusha mafuriko.

Subiri tu utaona.
NN ngoja tule Krismasi tusahau kabisa...halafu pamoja na hayo watu serikalini wameishapata sehemu ya kutengenezea petty cash vouchers za uongo na kweli..
 
MM kuna mtu nimebishana nae sana leo anasema eti mvua kubwa sana imenyesha
nikamuuliza mvua gani kubwa anayozungumzia wakati tatizo limesababishwa na miundombinu nikamwambia akitaka kuzungumzia mvua kubwa aangalie yaliyotokea Thailand na Phillipines...

Aisee mimi hili la miundombinu nimelisema sana katika maongezi na watu lakini ni wachache sana ambao hunielewa. Huwa naishia kuambiwa 'we Ngabu tatizo lako unalinganisha kila kitu na Marekani' Lol.

Huhitaji kuwa genius kuona mapungufu na udhaifu wa miundombinu yetu.
 
This is so touching.......what can I say brother?

hatujarogwa mkuu...tuna mtindio wa akili

Hakuna umeme, hakuna maji, hakuna usafiri, hakuna mafuta........kuna uchafu wa vinyesi, matakataka kila kona na bendera nyingi za CCM.

Seriously..I am leaving the city not after this stunning article..I thought before, there is no life in DSM...not at human standard

Mbeya my beloved city where are you? will you embrace me till I die...najuta ?kuifahamu DSM

Arusha my beloved city where are you? will you embrace me till i die... najuta kuifaham DSM.
 
Back
Top Bottom