Wakazi wa Arusha walazimishwa kwenda kuwatazama JK na Mafisadi..

CCM wanagawa bendera, Tshirt na kofia bure, mkakati mwingine ni ukiweza kuleta watu 100 unapewa kuanzia laki 2 na zaidi,

Sasa hivi biashara ya kununua watu inalipa sana.

CCM siyo chama cha siasa tena. Ni genge la wahuni wachache na wajinga walio wengi.
 
Kitendo cha kutuambia tufunge biashara zetu kisa kikwete anakuja kwenye shughuli za kisiasa kimeni kera sana...Jana tumepokea taarifa tukiambiwa tusifungue ofisi zetu kuanzia saa saba mchana kwa majengo yenye gorofa yaliyo karibu na uwanja wa sheikh Amri Abeid...eti kwa usalama wa JK...cha kushangaza soko la crocon lilioko umbali wa takribani km 1 nalo limeamliwa kufungwa eti waka msikilize JK na CCM yake, je hizi siyo njia chafu zinazotumiwa na CCM kuhakikisha wana pata watu wengi mikutano yao kwani hata Dar tulishuhudia CCM ikikodisha magari ili yasafirishe watu kwenda na kurudi kwenye uwanja wa jangwani...sijui mikoani anatumia mbinu gani zingine...

haya kweli ni mashokororooroo
 
Mbaya zaidi jiji la Arusha lilivyo na miundo mbinu barabara moja tu ikifungwa mji mzima unataabika leo watakapofunga sijui itakuwaje... Kikwete na CCM yake ameshindwa kututatulia halafu wanatuambia kafanya mengi yapi?..barabara hakuna, wameshindwa hata kujenga stand ya mabasi..stand iliyoko hata kampuni moja ikiamua kupaki mabasi yake yote haitoshi (Mtei) halafu eti wanaita stand kuu, stand ndogo naenye hafai yaani hata vibasi vya sakina havitoshei..sijui ni vigezo gani vilitumika wapa uizinisha kuwa jiji au fance za matairi...
ndugu Arusha ilipokwa hadhi ya kuwa jiji, kwa hiyo bado ni manispaa tu
 
Mwaka 2005 CCM walisema wanaojaa kwenye mikutano ya Mbowe wanaenda kushangaa helikopta. sijawasikia mwaka huu wanasema nini juu ya umati unaofurika kwenye mikutano ya Dk.Slaa.
Lakini ni ukweli kuwa moja kati yatofauti ya mikutano ya CCM na CHADEMA ni kuwa wako wanaokwenda kwenye mikutano ya CCM kwa kuwa wanalipwa na kupewa posho pamoja na kwenda kujionea shoo za bure, ila wale wanaojaa kwenye mikutano ya CHADEMA wanajipeleka wenyewe na wote wanakwenda pale kwa ajili ya kusikiliza sera, huu ndio ukweli.
 
Kuna kitu kinaitwa kulewa madaraka. CCM wamelewa madaraka. Kama wasemavyo Waingereza, power corrupts, and absolute power corrupts absolutely!

Ila tujipe moyo. Awamu ya pili ya UHURU iko mlangoni. Awamu ya kwanza imedumu miaka 50. Ina mapungufu mengi, yakiwa ni pamoja na hii hali ya chama tawala kuwa kama wakoloni mambo leo.

Independence - phase 2 will be ushered in less than two months. It will free us from the whims of the CCM leaders..
 
Na nyinyi mkakubali kufunga shughuli zenu kwa sababu wamewaambia?

Labda wanakuwa na thugs wao wanaopita wakilazimisha. Umewasahau CCM walivyo? Kuna wakati walilazimisha hata wafanyakazi wasio wanachama wao kuwachangia. Let me tell of a personal incident. Baada ya kumaliza BSc nilibaki TA UDSM. Kuna watu wa CCM walitaka kukata sehemu ya mshahara wangu kama changio wakati sikuwa mwanachama. Bahati nzuri niliondoka Bongo baada ya muda mfupi, kabla ya kupandisha hasira mno.

Chama ambacho kinathubutu kuchukua viwanja vya michezo vilivyojengwa na Watanzania wote na kusema ni mali yake ni chama hatari sana.

CCM imeshalazimisha watu kuchangia mbio za mwenge. Inatumia nguvu.
 
Siasa za rais wa marekani kuja na watu kuambiwa VAENI SUTI NDO ZINAENDELEA:becky::becky::becky:
 
Watu wamehamasishwa na si kwamba wamelazimishwa. Mimi niko Arusha, eneo nilipo sijaona mtu aliyelazimishwa kwenda uwanjani ila magari ya matangazo yanasikika, sijui tafsiri ya kulazimishwa ni ipi. Kama wewe ni mpangaji kwenye maeneo ya CCM ni wajibu wala siyo hiari kwenda uwanjani kumsikiliza landlord wako

acha uongo bana .Matoyo AKA boda boda wamewekewa mafuta 10,000.00 mitsheti yao ya njano na kijani .Kule krokoni wameambiwa afunge biashara zao waende uwanjani.Ajabu nae Mkwere kaingia saa kumi na mbili kasoro wakati mwisho wa kampeni ni saa kumi na mbili. Tumeona na tu mashuhuda
 
Nyie mlioko Arusha, acheni kulialia bana.

Vaeni hizo nguo za kijani na Njano na muende mkachukue 5,000.

Chukueni magari yenu na mjifanye ni TAXI na nendeni Petrostation mkajaze mafuta ya Elfu 10.

Jamaa nasikia wanajaza mafuta kama hawana akili nzuri. Hima hima wahini.

Someni hapa: https://www.jamiiforums.com/uchaguz...mkutano-wa-kampeni-arusha-jakaya-kikwete.html
Njaa ukiiendekeza ni tatizo...niweke bendera ya CCM kwenye pikipiki,gari yangu kisa umenipa 10,000!?, jana niliingia uwanjani nikakuta watu wamejaa kuwatazama wasani walikuwa wakitumbuiza huku kila pande picha za JK, si kusumbutu hata kupiga picha maana niliona uchafu kwenye kamera yangu
 
Watu wamehamasishwa na si kwamba wamelazimishwa. Mimi niko Arusha, eneo nilipo sijaona mtu aliyelazimishwa kwenda uwanjani ila magari ya matangazo yanasikika, sijui tafsiri ya kulazimishwa ni ipi. Kama wewe ni mpangaji kwenye maeneo ya CCM ni wajibu wala siyo hiari kwenda uwanjani kumsikiliza landlord wako
Mkataba wa upangishanaji huishia kwenye yaliyokubaliwa kwenye mkataba. Mahusiano ya nje ya mkataba ni hiyari ya walioingia mkataba. Hivi kwa mfano mpangaji akiwa na deni mwenye nyumba anapaswa kumlipia? Ama mwenye nyumba akiwa na harusi mpangaji na sharti amchangie? Mmezidi ubabaishaji bwana. Mnaongoza serikali kihunihuni tu, tumeshuhudia ofisi nyeti mawilayani zikifungwa sababu mke wa mgombea katembelea wilayani. Wizi mtupu!!!!!!!!!
 
Watu wamehamasishwa na si kwamba wamelazimishwa. Mimi niko Arusha, eneo nilipo sijaona mtu aliyelazimishwa kwenda uwanjani ila magari ya matangazo yanasikika, sijui tafsiri ya kulazimishwa ni ipi. Kama wewe ni mpangaji kwenye maeneo ya CCM ni wajibu wala siyo hiari kwenda uwanjani kumsikiliza landlord wako

.
Kumbe basi ile sh 10000 watu wanazogawiwa sii rushwa bali ni kurejashewa pesa ya pango waliotoa kwa siku hiyo na landlord wao. Wow! Good landlord!!
 
Watu wamehamasishwa na si kwamba wamelazimishwa. Mimi niko Arusha, eneo nilipo sijaona mtu aliyelazimishwa kwenda uwanjani ila magari ya matangazo yanasikika, sijui tafsiri ya kulazimishwa ni ipi. Kama wewe ni mpangaji kwenye maeneo ya CCM ni wajibu wala siyo hiari kwenda uwanjani kumsikiliza landlord wako
Kama unataka kujua nenda Namvua Plaza, saba General, Makuyuni Building, soko la crocon nk labda uniambia wamiliki wa hizi sehemu ni ccm...Hata hivyo sikuwa na haja ya kwenda kupoteza muda kumtaza msanii labda wale wana mziki waliokuwa wanatumbuiza pale...

Na nyinyi mkakubali kufunga shughuli zenu kwa sababu wamewaambia?
Sikuwa na haja ya kulazimisha kufanya kazi kwasababu mimi ni mwajiriwa tu kwa hiyo mkuu akisema fungeni ofisi huna budi kufanya hivyo lakini kama ingekuwa ni ofisi yangu aaahhh pange chimbika...mbaya zaidi tuliambiwa tufunge tangu saa saba akaja kwenye tamasha lake saa kumi na moja....
 
Watu wamehamasishwa na si kwamba wamelazimishwa. Mimi niko Arusha, eneo nilipo sijaona mtu aliyelazimishwa kwenda uwanjani ila magari ya matangazo yanasikika, sijui tafsiri ya kulazimishwa ni ipi. Kama wewe ni mpangaji kwenye maeneo ya CCM ni wajibu wala siyo hiari kwenda uwanjani kumsikiliza landlord wako

Sijui kama umeteleza au sijaelewa maana ya kitu unachokisema. Sielewe maana ya mpangaji na wajibu wa kwenda kumsikiliza landlord. Napenda kujua maana ya mpangaji ni mtu aliyepewa jengo au chumba ambacho ni mali ya chama hicho au kwamba mtu ni mwanachama wa chama hicho. Hata kama neno mpangaji litakuwa na maana zote hizo sidhani kama mkataba upangaji una wajibu wa namna hiyo kisheria. Nadhani Vincent umekurupuka na kueleza usichokijua. sijawahi kusikia kama Haki za raia kushiriki masuala ya kisiasa yanaruhusu hayo.
 
Back
Top Bottom