Wakazi D’Salaam kufidiwa bil. 15/-

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,080
kawambwa.jpg
NA MOHAMMED ISSA
SERIKALI inatarajia kutumia sh. bilioni 15 kuwalipa fidia wananchi watakaoathiriwa na ujenzi wa barabara ya Jangwani-Kigogo hadi Ubungo Maziwa. Barabara hiyo itajengwa kwa kiwango cha lami, ikiwa ni mkakati wa kupunguza foleni katika Jiji la Dar es Salaam na kuwaondolea usumbufu wananchi wa maeneo hayo. Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania
(TANROADS) mkoa wa Dar es Salaam, James Nyabakari, alisema hayo juzi, alipotoa taarifa ya ujenzi wa barabara hiyo kwa Waziri wa Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa. Nyabakari alisema fedha hizo zitatumika kuwalipa fidia wenye nyumba zilizo kando mwa barabara hizo na kuhamisha miundombinu ya maji, umeme na simu. Alisema barabara inayoanzia mtaa wa Twiga hadi Kigogo Mbuyuni, ambayo ujenzi wake utatekelezwa katika awamu ya pili, wananchi watafidiwa sh. bilioni nne. Meneja huyo alisema barabara ya kutoka Kigogo Mbuyuni hadi Ubungo Maziwa, ambayo ujenzi wake upo katika awamu ya kwanza, sh. bilioni 12 zitatumika kwa ajili ya kuwalipa fidia wananchi. Dk. Kawambwa alisema ujenzi wa barabara hiyo ni utekelezaji wa mpango wa serikali wa kuboresha miundombinu ya Jiji la Dar es Salaam. Aliagiza uhakiki ufanyike kwa umakini, ili kuepusha matatizo yanayoweza kujitokeza wakati wa ulipaji fidia. "Ninawaomba mfanye uhakiki wa kina kusije kukajitokeza migogoro baadae, natarajia katika kikao cha Bunge kitakachoanza hivi karibuni nitaomba ridhaa ya kutumia fedha hizo," alisema. Kwa mujibu wa Dk. Kawambwa, iwapo makadirio ya matumizi ya fedha ya wizara yatapitishwa na Bunge, miradi hiyo itaendelea kutekelezwa. Alisema watakaoathiriwa na mradi huo watatafutiwa eneo mbadala kwa ajili ya makazi na kwamba, ameridhishwa na hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa barabara hiyo.


Wakazi D
 
ni jambo la maendeleo kupunguza kero ya foleni jijini. naliunga mkono
 
Back
Top Bottom