Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 10,877
- 2,756
Kuna mambo mengi yanaendelea hapa nchini ambayo tunaweza kuyachambua na mengine kuonekana kwa wachache ambayo yote haya yanaumiza nafsi za watanzania wengi. Nikitaja madudu hapa sitamaliza ila wenzangu mnajua, tena zaidi kuliko mimi. Nimewahi kusema wakati flani kuwa mzalendo wa kweli ni yule mwenye sifa kuu mbili. kwanza uwezo wa kujibainisha, pili awe na dhamira iliyo hai. vingine ni mbembwe tu. sasa basi, haya yote yamefika hapa kwa uongozi 'imara' wa CCM. ndani ya chama kuna waadilifu wachache kama Sitta na kundi lake. Ili usemi wa baba wa Taifa utimie, LAZIMA hawa watu wajitoe ndani ya chama na kuangalia mistakabali wa taifa kwa mapana na uzalendo zaidi. kuendelea kubaki na kukubali kunyamazishwa huku ukijifanya unaumia ni unafiki tu! Mbona hawa viongozi wetu wanaogopa changamoto? Au siasa ndio ajira? Bila siasa mtu hawzi ishi? Bila CCM hakuna maisha? Obama alisema YES WE CAN! Na wao wanaweza kujiengua na kufanya mambo ya maana zaidi. Tunataka Tanzania mpya 2010 na kuendelea. Naomba kuwasilisha hoja!