Wakati TV za Kenya Wakirusha Live Kesi ya The Hegue; TV za Tanzania Zinaonesha Tamthiliya za Kigeni

Shame to all Tanzanian TV media kwa kushindwa kutuonyesha midahalo ya utoaji wa maoni juu ya katiba mpya iliyokuwa inafanyika Dodoma na Karimjee Dar Es Salaam. All the media wanafahamu kama si kujua kuwa watz walikuwa ancious kuona kinachoendelea kwa kuwa ni wa TZ wachache sana walioweza kushiriki.

1. Big shame and ooooohhhhhhhhhhhhhhh buuuuuuuuuuuuhhh toTBC1, kituo chetu cha taifa ambacho kodi zetu ndio zinazoendesha kituo hicho. Ishu ya muhimu na msingi kama hiyo na kushindwa kurusha live waka rusha ishuz zisizo na tija mbele ya wengi. mliogopa au? falsafa yenu ya ukweli na uhakika ipo wapi?Baadae mkatuletea eti Habari Mapsuko (BREAKING NEWS) wananchi walivyokuwa wanang'ang'ania kuingia ukumbini na polisi kutumia nguvu, lengo lenu ni kujenga chuki kuwa watu sio wavumilivu?

2. Big shame to Star Tv waliohaidi wangeonyesha live yanayoendelea Dodoma, tena wakaanza na uchambuzi na picha za nyuma kuonyesha mambo yameeanza halafu wakakatisha matangazo pasipo kutoa taarifa au hata kuomba radhi

3. Shame to Channel Ten ambao falsafa yao ni kutoa habari bila woga wala upendeleo, mbona woga uliwapata kuonyesha midahalo hii?

4. shame to ITV ambao toka mwanzo harakati za katiba mpya zilipo anza ndio kituo pekee waliokuwa wanaonyesha live midahalo hii ila kwa mdahalo huu nao wakaingia mitini na kutuacha kama watoto yatima.

Shame to usalama wa taifa naamini kabisa pia wameingilia uhuru wa vyombo vya habari na kuvitishia mpaka vyote kutoonyesha

All tv Media zina stahili kuiomba radhi jamii ya kitanzania kwa kushindwa kufikia matamanio yetu kwa kushindwa kuwashirikisha watanzania katika midahalo muhimu kama hii kwa mustakabali wa taifa lao na maisha yao kwa ujumla

They still do not think they must be accountable to wananchi in terms of news coverage. Wao wanafukuzia pesa zaidi kuliko kuhudumia wananchi. Mafisadi wakubwa! Wanafiki wakubwa!
 
Kwa kweli hawa jamaa wa media hawana uzalendo kabisa, toka tukio la mabomu gongo la mboto litokee sina imani nao kabisa...........wao kwao tamthilia za kigeni na vipindi vyao visivyo na tija ndio vya muhimu zaidi..
 
Mkuu hapa Bongo vyombo vya habari hatuna. Ingekuwa Mkutano mkuu wa CCM kila Redio na TV zingetuonyesha matangazo lakini kwa masuala mazito ya kitaifa huwezi kujua kama kuna TV hapa.

Au kama kuna maandamano ya Chadema kama ilivyokuwa kanda ya ziwa vile?
Kwa maoni yangu hilo ni moja kati ya mapungufu ya media ya Tz kwa ujumla wakati mwingine huwa hawatoi kipaumbele kwa masuala ya kitaifa kwa sababu zozote zile, wakemewe. Ila siyo lazima kuhusisha na airtime ya vyama kwenye tv sababu hapo unakuwa unaongelea biashara, kwa mfano Ccm wakilipia masaa mawili kurusha birthday yao kwenye tv bila kuvunja sheria thats ok, likewise kwa Chadema, Cuf, Nccr etc. Labda maamuzi yanabaki kuwa ya mtu mmojammoja kuangalia kama umependezewa au vinginevyo kama hakupendezewa, siyo ishu...
 
sijui kama ni swala la msingi sana kujadiliwa hapa, lakini jana ilibidi nijiulize inakuwaje serikali yetu inashindwa kuwapa raia wasiokuwa na uwezo wa kwenda karimjee au msekwa halls,kufuatilia mjadala wa katiba kupitia television ya taifa?

TV ya taifa inaonesha vipindi vya ajabu ajabu sijui 'Bango', mara 'Cherekochereko', sijui 'Orijino Komedi' mara 'karume alikuwa mvuvi wa fish' mara 'Karume alipigwa Risasi'. Hii imekaaje?

Star TV walijaribu, lakini na wao hawakuchukua raundi wakapotea. Wakatuwekea kipindi cha 'msanii wetu wa mduara'. Kila kitu usanii tu.

Lakini vyombo vya habari vya jirani zetu Kenya huwa hawana mzaha kunapokuwa na mambo ya msingi yanayohusu taifa lao. Iwe KBC, iwe Citizen, iwe NTV. kipindi cha mchakato wa katiba yao kila kitu kulikuwa 'live and interactive'.

Jana vilevile, "The Ocampo Six" ilikuwa live kwenye TV za Kenya.

Lakini Bongo mmmmmmmmmmmh!!

Tanzania bado sana.

very true bro, nimekuwa nikifuatilia hii issue ya kenya live KTN! wenzetu wako mbali saaana!! nikicheki ITV.. poor quality katka picha, vipindi... news...:tape: huyu ng`ombe wa maskini " TNZ " Sijui atakuja kuzaa lini..?
 
Kuna mtangazaji mmoja, kwenye redio fulani, jana wakati akitangaza mechi ya yanga na african lyon, alisema 'nchi yetu inajivunia kuwa na mchezaji mwenye kipaji kama Davis Mwape'.

Tuna watangazaji wajinga ambao wao ni kuropoka tu hata hawajiandai nini wanachotangaza....
 
Nimefurahi sana. kwa namna moja au ingine athari za mwl nyerere zinaonekana mpaka leo. kipindi chake tv ilikuwa ikulu tu na wengine tulikuwa hatujui kama hata kuna kitu kinaitwa tv wakati wenzetu wazenji walikuwa nayo long time (1960s).
kam si juhudi za mwalimu katika kuwanyima watu taarifa basi huu utamaduni tusingekuwa nao, na mengineyo mengi. you pipo watch out and get out of the box
simply acha kulalamika kwani hiyo ndo misingi imara aliyotuachia mwl!

Nakumbuka mpaka mwishoni mwa miaka ya 90 tv hitachi 21" ilikuwa inauzwa kati ya sh 400'000 na 500'000 sikumbuki hali ilikuwaje kabla ya hapo. Ninakumbuka pia kuwa RTD ilikuwa inasika sehemu nyingi na magazeti japo kwa kuchelewa kutokana na matatizo kama ya usafirishaji still yalikuwa yanapatikana.
Nashawishika kuamini kuwa Mwalimu hakukosea kuzuwia usambazaji wa tv kama alizuwia. Ikiwa habari zilikuwa zinawafikia wananchi kwa njia ya radio na magazeti with reasonable price, then it was too luxurious to have tv with such prices hasa kwa sera zake za ujamaa. Pengine ndiyo maana Nyerere anakuwa kiongozi aliyefanikiwa kudhibiti pengo kati ya matajiri na masikini japo lilikuwepo...
 
Tutabaki kununua pirated kit za timu za ulaya na kuanzisha mabonanza ya ajabu sana katika ule mpango maaluma wa kugawiana virusi. hamna cha maana.
 
Ngoja JF tuwawekee somo media ya Tanzania kuhusu freedom of expression kama ilivyochambuliwa na Balozi Juma .V. Mwapachu ktk mkutano wa Media Council Of Tanzania ambapo Balozi Mwapachu alitoa 'paper' kwa kifupi jukumu la vyombo vya habari kuwa huru bila kujipendekeza 'kutowaudhi watawala' kwa kutoa habari muhimu kwa umma, tumsikilize Balozi akijaribu kuwaamsha waandishi wa habari na wenye vyombo vya habari kutumia haki yao ya kikatiba 'kuandika na kurusha' habari kwa umma:

 
Last edited by a moderator:
Kenya wana mpaka high definition TV. Na wana documentary bomba za Babu wa Loliondo wakati sie hakuna kitu. TV zetu zinambore hata mbwa wangu.

 
Last edited by a moderator:
Wanasubiri waoneshe jinsi, jk, ra, el na wengine watakaposomewa mashitaka nao the Hague. We subiri tu!
 
1] Kwanza journalists/ broadcasts hawana uzalendo na nchi yao
2] Pili hata waajiriwa wengi wa TBC,ITV,CH10,STRTV ni wana ukoo / wenye sifa zenye utata(incompitent) hivyo waoga kutimuliwa
3] Wengi wao bado wana damu ya CCM/ ni makada maarufu wa ccm
4] Wanafanya kazi kwa sifa (kujikomba) kwa waajiri wao ili wateuliwe kwenye chama
5] Wengi wao elimu zao ni ndogo sana (low qualifications)
6] Wamiliki wa Vyombo hivi ama ni makada ama ni wafanyabiashara wenye kuhitaji misamaha ya kodi kila kukicha. Hizi ndo media za Tz na wanahabari wa Tz (95%)
Ushauri wangu ni hivi tuanze Movements za kuidai TBC maana pale ndo petu ...

mkuu umenena! Tanzania bado safari ni ndefu
 
Back
Top Bottom