Wakati Museveni aki... Kenya Mabomu 60 Yakutwa

Bowbow

JF-Expert Member
Oct 20, 2007
541
31
Wakati Museven akihaha kuingiza majeshi yake Kenya kumuunga mkono Kibaki

Polisi wametegua mabomu 60 kwenye Reli katika mji wa Jinja
soma hiii

Polisi wategua mabomu 60 kwenye njia ya reli

KAMPALA, Uganda

WATAALAMU wa milipuko wametegua mabomu 60 yaliyotegwa katika njia ya reli mjini Jinja, Kusini Magharibi mwa nchi hiyo.

Iliripotiwa jana kuwa mabomu hayo yaliokotwa katika kijiji cha Kiriya kilichopo Jinja Jumatatu wiki hii, ingawa mtu ambaye aliyehusika na kutega mabomu hayo hakutajwa katika vyombo vya habari. Kwa mujibu wa taarifa za kipolisi, mabomu hayo yalikuwa na ukubwa wa kati ya milimeta 66 na 82 na yalitupwa katikati ya mataruma ya reli. Kati ya mabomu hayo, moja lilikuwa jipya na yaliyosalia yalikuwa na kutu.

“Ilikuwa ni hatari sana, kwani yangelipuka kama treni ingepita kabla ya kuteguliwa,” alisema Kamishna Mkuu wa Polisi wa Kusini Magharibi, Bw. Christopher Kubai, alipozungumza na gazeti la Daily Monitor juzi. Kamishna huyo alisema bado Jeshi la Polisi linafanya uchunguzi ili kujua jinsi mabomu hayo yalivyotegwa katika reli hiyo.

Bw. Kubai aliongeza kuwa mtu yeyote takayebainika kutega mabomu hayo Jeshi lake litamchukulia kama gaidi na akawataka wananchi kutoa taarifa katika kituo chochote cha Polisi kama wanamshuku mtu aliyehusika na tukio hilo.

Alisema yangetokea maafa makubwa kwa wakazi wa Jinja na kuongeza kwamba tayari uchunguzi wa umeanza ingawa hakuna hata mtu mmoja aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo.

Chanzo kimoja cha habari kililiambia gazeti la Daily Monitor toleo la jana kwamba tukio hilo linachukuliwa kwa uzito mkubwa kutokana na kuyaweka maisha ya watu hatarini.

“Hatuwezi kulichukulia jambo hilo kwa urahisi kwani kwa kufanya hivyo ni kuhatarisha maisha ya watu na mtuhumiwa atakayekamatwa ni lazima achukuliwe hatua kali,” kilisema chanzo hicho cha habari.

Ilielezwa kwamba kufuatia taarifa hizo za kuokotwa mabomu katika nji ya reli kumezua hali ya wasiwasi mkubwa kwa wakazi wa mji wa Jinja huku wengine wakikumbuka tukio la kigaidi la mwaka 2000 wakati ulipotokea mlipuko wa bomu katika mji huo.

http://www.majira.co.tz/kurasa.php?soma=kimataifa&habariNamba=5360
 
Back
Top Bottom