WAKATI KIPROTICH AKIIBUKA NA 200MIL UG SH kwa Gold Medal; Sisi Twaibuka na Mabegi Yamejaa

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797


WAKATI KIPROTICH AKIIBUKA NA SHILINGI MILION 200 UGANDA KWA KUSHINDA MEDALI OLIMPIKI, WASHIRIKI WA TANZANIA WAREJEA NA VISINGIZIO.


  • 16 August 2012


Rais Yoweri Museveni wa Uganda ameiagiza Wizara ya Elimu na Michezo nchini humo kuhakikisha wanamichezo wa Uganda wanaoshinda medali katika ngazi ya Afrika na zaidi ya hapo wanapata usaidizi kutoka serikalini na pia kupatia ajira katika taasisi za serikali haswa Jeshi, Polisi, Magereza, Mamlaka ya Wanyamapori na Idara za Usalama.

Museveni pia ameagiza Wizara hiyo kujenga kituo cha kisasa cha mafunzo cha michezo katika eneo la Sebei ndani ya mwaka mmoja na kusema wanamichezo walioajiriwa na serikali wanatakiwa kupewa muda zaidi wa kufanya mazoezi mbali majukumu yao ya kazi.

Rais Museven alimkabidhi mshindi wa medali ya dhabu katika michezo ya Olimpik Stephen Kiprotich hundi ya shilingi milioni 200 na kuamuru fedha hizo ziwe zimeingia kwenye akaunti ya siku hiyo hiyo.

MO BLOG: Wanamichezo wa Tanzania hongereni kwa kushiriki; lakini kusema ukweli kamati nzima ya Olimpiki ya Tanzania mnajisikiaje? Mtatoa sababu mpaka lini? Kuacha kutalii na Mizigo.

Hizo pesa ni sawa na $ 80,000 ni zaidi ya Wamarekani wao ukipata Gold wanapewa $ 25,000

427205_340977205988229_1910571271_n.jpg



Wapendwa Wamerudi Mizigo Kibao; Wametakata Walishiriki nusu siku wakakaa London siku 18 Mapumzikoni
 
Ninapata shida sana na jinsi sisi watanzania tunavyoongelea hawa wana michezo walioshiri Olympics London. Tunajikita sana kwenye ku-attack watu bila ya kuungalia tuliwaandaaje? Hivi ni kiasi gani serikali na watanzania kwa ujumla wetu tulishajadili Olympics? Tulichangia nini hadi wakafikia hapo walipo? Hawa wana michezo wametokana na juhudi binafsi, wanapata msaada next to nothing, kwanini tusione hilo?

Kenya wamewekeza sana kwa wanamichezo wao, na walianza kujiandaa miaka mingi nyuma, hapa Tanzania tumekaa kupiga domo!

Binafsi nawapongeza wanamichezo wote walioshiriki, hata kama hawakupata medal. Na nina hakika kama wangekuwa wamepata msaada huko nyuma wangeweza kufanya vizuri.
 
Back
Top Bottom