Elections 2010 Wakati Dk Slaa anatafuta kura za urais mimi nimeamua kuzunguka Tanzania kutafuta wabu

Mallaba

JF-Expert Member
Jan 30, 2008
2,554
47
Akihutubia maelfu ya wakazi wa Musoma, Zitto alisema kuwa lengo la kufanya ziara katika Jimbo la Musoma ni kutaka kuhamasisha wakazi wa mji huo kumchagua mgombea ubunge wa Chadema, Vincent Nyerere katika Uchaguzi Mkuu ujao.

“Wakati Dk Slaa anatafuta kura za urais mimi nimeamua kuzunguka Tanzania kutafuta wabunge ambao tutaweza kufanya nao kazi ili kutetea maslahi ya Watanzania na kati ya wabunge ninaowahitaji mmojawapo ni Vincent Nyerere,” alisema Zitto huku akishangiliwa na umati mkubwa wa watu.

Alisema ili Watanzania waweze kuondokana na umasikini uliokithiri miongoni mwao hawana budi kufanya mabadiliko ya uongozi ambapo alidai kuwa chama pekee kinachoweza kuwakomboa ni Chadema.

Zitto alisema kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita chama hake kimeweza kuibua kashfa mbalimbali, lakini wahusika hawajakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya dola.

“Bila Chadema msingejua mambo yaliyofanywa Benki Kuu, bila Chadema msingejua Richmond na ilitakiwa watu hawa wachukuliwa hatua. Naomba safari hii mtupatie dola, Jeshi na Mahakama tuwatumikie kwa uadilifu ,” alifafanua Zitto.

Zitto aliwaomba wananchi kukichagua chama chake ili watuhumiwa wote waweze kuchukuliwa hatua za kisheria kazi amabyo alidai kuwa haiwezi kuifanywa na CCM.

“Watu wa Musoma, siamini macho yangu tangu nianze kuzunguka sijahutubia watu wengi kiasi hiki, hivyo nawaomba kwa kutumia uwingi huu mkipigie kura Chadema katika Uchaguzi Mkuu ujao ili tuweze kuwatumikieni na hatimaye kufaidi maliasili zilizopo nchini,” alisema Zitto.

Akizungumzia sula la vurugu katika zoezi zima la kampeni mjini hapa, Zitto alilitaka Jeshi la Polisi mkoani hapa kufanya uchunguzi wa haraka na
kuhakiskisha kuwa watu wanohusika katika vurugu hizo wanafikishwa katika vyombo vya sheria.

Zitto alisema amesikitishwa na kitendo cha baadhi ya watu kujichukulia sheria mkononi kwa kuwakata watu mapanga kwa ajili ya kura hali amabyo alisema kuwa inatishia amani na usalama wa wakazi wa Musoma na Tanzania kwa ujumla.

“Namtaka RPC, OCD na RCO kufanya uchungzi wa haraka na kuhakikisha kuwa watuhumiwa wanakamatwa na wanafikishwa katika vyombo vya sheria ili sheria ichukua mkondo wake, hatuwezi kuwamaga damu kwa ajili ya watu wachache wenye uchu wa madaraka,” alisema.

read more here
 
Zitto una akili kuliko Slaa, hutaki mikataba ya kula ruzuku bali unaimarisha demokrasia, wewe ni mpinzani wa pili baada ya mtikila ambaye mngegombea ubunge ilala ningekupigia kura(japo una element za umangi)
 
kumbe unakaa Ilala ndo maana mawazo yako yako namna hiyo..sikushangai
 
Zitto una akili kuliko Slaa, hutaki mikataba ya kula ruzuku bali unaimarisha demokrasia, wewe ni mpinzani wa pili baada ya mtikila ambaye mngegombea ubunge ilala ningekupigia kura(japo una element za umangi)

Mzee wa kuchakachuliwa..........
 
Honestly Thito hunichanganya, Not very sure where he stands! But in a mean time hebu tuungane kukata mbuyu, mengine kitaelewka mbele kwa mbele
 
"Bila Chadema msingejua mambo yaliyofanywa Benki Kuu, bila Chadema msingejua Richmond na ilitakiwa watu hawa wachukuliwa hatua. Naomba safari hii mtupatie dola, Jeshi na Mahakama tuwatumikie kwa uadilifu ," alifafanua Zitto.

Hivi mahakama ni tawi huru la serikali au lina kuwa chini ya chama? Mh. I guess hapa aidha aliongea bila kutilia maanani anacho kisema au kweli ana amini kwamba chama kinacho kuwa madarakani ndicho kinacho ongoza mahakama. Anyway wanasiasa wetu hao.
 
nimeunga tu sentesi..mzee wa kuchakachuliwa na mama yake..usije enda kuwaambia mods wenu ukanipa usumbufu usio wa lazima.

Hivi kumbe kuunganisha sentensi ndio hivi:A S 103:yaani maneno yanakuwa muungano eti ..au siyo
 
"Bila Chadema msingejua mambo yaliyofanywa Benki Kuu, bila Chadema msingejua Richmond na ilitakiwa watu hawa wachukuliwa hatua. Naomba safari hii mtupatie dola, Jeshi na Mahakama tuwatumikie kwa uadilifu ," alifafanua Zitto.

Hivi mahakama ni tawi huru la serikali au lina kuwa chini ya chama? Mh. I guess hapa aidha aliongea bila kutilia maanani anacho kisema au kweli ana amini kwamba chama kinacho kuwa madarakani ndicho kinacho ongoza mahakama. Anyway wanasiasa wetu hao.

Nadhani hapa anamaanisha tu kuwa kama wakishinda serikari si ndio inakuwa juu ya mihimili yote na hiyo serikari lazima iwe chini ya chama husika hivyo ni automatically (serikali na chama husika) ndivyo vianaongoza inchi.
Kwa mfumo wa nchi yetu kwani kila kitu kinateuliwa au kuwa chini ya Rais basi in short chama ndio kinaongoza.
Ndio maana unawaona hata CHICHIEMU wanakiburi maana wanajua kila kitu kiko chini yao ndio maana wanafanya wanavyotaka.
 
Back
Top Bottom