Wakamatwa wakinadi nyeti za baba yao

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,720
21,778
Wakamatwa wakinadi nyeti za baba yao



Na Cresensia Kapinga,Songea

JESHI la Polisi mkoani Ruvuma limewakamata ndugu wawili wakitafuta soko la viungo vya binadamu walivyotarajia kupita kwa kumuua baba yao mzazi.Vijana hao walikamatwa wakitafuta soko hilo kwa mfanyabiashara maarufu wa mafuta katika
manispaa ya Songea.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Bw. Michael Kamuhanda alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa 6:00 usiku katika eneo la Msamala mjini hapa, kwenye ofisi ya kampuni moja ambayo inajishughulisha na uuzaji wa mafuta na usafirishaji wa abiria.

Alisema kuwa watu wawili ambao ni Mohamed Mohamed (25) na Hashim Yasin (25) wote wakazi wa Kijiji cha Hanga Monasteri wilayani Namtumbo, walifika kwenye ofisi hiyo na kumkuta mkurugenzi wa kampuni na kumueleza kuwa wana viungo vya binadamu ambavyo wanataka kumuuzia.

Baada ya mazungumzo, watu hao walikubaliana kuwa viungo hivyo ni sehemu za siri za baba yao, ambazo zingeuzwa kwa sh. milioni sita na za kaka yao kwa sh. milioni tatu.

Baada ya makubaliano hayo, mkurugenzi huyo aliwasiliana na polisi ambao waliweka mtego na kufanikiwa kuwanasa watuhumiwa hao.

Kamanda Kamuhanda alisema kuwa watuhumiwa hao baada ya kuhojiwa na polisi kuhusiana na madai hayo walikiri na kuwa walikuwa na mpango wa kwenda Tunduru kuwaua baba yao na kaka yao ili wafanikiwe kuchukua viungo hivyo na kuviuza kwa mfanyabishara huyo.






 
madogo maisha yamewachapa mpaka wamefikiria hivyo!!!!kweli hali ni mbaya kuliko inavyofikiriwa.haya maisha bora kwa kila mtanzania sijui yako wapi?
 
Huyu mfanyabiashara unaweka ndani hao unaweka ndani aiwezekani amwache mfanyabiashara kaama wakina didy aje kwako una nini wewe na viuongo vya bindamu yawezekana unanunuaga sehemu za maumbile walipokuletea hiyo ukawekea hasira..hawana maana kabisa utajiri wa kipuuzi kabisa
 
Kemea Kemeea Ndugu Kemeea kwa JIna la YESU......SHiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiindwa toka mapepooooo kwa JINA la Yesu TOkaaaaaa!
 
thanks God kwamba walikuwa hawajawaua mzee wao na kaka yao! ooh, our mercifulGod
 
JESHI la Polisi mkoani Ruvuma limewakamata ndugu wawili wakitafuta soko la viungo vya binadamu walivyotarajia kupita kwa kumuua baba yao mzazi.Vijana hao walikamatwa wakitafuta soko hilo kwa mfanyabiashara maarufu wa mafuta katika
manispaa ya Songea.

Siri kuu ya umasikini wetu ni ushirikina tu hakuna siri nyingine........badala ya watu kufanya kazi na kuwa wabunifu tumeshikilia kuamini nguvu za giza......kwa hali hii kamwe hatutaendelea..........................
 
Back
Top Bottom