Wakala Tigo Pesa adaiwa kuiba muda wa maongezi

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
WAKALA wa Tigo Pesa, Francis Aloyce (43) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam akidaiwa kuiba fedha za kampuni hiyo ya simu kwa njia ya mtandao.

Aloyce ambaye alirudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana, alifikishwa mahakamani hapo na kusomewa mashitaka mbele ya Hakimu Karim Mushi.

Wakili wa Serikali Alice Mtulo alidai kuwa Desemba 31 mwaka jana saa 12 jioni katika eneo la Azikiwe, Aloyce aliiba muda wa maongezi wa Sh 500,000 zilizotumwa kwake kupitia huduma ya Tigo pesa.

Ilidaiwa kuwa Aloyce alirushiwa fedha hizo na Vicent Mahimbo kupitia namba 0717 153134 ili aziuze na kumpelekea mteja huyo fedha lakini badala yake alizitumia kwa matumizi yake binafsi.

Mshitakiwa alikana mashitaka na kurudishwa rumande hadi Juni 13 mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.

Katika hatua nyingine mkazi wa Manzese, Ramadhan Shaban (28) amefikishwa katika Mahakama hiyo akikabiliwa na mashitaka ya kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi.

Mbele ya Hakimu Pamela Kalala, Wakili wa Serikali, Honorina Mushi alidai kuwa Aprili 12 mwaka huu saa 3 asubuhi mshitakiwa alikamatwa akiwa na dawa hizo zenye thamani ya Sh 30,000.

Mshitakiwa alikana mashitaka na kurudishwa rumande hadi Juni 13 mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.
 
Back
Top Bottom