Wajumbe wa mashina na uongozi wa serikali

Yetu Macho

JF-Expert Member
Jun 15, 2008
224
31
Viongozi

Nimekutana na kizungumkuti weekend hii nilipoenda kwa serikali ya mtaa kuomba wanijazie form flani na si mgeni kwenye mtaa ule na viongozi wananifahamu. Lakushangaza nilielezwa nipite kwanza kwa mjumbe wa shina ndiye anaetakiwa aniadikie barua kabla ya kwenda kwa serikali ya mtaa. Niliivutana na wao kuitaji ufafanuzi zaidi wa ni ipi nafasi ya mjumbe wa shina kwenye uongozi wa kiserikali bila mafanikio. sasa naileta hapa wakuu mnipe shule kidogo
1. Je, viongozi wa mashina wananafasi yeyote ktk mtiririko wa uongozi wa kiserikali?
2. Ni yapi majukumu ya viongozi wa shina? Hawa ni viongozi wa chama au serikali?
3. Kama hawa ni viongozi wa chama na si serikali, je ni hatua gani zinaweza chukuliwa dhidi ya watu hawa wanaolazimisha watu kupata baraka za serikali kupitia viongozi wa vyama vyao?
4. Je, kama viongozi hawa ni viongozi wa serikali, wanachaguliwa au wanateuliwa? wanachaguliwa kwa ucha uchaguzi gani au wanateuliwa na mamlaka gani?

Naomba uelimishaji hapa.
 
Back
Top Bottom