Wajumbe wa baraza la uwakilishi wapendekeza muungano wa mkataba bada ya wakikatiba.

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
mansoor-yussuf-himid1.jpg

Waziri asie na wizara malumu na Muwakilishi wa Kiembe Samaki Mh Mansour Yussuf Himed
[h=1][/h]Written by Foum // 20/06/2012 // Habari // 9 Comments

Mheshimiwa Mansour Yousouf Himid, Mwakilishi wa jimbo la Kiembe samaki na waziri mwandimizi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar asie na wizara maalum. Kwa keli nataka kwanza kumpongeza kaka yetu Mansour kwa ujasiri wake na mapenzi yake kwa Zanzibar na kwa Tanzania kiujumla.
Mheshimiwa Mansour, amegusia suala muhimu katika future ya muungano wetu, na ametuonyesha kwamba CCM ipo tayari kusikiliza maoni ya wazanzibar juu ya mfumo gani wanaoutaka wa muunganop wa Tanzania. Ameeleza kinaga ubaga kwamba muungano unawezekana kuendelea katika mfumo mpya wa mkataba baina ya nchi mbili huru za Tanganyika na Zanzibar kama vile muungano wan chi za ulaya.
Mheshimiwa Mansour hakumalizia hapo tu bali aliendelea kuchambuwa kwamba katika dunia ya sasa ya globalization na utandawazi ni muhimu kujuwa kwamba muungano wan chi mbili unawezekana ukaimarika zaidi bila ya nchi moja kupoteza identity ya uraia wake na asli yake, na akamalizia kwa kusema kwamba Zanzibar inaweza kufarajika zaidi katika mfumo mpya wa maelewano mazuri zaidi na Tanganyika katika mfumo wa kimkataba, huku baadhi ya sekta za serikali kubakia ndani ya miongozi ya serikali husika na baadhi kubakia katika frame work ya muungano. Aligusia pia kuhusu kiti cha UN kwamba tunaweza kurejesha kitu chetu bila ya kuvunja muungano wa udugu baina yetu na Tanganyika katika mfumo huo mpya.
Serikali ya Mheshimwa Dr. Jakaya kikwete imejitahidi sana kuondosha zile kadhia za kukandamiza wananchi, na binafsi nampongeza Rais Kikwete kwa kuwa muwazi na mpenda demokrasia ya kweli. Wale wengi waliomsikiliza Rais Kikwete katika hotuba yake ya mwanzo tangu kuchaguliwa kuwa Rais wa Tanzania watakumbuka kwamba alisisitiza kulisimamia suala la Zanzibar na kuhakikisha migogoro yote baina ya wanasiasa yanamalizika na hata migogoro ya muungano. Tuanze na kuangalia namna gani hakuingilia muundo wa katiba mpya ya Zanzibar na namna gani amewaachia wazanzibari kuamua nini wanachokitaka katika muundo wa serikali mpya. Haya maneno ya CHADEMA kwamba Rais Kikwete ni dhaifu ni kwa sababu ya mtazamo na msimamo wake juu ya Tanzania mpya yenye uhuru zaidi na Zanzibar mpya yenye nafasi inayoridhiwa na wananchi katika masuala ya muungano.
Wazanzibari tuwashukuru sana Dr Amani Karume kwa kuweka msingi madhubuti wa serikali ya umoja wa kitaifa pamoja na Maalim Seif kwa jitihada zao katima kuondosha dosari zilizodumu kwa takriban miaka 20. Kukubali kuondowa tafauti zao za kisiasa na kukaa pamoja kushirikiana pole pole kuendeleza gurudumu la maendeleo ya nchi kumepelekea nchi kurejea katika hali ya utulivu na amani ambayo yapaswa kudumishwa.
Rais Shein na Makamo wake Maalim Seif ndio kikatiba na kidemokraisia waliopewa dhamana na asilimia 98 ya wananchi kuliongoza taifa hili la Zanzibar kwa kile wananchokiamini kuwa ndicho chenye “best interest” ya nchi. Masuala ya uongozi hayataki wakuu wan chi kufuata just popular issue bali ni kipe wanachokiamini chenye interest ya wananchi na taifa kwa jumla. Wananchi waliowengi ndio waliowapa haki ya mwisho ya maamuzi yao bila ya mapingo. Kama kuna watu baina yetu wanaoamini kwamba serikali haipo sawa katika masuala kwa mfano ya kura ya m aoni basi njia iliyomadhubuti ya kupinga maamuzi ya serikali ni kwa kutumia haki yao ya kidemokrasia ya kuwa-challenge katika uchaguzi unaofuata kwa kuenda kinyume na masharti ya wapiga kura wao. Masuala ya kura ya maoni yanaweza kukubalika au kukatakiwa na serikali bila ya serikali kuwajibika kwa sababu ya ile mandate ya kura walizoshinda katika uchaguzi mkuu. Mifano ipo tele katika nchi zilizojengwa katika misingi ya demokrasia kuliko Tanzania, mfano Uingereza ambako wananchi wengi kwa miaka wamekuwa wakililia kura ya maoni ya kuitoa katika umoja wa ulaya huku serikali zote tokea ya Labour na hadi sasa ya Conservative na Libdems kuwa wawazi kwamba hawako tayari kuwapa wananchi haki yao hiyo kwa sababu kubwa kwamba hilo halikuwa katika manifesto ya chama kabla ya uchaguzi na wananchi walijuwa hilo mapema na still wakawachagua.
Mombi yangu kwa sasa kwa jamii ya wazanzibari kukaa chini na kutafakari njia mpya za kuimeguwa Zanzibar katika mfumo wa sasa potofu wa mungano kwa kutoa terms of reference mpya ya namna gani muunganon uendeshwe na kwa mfumo wa aina gani. Kama lengo kuirejesha Jamhuri ya Watu wa Zanzibar basi katika mfumo wa mkataba tunaweza kuirejesha serikali iliyohuru na kutambulika kama nchi kamili huku tukifaidika na muungano mpya uyliojengwa kwa misingi ya fairness na umoja wa kimaendeleo. Tukumbuke wazanzibari kwamba umoja wetu ndio msingi wa maendeleo makubwa ya visiwa hivi.
Tuangalie ugumu wa kura ya maoni katika mifano ifuatayo, kwanza katika daftari la wapiga kura, wanaostahili kupiga kura ya maoni ni watu wasiozidi laki sita kwa Zanzibar yote, takwimu kutoka bara zinaonyesha kwamba Daresalama peke tyake kuna watu karibu laki tatu na nusu, jee Tanzania nzima? Dhana kubwa inayowahofisha viongozi wa serikali juu ya kura ya maoni ni kwamba jee ikiwa 30% ya wazanzibari wanaoishi Zanzibar wataukubali muungano wa sasa au wa serikali moja wakiungwana mkono na wazanzibari laki tatu na nusu kutoka bara kweli kutakuwa na future ya Zanzibar huru? Au kukiwa na hang result bila ya majibu sahihi itakuwaje? Tukumbuke kwamba asilimia karibu 40 ya wazanzibari waliyapinga mapendekezo ya katiba mpya ya 2010, sasa iukiwa watajumuika na wazanzibari waishio bara itakuwaje?
Kwa upande wa upinzani mazingatio yao makubwa yalilenga katika Tume ya uchaguzi mabayo imekuwa ikiilalamikia kwa miaka zaidi ya ishirini kuwa haiku fair, wakitathmini kwamba matokeo pia yakitangazwa kinyume na matarajio yao itakuwa na impact gani kwa Zanzibar mpya? Solution kubwa iliyowafikiwa kwa wote ni kuwaachia wananchi kutoa maoni ya mfumo upi wanautaka na serikali kulinda maamuzi ya wanchi hao na ndio maana kura ya maoni ya kuwepoi au kutokuwepo kwa muungano imekuwa nngumu kuwaendorse na wanasiasa wengi wa visiwani kwa hofu hiyo.
Katika mfumo mpya wa mkataba Zanzibar itaweza kurejesha mamlaka yake ilyoyapoteza tokea kuunganika Tanganyika na Zanzibar, huku muungano ukilenga masula ya kiserikali yasiyoingilian na uhuru wa kitaifa au maamuzi ya maslahi ya taifa la wazanzibari. Ndio tukasema katika mfumo huu wa mikataba kila mzanzibari ni mshindi, kwa wapenda muungano (wale asilimia 40 zanzibar na wazanzibari wanaoishi Tanzania Bara) hawatakuwa na ile immediate khofu ya kupoteza mali zao walizozichuma kwa jasho lao, wale wanaopendezewa kuerejea kwa jamhuri ya watu wa Zanzibar kwanza basi pia kiu yao kitakuwa imepatiwa ufumbuzi kwani muungano wa kimkataba hauondoshi utaifa wa nchgi zilizoungana na mwisho nwasioutaka muungano kabisa watakuwa na haki ya kuuukataa kata kata katika kura ya maoni kwa yale yaliyopendekezwa kuwamo katika muungano au katika chaguzi zijazo.
Wazanzibari tusahau tafauti zetu na tuachane na masuala ya wapi asili zetu zimetokea tukae pamoja kushiriki kikamilifu katika zoezi la kuirejesha Zanzibar katika ramani ya kimataifa. Kubakia kwa muungano kunawezekana bila ya kupoteza utaifa wetu. Tutapokaa tukabishana na kupigana miongoni mwetu basi ni sawa na vita vya panzi faida kwa kunguru. Hivi tutathmini kwamba kura ya maoni ndio njia pekee ya kuirejesha Zanzibar katika mamlaka ya uhuru pekee? Ikiwa njia hii imeweza kutumiwa kuwagonganisha wazanzibari wenyewe kwa wenyewe, jee ni hekima kushikilia msimamo huo huku tukijuwa inaweza kuwagawa wazanzibari katika makundi yatayoimega Zanzibar kidogo kidogo? Kama ipo alternative kwa nini tusitumie alternative mpya yenye kuleta msimamo mmoja wa wazanzibari wote? Hebu tukae chini tufikiri kwani kura ya maoni hazijapigwa tokea mwaka 1995 mpaka 2000 na jee result hazijulikani? Tafauti gani ya miaka ya nyuma na sasa wakati system ndio ile ile? Tufikiri namna gani Scotland imeweka strategies za kushinda kura ya maoni yao, kwanza referendum yao inmepangwa kupigwa katika mwaka 2014 kwa sababu ndio historia ya Scotland ya kujitenga inapokuwa significant, jengine ni kuhakikisha hata wale wenye miaka 16 wanapiga kura kwa sababu wnaanjuwa vijana wengi ndio wnaaosupport kujitenga kwao. Kwa sisi wazanzibari nini sytrategies zetu katika kura ya maoni? Jee haitakuja kututia shimoni zaidi ikiwa Tume itaamua kutangaza matokeo yasio sahih? Au tuseme haya masuala ninayoyauliza ni ndoto zaidi kuliko reality ilivyo?
Kama wametupa terms of reference katika kujadili katiba mpya wakisistiza kujadili kuvunja muungano ni kosa la jinai basi kwa nini tushindane nao kimaguvu wakati nafasi na sisi tunayo ya kuwapa hadidu rejea zetu (terms of reference) ya namna gani mfumo mpya wa muungano tunaoutaka? Hivi sote tukisema tunataka muungano wa kimkataba wenye lengo la kuirejesha Jamhuri ya watu wa Zanzibar hatutafaidika na umoja wetu. Akushindae kwa matonge mshinde kwa kutoelea

Baraza la Wawakilishi Chukwani Z'bar
 
Back
Top Bottom