Wajukuu wa Jaji Warioba watekwa;Wapatikana baada ya msako...

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
amka2.gif

WATU wawili wakazi wa jijini Dar es Salaam wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuwateka wajukuu wa aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba.
Wajukuu wake hao ni pamoja na Joseph Warioba (5) na Kyara Warioba (4) na mwenzao Stephano Mworia (4) ambao walitekwa pamoja na gari walilokuwamo.
Kwa mujibu wa taarifa za kipolisi, watuhumiwa ambao wanaendelea kuhojiwa kwa tuhuma za kuwateka ni Juma Shaaban (25) mkazi wa Mwembechai na Faridi Kadau (33) wa Magomeni Kagera.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni aliwaambia waandishi wa habari ofisini kwake kuwa tukio hilo lilitokea Machi 6 mwaka huu majira ya saa 9.49 alasiri katika baa ya Q iliyoko Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Alisema siku hiyo mlalamikaji alitoa taarifa kituo cha polisi Oysterbay Machi 6, mwaka huu.
“Mwanamke Rosaline Mworia mkazi wa Oysterbay alitoa taarifa kuwa aliegesha gari lake aina ya Suzuki lenye namba T 959 AZC likiwa na watoto watatu kisha akaingia baa kwa ajili ya kuchukua chakula,” alisema Kenyela.
Alisema baada ya mwanamke huyo kutoka ndani ya baa hiyo hakulikuta gari ambalo lilikuwa na watoto hao watatu ndipo alipoamua kwenda kuripoti polisi.
Alisema baada ya taarifa hizo polisi walifanya ufuatiliaji na kufanikiwa kulikamata gari hilo siku hiyo hiyo majira ya saa 11.30 jioni katika eneo la Magomeni Mwembechai likiwa na watoto hao pamoja na watuhumiwa.
“…Watoto hao walishatambuliwa na wazazi wao pamoja na gari lililoibwa na tunaendelea kuwahoji watuhumiwa hawa,” alisema Kenyela. Mmoja wa watu walio karibu na familia ya Jaji Warioba, alithibitisha kuwa watoto wawili kati ya waliotekwa, Joseph na Kyara, ni watoto wa Kippi Warioba ambaye ni mtoto wa Jaji Joseph Warioba. Hali kadhalika imefahamika kuwa siku ya tukio, walikuwa na mama yao Rosaline Mworia
 
amka2.gif

WATU wawili wakazi wa jijini Dar es Salaam wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuwateka wajukuu wa aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba.
Wajukuu wake hao ni pamoja na Joseph Warioba (5) na Kyara Warioba (4) na mwenzao Stephano Mworia (4) ambao walitekwa pamoja na gari walilokuwamo.
Kwa mujibu wa taarifa za kipolisi, watuhumiwa ambao wanaendelea kuhojiwa kwa tuhuma za kuwateka ni Juma Shaaban (25) mkazi wa Mwembechai na Faridi Kadau (33) wa Magomeni Kagera.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni aliwaambia waandishi wa habari ofisini kwake kuwa tukio hilo lilitokea Machi 6 mwaka huu majira ya saa 9.49 alasiri katika baa ya Q iliyoko Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Alisema siku hiyo mlalamikaji alitoa taarifa kituo cha polisi Oysterbay Machi 6, mwaka huu.
"Mwanamke Rosaline Mworia mkazi wa Oysterbay alitoa taarifa kuwa aliegesha gari lake aina ya Suzuki lenye namba T 959 AZC likiwa na watoto watatu kisha akaingia baa kwa ajili ya kuchukua chakula," alisema Kenyela.
Alisema baada ya mwanamke huyo kutoka ndani ya baa hiyo hakulikuta gari ambalo lilikuwa na watoto hao watatu ndipo alipoamua kwenda kuripoti polisi.
Alisema baada ya taarifa hizo polisi walifanya ufuatiliaji na kufanikiwa kulikamata gari hilo siku hiyo hiyo majira ya saa 11.30 jioni katika eneo la Magomeni Mwembechai likiwa na watoto hao pamoja na watuhumiwa.
"…Watoto hao walishatambuliwa na wazazi wao pamoja na gari lililoibwa na tunaendelea kuwahoji watuhumiwa hawa," alisema Kenyela. Mmoja wa watu walio karibu na familia ya Jaji Warioba, alithibitisha kuwa watoto wawili kati ya waliotekwa, Joseph na Kyara, ni watoto wa Kippi Warioba ambaye ni mtoto wa Jaji Joseph Warioba. Hali kadhalika imefahamika kuwa siku ya tukio, walikuwa na mama yao Rosaline Mworia
Jaji Warioba ameanza misukosuko siku nyingi
 
Back
Top Bottom