Wajifungua kwa kutumia mwanga simu

Dingswayo

JF-Expert Member
May 26, 2009
4,019
2,923
Sunday, 11 December 2011 09:45
Na Sanjito Msafiri, Kibaha

MADAKTARI na wauguzi wa Kituo cha Afya Muhoro, Rufiji mkoani Pwani wanalazimika kutumia mwanga wa tochi ya simu ya mkononi usiku kuzalisha wajawazito wanaofika kituoni hapo.
Hayo yamebainishwa na Mganga Msaidizi wa Kituo hicho, Idd Hassan juzi alipokuwa akisoma taarifa na changamoto mbalimbali zinazokikabili kituo hicho katika utoaji huduma.

Idd alisema kutokana na kituo hicho kuwa kikubwa ndani ya wilaya hiyo kinatoa huduma kwa wagonjwa wa matatizo mbalimbali zikiwamo kuzalisha wanawake wajawazito, lakini ukosefu wa umeme umekuwa ni tatizo kubwa linaloathiri utendaji wa kazi.

Alisema kazi ya kuhudumia wajawazito wakati wanapojifungua hasa nyakati za usiku ni ngumu na inahitaji mwanga wa kutosha, lakini kutokana na hali hiyo, wamekuwa wakiifanya kazi hiyo katika mazingira magumu.
Mganga huyo alisema wameshapeleka malalamiko mara kadhaa kwa uongozi wa juu, lakini cha kushangaza wamekuwa wakiahidiwa bila ya utekelezaji.

" Kutokana na kazi tunazofanya umeme ni muhimu sana maana kinamama wengine wanakuja na matatizo makubwa sasa mwanga wa tochi ya simu hauwezi kuhimili na kumuwezesha mtoa huduma kuona vizuri,"alisema.

Aliomba uongozi wa mkoa kuliangalia kwa jicho la huruma ombi lao ili kuwapatia umeme ilikurahisisha ufanisi hospitalini hapo.Akijibu juu ya ombi hilo, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza alisema amelisikia, atahakikisha linafanyiwa kazi kwa kipindi muafaka ili kuondokana na adha hiyo.

Mwantumu alisema kwakuwa kwa sasa anaendelea na utaratibu wa kukutana na idara zote za mkoa kubaini matatizo na kero mbalimbali zinazowakabili, hivyo atalijadili kwa kina tatizo hilo atakapokutana na wafanyakazi wa idara ya afya.



Wajifungua kwa kutumia mwanga simu
 
miaka 50 baada ya uhuru.
tumethubutu, tumeweza na tunazidi kusonga mbele.
 
Hii habari mfowardie Paschal Mayala anaesema tumejitahidi kimaendeleo katika miaka hii 50!!!
Usiache kumwambia pia ziko hospitali ZA RUFAA (ikiwamo Muhimbili) ambazo wagonjwa wanalala CHINI,
Wakati pia mpaka leo kuna shule za Chini Ya Mti Primary School,
Nyoka akidondoka kutoka mtini Mapumziko,
Mvua zikianza Likizo!!
 
Back
Top Bottom