Wajibu wetu ni nini?

Amoeba

JF-Expert Member
Aug 20, 2009
3,289
781
Wakuu wana-JF! Binafsi nimekuwa hapa JF kwa muda mrefu sasa, shukrani kwa maxence na wote walio nyuma ya JF: Jukwaa hili sasa ni kutaniko kuu la Vijana, Wazee, Wasomi, Wanasiasa (Vyama Vyote) na watu wa kada zote. Pia nafarijika sana napokutana na Nguli wa siasa za Tanzania, Japo wengine tunaficha majina lakn lengo linabaki moja-Kuijenga msingi wa maendeleo ya TANZANIA.

Mimi si mchambuzi wa siasa, lakn Kulingana na muenendo wa siasa za nchi yetu kwa miaka ya karibuni, ni dhahiri kabisa kuwa CCM, CHADEMA na CUF ndiyo vyama pekee ambavyo vinawanachama na wafuasi wengi katika Mikoa yote ya Tanzania, hii inatokana na ama sera ziletazo matumaini au ushabiki wa kawaida kama wa simba na yanga, makundi yote hayo hukipa uhai chama, japo kundi la pili linaleta mashaka kidogo-Ushabiki. Ushabiki usingekuwa na tabu sana kama ungeonekana vijiweni, lakn inatia mashaka kiasi kama suala la ushabiki linakuwa kipaumbele kwa wanachama wengi wa JF (The Home of Great Thinkers)! Inakuwa ngumu kuingia akili pale Kijana wa kitanzania anaposhabikia hoja zenye muelekeo hasi kwa maendeleo ya nchi yetu, ati kwa sababu tu ya u-CHADEMA, u-CCM, au u-CUF!

Hivi wajibu kwa nchi yetu na vizazi vyetu vijavyo ni upi? Hivi kuna muda ambao tunawaza huru bila kuathiriwa na imani zetu za kichama? Hivi kuna muda ambao tunajadili mada ki-great thinker kweli! Lugha zenye utata na mielekeo hasi ziko dhahiri hapa JF, tena kauli nyingine zinatoka miongoni mwa viongozi wetu, ndiyo: Haiingii akilini Mbunge, Waziri au Raisi (aliye madarakani au mtarajiwa) anatetea hoja hasi kwa nguvu ya kushangaza. Hivi kweli siasa za Tanzania zimefikia hatua ya kutuma Majeshi ya kuchafua katika Mitandao. Siyo siri kuna vijana wanalipwa na vyama kuja JF kuleta propaganda za uchafuzi (vyama vyote)!

Sioni kabisa muelekeo wa nchi kwa sr tunazosimamia, hasa sisi vijana. Ulishawahi kujiuliza Tanzania itakuwa katika hali gani miaka ishirini ijayo? Ulishafanya nini kuleta impact katika future ya Tanzania pendwa? Tutake tusitake, Tanzania ni nchi yetu; itajengwa ama kubomolewa na sisi wenyewe! Maandishi ttunayoandika humu yatabaki, na yatatushitaki katika nyakati!

Ningefurahi kama mods wangeiweka thread hii sehemu inayoonekana vyema, ili kila awaye aisome; HUENDA WATU TUKAUMIA VICHWA VYETU KUFIKIRI!

Asanteni kwa kuniskiliza!
 
mkuu vijana wa kinepi ndo wapo wengi sana humu, japo hata vijana wa magwanda pia wapo.
 
Si mbaya mkuu kuwa na vijana wa CDM, CCM, CUF, na vyama vyote! Alimradi tu wasimamie maslahi ya UMMA, na si maslahi ya "mabwana" wao na matumbo yao! They are a shame!
 
Back
Top Bottom