Wajenzi wa Barabara Nelson Mandela wanawakomoa wakazi wa Tabata

Iga

Senior Member
Dec 17, 2007
112
6
STAILI ya ujenzi wa barabara ya Mandela katika kipande kati ya Buguruni na Ubungo kinatutia wananchi hofu kwamba huenda wajenzi hao wanafanya makusudi ili tuteseke bila sababu ya kuridhisha.

Hivi katika barabara yenye njia mbili unawezaje ukawa unajenga njia zote kwa wakati mmoja. Na siyo hayo tu bado unalundika mchanga kati na pembeni ya njia huku ukijua fika hilo linakwamisha wengi kwa kuwaweka wengi kwenye 'strait jacket'.

Na hivi jamaa hawa wameshindwa kuchanja njia zingine za kutosha ili wanaokwenda kushoto a u kulia na wamekaribia kuingia makwao waondoke kwenye foleni?

Hivi hapawezi kutumika taa za barabarani za dharura kuongoza madereva ili kuepuka ile tabia mbaya ya kila mmoja kutaka kufika kwanza aendako ili hali kila mtu kachelewa kutoka alikotoka ?

Kwa haya yote ninawaomba wanajamii forums kutafakari uwezekano wa kuanzisha taasisi kama HAKI ELIMU kwa majina vile nilizoorodhesha hapo chini:


HakiSafari
HakiNjia
HakiBarabara


Ili ziwe zinakumbusha watu waache kuwasababishia wenzao matatizo wanapokuwepo mabarabarani,

Iga
 
inawezekana wanasumbuliwa malipo na serikali ndo maana wanafanya hayo ili kuikera serikali.
 
Back
Top Bottom