Wajanja watia ndani 40m za Arusha Football Club

Mantisa

JF-Expert Member
Dec 20, 2010
322
236
Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Arusha Football Club( AFC) inayoshiriki ligi ya Vodacom premium league unaeleza kuwa kuna wajanja wachache wanaonufaika sana na timu ambao kwa muonekano huonekana wako mstari wa mbele katika kusaidia timu hiyo.

Hii ni kutokana na ukweli kwamba wajanja hao mwaka jana waliandika proposal na kuipeleka TANAPA kwa ajili ya kuomba pesa ili kufanikisaha kulipia gharama zote za uendeshaji wa kituo cha mashindano ya ligi daraja la kwanza taifa hatua ya fainali ili fanali hizo zifanyike katika kituo chenu mnatakiwa kuihakikishia TFF kuwa mna uwezo wa kulipia gharama za uendeshaji ikiwa ni pamoja na kuwalipa waamuzi posho zao, chakula, usafiri , msimamizi wa kituo pamoja na timu zitakazokuwa kwenye kituo hicho

Hata hivyo uongozi wa mpira wa mguu haukuwa na uwezo huo ukaona ni bora kuomba udhamini TANAPA. Ombi hilo lilikubaliwa ila malipo yalichelewa kutoka yakakuta mashindano yameshaisha. Hivyo basi wajanja hao wakaona ndo muda muafaka wa kuziitia pesa hizo ndani

AFC ilifanikiwa kupanda daraja na kuanza tena kutafuta udhamini ndipo ikagonga tena hodi TANAPA na kukutana na taarifa kuwa zile pesa zilishatoka na wanataka kujua zilitumikaje?

Kimsingi waliochukua wanajulikana. Sasa sijui kwa nini yafuatayo hayafanyiki?


  1. Kwa nini wasirudishe pesa hizo?
  2. Kwa nini walichukua pesa za timu na wakaweka kwenye account yao na kuanza kuzituma?
  3. TAKUKURU wanajua jambo hili, kwa nini wamekaa kimya?
 
Back
Top Bottom