Wajanja wa Mgodini wachota mamilioni NSSF

Mongoiwe

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
524
263
Wajanja wachota mamilioni NSSF Send to a friend Sunday, 27 March 2011 05:43 Frederick Katulanda, Geita
WAKATI shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kilifikiria kuwekeza zaidi fedha za wanachama wake katika uzalishaji wa Umeme, imebainika kuwa wajanja wamefanikiwa kupeleka vielelezo vya uongo na kuchota mamilioni kwa kulipwa mafao yao wakati wakiendelea na kazi.

Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi Jumapili kwa muda mrefu sasa umebaini kuwa tangu mwaka 2008 hadi Februari 2011 jumla ya wafanyakazi 40 wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) ambao majina yao tunayo walilipwa mafao yao kwa kupeleka vielelezo vya kughushi kuwa hawako kazini, huku wakiwa bado wanaendelea na kazi mgodini humo.

NSSF ilianzishwa kwa Sheria ya Bunge namba 8 ya mwaka 1997, sheria hiyo pamoja na mambo mengine imelenga kulinda maslahi ya mfanyakazi muda wote awapo kazini, baada ya kustaafu, baada ya kifo chake na hata maslahi ya watu wake wanaobaki pindi anapofariki dunia.

Hata hivyo, Sheria hiyo inaruhusu mfanyakazi kulipwa mafao yake pindi anaposimamishwa kazi ama kuacha kazi kulingana na muda ambao amechangia wakati akiwa kazini, jambo ambalo limetoa mwanya kwa wafanyakazi hao kughushi barua hizo na kulipwa mafao.

Akizungumza na gazeti hili Meneja wa NSSF Mkoa wa Geita Nyabuyonza Kilondera alikiri kuwepo kwa hujuma hiyo, lakini alisema kuwa hawezi kulizungumzia suala hilo kwa undani akidai kwamba anahitaji muda kupitia nyaraka mbalimbali za ofisi yake kujua ukweli wa tukio hilo.

"Mimi ndio nimefika kuchukua nafasi ya meneja hapa, nina siku tatu, pengine nipate muda wa kutosha kupitia nyaraka nilizokabidhiwa na ofisi hapo ndipo nitakuwa kwenye nafasi nzuri ya kulizungumzia hilo," alisema.

Hata hivyo uchunguzi zaidi umebaini kuwa baadhi ya wafanyakazi wa mgodi huo kwa kushirikiana na maofisa wa ofisi ya raslimali watu (HR) na baadhi ya wafanyakazi wa NSSF wamekuwa wakichota mafao yao kwa makubaliano ya kuwaachia sehemu ya fedha za mafao maofisa wa NSSF.

Habari hizo zinaonyesha kuwa watendaji hao wa NSSF huachiwa kati ya Sh 1 milioni hadi Sh 2.5 milioni na wateja hao wanaojichotea na fedha hizo huongezeka kutegemea kiasi cha mafao yanayochotwa.

Taarifa zinaonyesha kuwa wafanyakazi wa mgodi huo wamekuwa wakighushi barua za kusimamishwa kazi au kuacha kazi pamoja na barua za uthibitisho wa kuwa watumishi wa mgodi huo ambayo kwa utaratibu hutolewa na mgodi kumthibitisha mhusika kwamba alikuwa mtumishi wake na kuziwasilisha katika ofisi za NSSF Geita ambapo na huandaliwa mafao yao.

Habari zaidi zinaeleza kuwa katika mpango huo wafanyakazi hao wa GGM walikuwa wakighushi barua za mwajiri zikiwa na sahihi halali za meneja mwajiri, meneja mwajiri Utawala pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa mgodi huo na kuziwakilisha NSSF zikiwa na fomu ya madai ya mafao ya NSSF ambayo hujazwa na mwajiri kitengo cha raslimali watu na huwachukua siku 14 kuweza kujichotea mafao hayo kwa ujanja.

“GGM ni mteja mkubwa kwetu NSSF, tunao wanachama wengi toka mgodini lakini pia kwa mazingira ya kazi yao iwapo mtumishi huyo wa mgodi akiacha kazi na kuwa na vielelezo, basi humchukua wiki mbili ama tatu mpaka kukamilisha taratibu na kulipwa,” alieleza mmoja wa mtumishi wa NSSF ambaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini.

Taarifa zaidi toka GGM ambazo pia zimethibitishwa na afisa uhusiano wa mgodi huo Ahmed Merere zimedai kuwepo kwa hujuma hiyo ambayo kwa sasa imeanza kuchunguzwa na uongozi wa mgodi huo huku wafanyakazi watatu wakisimamishwa kazi kwa ajili ya uchunguzi huo.

“Inasemekana hivyo lakini uongozi wa mgodi umeamua kulifanyia kazi kuanzisha uchunguzi wake ili kubaini ukweli wake, kwa sasa wamewasiliana na uongozi wa NSSF kuomba kupatiwa orodha ya wafanyakazi wote mgodi ambao wamekwishalipwa mafao yao katika kipindi cha miaka miwili iliyopita ili kulinganisha na rekodi zake kubaini waliohusika na hujuma hiyo,” alieleza Merere bila ya kufafanua kwa kina.

Hata hivyo wakati mgodi huo ukidai kuanza uchunguzi, imedaiwa kuwa wafanyakazi ambao mpaka ndiyo wanaoongoza kunufaika na hujuma hivyo kinyume na sheria ni wale wenye ngazi ya kati ya mshahara ambao wengine ni wafanyakazi wa kawaida na wengine ni wasimamizi wa vitengo mbalimbali vya mgodi huo.

“Katika mpango huu kuna baadhi ya wafanyakazi ambao waliwasilisha termination letter wengine Resignation letter pamoja na Certificate of service, vyote hivi vilikuwa na sahihi za uongozi wa juu wa mgodi na kulipwa mafao yao.” Kilieleza chanzo chetu kimoja toka NSSF.
 
Kama wame "forge" hizo shahada za kuachishwa kazi au wameshirikian na baadhi ya watu wa idara ya malipo NSSF inabidi wote wachukuliwe hatua za kisheria. Lakini, kama waliachishwa kweli kazi, halafu baada ya muda wakarudishwa kazini, na wakati huo walishalipwa mafao yao, sioni kama kuna tatizo hapo.
 
Ukiachisha kazi, hakuna tatizo lakini hawa inaonekana wako kazini wameghushi barua hili ndiyo tatizo na wote wako kazini haionyeshi kuacha kazi
 
Hapo hakuna any serious issue. Si wanachukua michango yao? Mbona hao mafisadi wanachota kwenye mfuko kiujanja janja tu bila kuwashirikisha wadau wenyewe?
 
Back
Top Bottom