wajamani huyu mama sasa habanduki mawazoni kwangu............

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,172
Sijui mama huyu kanifanyizia nini kwani najisikia amenielemea,
Tangia akiwa kinda nilimpenda kikwelikweli naye kujulishwa.....
Naye nahisi alinipenda japo hakunambia kiuwaziwazi........
Walakini wapambe wake walimjongelea naye kunitupia virago,
Wajamani huyu mama sasa habanduki mawazoni kwangu!

Kutokana na majukumu siko radhi kumshtua
Ninaamini naye huniwazawaza pamoja anipigia ganzi
Sijui ana nini huyu mama mbona anitawala hivyo?
Mengi hutafakari na hamu ya kurudisha siku kunizingira,
Wajamani huyu mama sasa habanduki mawazoni kwangu!

Sijui ni lipi ningeliboresha ili hadi leo tungelikuwa sote.
Najua yu mtaani akitesa na mwingineo bila zengwe
Mara kwa mara hutikisa kichwa kwa majonzi na kutaabika
Kisa nikumkosa kuwa ndani ya maisha yangu na kutojua la kufanya
Wajamani huyu mama sasa habanduki mawazoni kwangu!

La kushangaza ni kuwa hata wakati wa mahaba ni yeye kutia fora!
Nisipofanya hivyo sipatwi na mpango wa nyevu endelevu!
Hivi haya ayajua au mie tayari amenikitisha kwenye kapu lake?
Mie sitamtonya kwa kukhofu kuanzisha vagi....acha niteseke tu mwaya!

Wajamani huyu mama sasa habanduki mawazoni kwangu!

Inspired by this piquant narrative......I can't get her out of my mind

..........jisomee mwenyewe kama waujua umombo au ridhika na hamirojo yanguhttp://www.standardmedia.co.ke/rela...&cid=431&story=I can’t get her out of my mind

Ruta so nice
Nakukubali sana na kipaji chako na the way ulivyotulia kuweka mawazo yako

May be upige hatua zaidi kutafuta namna ya kumweka karibu maana inawezekana umemweka mbali sana na himaya yako
bado una nafasi ya kufanya hivyo kabla hujaumia moyo zaidi
 
he ,ruta umeona leo ufichue sir? haha pole sana ,, kama unaona vip mzukie ummwagie mistari iyo,u never now ,amini secnd chance best ,,, s sadddddd
 
Pole ndugu yangu,wapambe ni watu wabaya sn. Jitahidi kama unaweza mtafute umwambie ukweli wa mambo yalivyokuwa na jinsi wapambe walivyotia fitna kwenye penzi lenu. Nina imani atakusikiliza tu.
 
La kushangaza ni kuwa hata wakati wa mahaba ni yeye kutia fora!
Nisipofanya hivyo sipatwi na mpango wa nyevu endelevu!
Hivi haya ayajua au mie tayari amenikitisha kwenye kapu lake?
Mie sitamtonya kwa kukhofu kuanzisha vagi....acha niteseke tu mwaya!

Wajamani huyu mama sasa habanduki mawazoni kwangu!
Ahaaaaaa...Ruta banaa...lol
 
Ruta huyo mwanamama hana roho ya paka mmwagie tu hiyo mistari atayeyuka kama samli motoni maana naye anakuzimikia.
 
Ruta so nice
Nakukubali sana na kipaji chako na the way ulivyotulia kuweka mawazo yako

May be upige hatua zaidi kutafuta namna ya kumweka karibu maana inawezekana umemweka mbali sana na himaya yako
bado una nafasi ya kufanya hivyo kabla hujaumia moyo zaidi

ana mtu si wajua vagi la kumchomoa wa mwingine,......acha nivumilie maumivu haya ndiyo maisha........[MENTION]@Mr Rocky[/MENTION]
 
Walakini wapambe wake walimjongelea naye kunitupia virago,

Najua yu mtaani akitesa na mwingineo bila zengwe

Ninaamini naye huniwazawaza pamoja anipigia ganzi...???????

Mbona mawazo yanapingana hapo juu....amekutupia virago, anatesa na wengine....lakini bado anakuwaza na kukupigia ganzi?

Huko ni kutafuta ugonjwa wa moyo bure bilashi. Au ule msemo wa "mwenye mapenzi haoni ingawa macho anayo" unafanyakazi yake kwako?

Ushauri, kwanza kamuone daktari wa macho kabla hujachukua hatua yoyote nyengine.
 
ndugu yangu wanawake watakuuwa sasa,yaan namba zote unacheza nazo nikianza L,XL,XXL,XXXL,XXXXL size zote tafuta size yako ili mechi iwe sawa sa we kila mara unafungiwa nyumbani.
ummu kulthum.....usichojua ni kuwa kupenda ni ugonjwa siyo kazi ya kutafuta mwingineo...............ni lazima awe yeye nayye sioni mwelekeo...........kwa hiyo ni lazima nikubali yaishie...[MENTION]@ummu kulthum[/MENTION]
 
pole kaka......
hata mimi kuna mtu habanduki mawazoni mwangu humu jf
na kuwa nae siwezi wala sitaki ,wala yeye hataki ..... hata situation hairuhusu.... soo painful

labda ni Mr Rocky nini ambaye unamuwazawaza naye anakuwazawaza? [MENTION]Smile, Mr Rocky[/MENTION]
 
Last edited by a moderator:
Afu mbaya zaidi huko aliko awe anajaliwa sana...dah nakupa pole rafiki yangu,hawezi kukukumbuka.
ana mtu si wajua vagi la kumchomoa wa mwingine,......acha nivumilie maumivu haya ndiyo maisha........[MENTION]@Mr Rocky[/MENTION]
 
Ukisikia ukubwa dawa ndio hivyooo! ungeanza na visamaki vidogo vidogo, wewe umekimbilia PAPA mwenzangu,ndio mana unapenda sana nyimbo za ma LOVE kumbeeeeeeeeeee sana nimekupata Ruta. LOL
 
Back
Top Bottom