Waislamu tukatae udini wa akina Ponda

They r talkin bout christianity as a proper way of livin n islam as a satanic
ask them how did their ancestors survived to live before the introduction of colonialsim n christianity in this continent??
Du they now agree with them whites that their ancestors were satanic n pagans n that this white religion is a proper n perfect religion??du they now deny their origination n agree with whites religion that they comin from a cursed generation??
 
Kwa maoni yangu sikubaliani na mtu wa dini yeyote kufanya fujo, kuua, au kutoa kashfa kwa binadamu mwenzie kwa kisingizio cha kutetea dini yake.

Hivi, nyie watanzania ngoja niwaulize: mnajiharibia Amani yenu kwa sababu ya dini ambazo mmeletewa na wageni? Kwa nini msithamini utanzania wenu kwanza! Udini baadae? Tena baadhi yetu katika hata ukoo mmoja kuna waislamu na wakristu! Wengine mme na mke dini tofauti. Kwa nini we kama una dini yako unayoamini itakufikisha mbinguni kwa nini udharau ya mwenzio?

Mimi narudia tena; nashangaa sana waislamu wanaomfuata Ponda. Ponda hasimamii misingi ya kiislamu, ponda akili yake haiko sawa, ponda ni wale watu kwa Kiingereza wanaitwa psychopath.

Halafu, waungwana kitendo cha mtoto kukojolea msaafu baada ya mabishano na mwenzake chawezaje kuwa ni kitendo cha dini moja kukashifu dini nyingine? Je dini ya kiislamu inatufundisha tuwe na akili za kitoto au ki uwendawazimu kama akili za ponda? La hasha! Dini ya kiislamu ni dini ya kweli ya Allah na inafundisha yaliyo mema kutoka kwa mwenyezi mungu. Kwa hiyo waislamu wa kweli tuachane na vurugu za Ponda kwa sababu ponda hasimamii misingi ya dini ya kiislamu
 
Well said mtoa mada, hawa wenzetu wanacreate mambo yasiyokuwepo ili kutimiza waliyokusudia, busara kwao ni sifuri wanachojua ni kutumia nguvu tu, nchi nyingi duniani zenye vita source ni hawa 'wenzetu'. Lord have mercy!
 
Nchi yetu iko katika hatari kubwa ya kuingia katika machafuko ya kidini yanayotokana na kufumbiwa macho chokochoko za kidini ambazo zimeanza muda mrefu sasa. Uvumilivu miongoni mwa waumini wa dini kuu chini yaani uislamu na ukristo ambao umekuwepo nchini toka uhuru sasa unatoweka kwa kasi ya ajabu.

Nimesoma kinachoitwa "waraka wa waislamu" nimeweka inverted commas kwa sababu sikubaliani kabisa na title hiyo. Kilichomo ndani ya waraka huo hakina sifa ya kuitwa waraka wa waislamu kwani ni dhihaka na tusi kubwa kwa waislamu wengi ambao ni wastaarabu, wastahimilivu na wasomi. waraka umejaa ujinga mtupu ukisherehesha na matukio ya kubuni ya uongo na ya kiwango cha chini sana ndiyo maana nasema haustahili kuitwa waraka wa waislamu, ungefaa kuitwa "waraka wa ponda kwa waislamu ambao ni wajinga"

Waraka unajaribu kutuaminisha kuwa Mhe Hadji Mponda na Mhe. Mustapha Mkullo walipoteza nafasi zao za uwaziri kwa shinikizo la wakristo bila kujali tuhuma mbalimbali zilizoelekezwa kwao ikiwamo ubadhirifu na kushindwa kumudu majukumu yao. Tunafahamu Mhe Mponda alishindwa kushughulikia ipasavyo mgogoro wa madaktari na serikali, pia ili lazimu awajibike kwakuwa MSD iliyo chini ya wizara yake ililitia hasara taifa la zaidi ya shs 5bilioni kwa kusababisha dawa zenye thamani ya pesa hiyo kuharibika kwa kufikia mwisho wa muda wake wa matumizi(expiry) bila kuzisambaza mahospitalini ambako zilikuwa zikihitajika sana na wagonjwa wakifariki kwa kuzikosa dawa hizo. Pamoja na Mhe Mponda mwingine aliyewajibika katika hili ni Mhe Dr Lucy Nkya aliyekuwa naibu waziri, lakini waraka haumtaji kwa kuwa ni mkristo hivyo hoja ya udini inayojengwa itavurugika.

Mhe Mkulo pamoja na kushindwa kabisa majukumu yake kama waziri wa fedha alikuwa na tuhuma za kuuza kinyemela kwa kampuni ya METL kiwanja mali ya PSRC. Pia Mkulo alishinikiza kuvunjwa kwa taasisi ya CONSOLIDATED HOLDING LIMITED na kuhamishiwa shughuli zake kwa msajili wa hazina. Hapa lengo lilikuwa ni kuwalinda wadaiwa sugu ambao bado hawajamaliza kulipa madeni yatokanayo na ununuzi wa mashirika ya umma. CHL ni mrithi wa iliyokuwa ikiitwa PSRC. Mhe Zitto Kabwe ndiye aliyeibua sakata hili lakini waraka haumtaji kwakuwa ni muislamu ili kujenga dhana kuwa Mkullo aling'olewa kwa shinikizo la wakristo.

Waraka una maelezo marefu lakini yasiyoeleweka juu ya chadema kuwa chama cha kikristo ambacho waislamu tumetakiwa kujiepusha nacho bila kutueleza na kutuelekeza chama cha kukiunga mkono ambacho bila shaka ni cha kiislamu. Jambo lingine ni mali nyingi zinazomilikiwa na makanisa kuwa eti imewezeshwa na mfumo kristo uliopo nchini. Nasema huu ni ujinga na uongo wa mchana kweupe kwani taasisi za kikristo toka kabla ya uhuru pamoja na kuandaa waumini wao kiroho hazipata kuwa nyuma katika kushughulikia huduma za kijamii kwa waumini wao pamoja na wasiokuwa wakristo. Wakristo walimiliki shule na hospitali nyingi ambazo zimehudumia watanzania wote bila ubaguzi. Baba yabgu mzazi ambaye ni mwislamu alisoma katika shule za kikristo yaani st mary na st andrews. Shukrani za pekee kwa baba wa taifa(mkristo) ambaye alitaifisha shule za kanisa ili kuwezesha waislamu kusoma katika shule hizo, pamoja na hatua hiyo ya kizalendo kuna waislamu wenzetu ambao wanamdhihaki mzee huyo kwa udini, huku ni kukosa shukrani kwa kiwango cha juu sana.

Najiuliza bila hatua hiyo ya Nyerere wazee wetu wa kiislamu wangesoma wapi ilhali Mazengo sec schoo, Mkwawa sec. school, Tosamaganga, Musoma alliance, Pugu, Minaki, Malangali, Rugambwa, Forodhani zilikuwa mali ya madhehebu ya kikristo. Narudia kuandika tena kuwa waraka huu ni janga na ni kielelezo kuwa waislamu bado tunasafari ndefu ya kuutokomeza ujinga kama wanaojiita viongozi wetu wa uislamu wanaweza kuandika waraka muflisi kama huu.
NAWASILISHA

Katika yote nakubaliana na wewe ila chadema kuwa kina udini hapo nawaunga mkono hao kina ponda kwa 100% ila mengine wametia chumvi tu na wanatumia ujinga wa baadhi ya waislam wasiojitambua
 
Mkuu hao jamaa wamezidi yaani kila siku humu ni matusi na kashfa zidi ya waislam. imetosha sasa kuweni wastarabu lasivyo mtaendelea kulia kila siku kwani dawa ya moto ni moto.

Nani alie!! Mnadhani tunawaogopa eeh! Waulize wenzako al shabaab kilichowapata, watu kama nyie ni kuwapoteza tuu fisi mumaji!! Kwa kweli sasa uvumilivu umekwisha, Namshukuru sana Nyerere, mimi ni mkristo lakini nakiri enzi nasoma wengi wa marafiki wangu walikuwa waislam, tuliishi kama ndugu lakini sasa ni ujinga umeachwa, ni waislam wachache wanaotaka kuharibu nchi yetu..
 
Kwa hiyo unathibitisha kuwa serikali ya kenya ni ya kikristo? Maana ndio wanapambana na al-shabab
Hata hivyo nakubaliana na wewe hata mimi wakati nasoma friends wangu wengi walikuwa sio waislam wenzangu lakini tuliishi kwa raha sana wengine mpaka leo ni marafiki zangu tu,muhimu turudi kuishi kama zamani hii habari ya udini ni jambo baya sana kwa mustakbali kama taifa
 
Jamani kama kweli tunapenda nchi yetu iwe na amani milele lazima kila mmoja kwa nafasi yake, hususan wale wenye kujiona wana busara wajiepushe na kila aina ya matusi au ucochezi wa aina yoyote kwa binadamu mwenzake bila kujali dini yake.
Wale ambao wamejaliwa kuwa na blogs na mitandao yoyote ile pia na vyombo vya habari basi wawe wa kwanza kuweka mbele azma ya kuminya kwa nguvu zao zote kauli za ucochezi kupitia katika vyombo vyao. Tanzania ikichafuka hakuna atakayefaidika. Hata akifa nduguyo ni hasara. Uchumi ukiharibika kutokana na machafuko ni hasara kwa kila mtu.
Nawaombeni wana blog tafadhali sana lindeni taifa letu changa. acha kabisa ku-post maandishi ya uchochezi kabisa ndugu zangu. kuweni na huruma na Taifa letu. tusikubali kutawaliwa na nguvu ya wajinga wachache hawa katika jamii yetu. kwani wana blog mwafaidika nini ku-post maadndishi ya uchochezi? Tumieni kipindi hiki tete ku-post maoni ya busara na ya kutuunganisha. Chonde chonde ndugu zangu. Twaua taifa letu kwa mikono yetu wenyewe? Na sisi wenye busara twakubali kuingia kwenye mtumbwi na wapumbavu wachache hawa ambao wameajiriwa kufanya kazi hatari kwa ulafi na upumbavu wao. sasa sisi waungwana tunakubali kuwa vipaza sauti vyao? Oh Mungu tujalie utujaze hekima mioyoni mwetu ili wote tujitambue.
Namaliza kwa kuwashukuru sana viongozi wa Kikristo kwa kuonyesha mfano. Busara mlizo oonyesha kwa Watanzania wakiwemo waislamu wenyewe ni za kuigwa na kila kiongozi wa dini yoyote. viongozi wa dini ya Kiislamu wengi hawajafanya kile Waislam na watanzania wote wenye busara tungetegemea mkifanye. Tulitegemea Viongozi wote wa Waislam mikoa yote monyeshe chuki zenu za dhati kwa kukana na kukaripia wahuni hawa wanaochafua hali ya hewa nautulivu wa taifa letu. Pigeni kelel kutoka kila kona ya nchi hii. Laani kabisa vitendo vya kihuni kwa kutumia kofia za dini.
Shekh Mkuu umefika wakati sasa wa kuangalia upya safu ya uongozi wako katika Bakwata. Angalia upya hata muundo wa utumishi wa baraza hilo. tunahitaji viongozi wa mfano wa shekh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaamtu. Lakini vile vikundi vya kihuni ambavyo navyo vimeasjiliwa kisheria na viko njia panda na pakwata hivyo huviwezi kwa kuwa havikutambui na wala huna mamlaka navyo. Hivyo viachie serikali kama ikiamua kuwalea basi watanzania 2015 wataamua ni srikali ipi iingie madarakani. Najua Kikwete na baadhi ya wenzake watakuwa wamemaliza awamu yao lakini wajue mzimu wa udhaifu wao utawfuata popote watakapokuwa. Mungu ibariki Tafa letu mungu barki dini zetu halali na makini tu.
 
Amani bila kuvumiliana haiwezekani. tuna imani tofauti kwahiyo ni jambo la kustahiana na kuvumiliana.
Kila dini inafundisha watu wake kwamba yenyewe ndio njia pekee ya kufika kwa Mungu. Mimi ninasema busara lazima itumike. Leo tuko hapa kwasababu tumeamua kupuuza misingi ya maisha ya amani.
Kila mmoja awafundishe watoto wake kwamba dini ya mtu mwingine ni njia yeye anayoamini itampeleka kwa Mungu kwa hivyo iheshimiwe hata kama wewe hauiamini. Watoto waepushwe na uwezekano wa kutumika kwenye mitego yenye lengo la kueneza chuki miongoni mwa watu.
Serikali itunge sheria kali dhidi ya kejeli, mizaha na matusi yanayotolewa na watu Fulani dhidi ya dini nyingine. Watu hao wasionewe aibu wala huruma wapeqe adhabu kali haraka iwezekanavyo na iwe fundisho.
Wengi wa watu wanaoshiriki sasa kwenye fujo hizi ni victims tu - wachochezi wenyewe Wako salama. Serikali iwatafute hao na iwarudi kwa kishindo kikuu.
Zaidi ya hapo itakuwa upuuzi kwa Wakristo kurusha matusi hewani dhidi ya Uislamu. Uislamu ni dini mama nyingine lakini ni kweli elimu kwa wengi wao imechelewa sana. Hata hivyo watu Fulani wanawatumia watu hawa kama mtaji wa kutekeleza malengo Yao.
Mimi sina ugomvi, chuki wala uhasama na Waislamu wenye dini Yao. Nimeshakutana na Waislamu ambao ni Waungwana na waadilifu kuliko mimi na huenda hata wewe Mkristo mwenzangu.
Tutumie busara katika reactions zetu. Tusiwape wachochezi nafasi ya kututumia na sisi kufikia malengo Yao.
Wanaoshiriki Leo kwenye Fujo Fuji tutakuwa tayari kusamehe na kusonga mbele na uhusiano wetu utakuwa strong zaidi baada ya hapo.
Refer South Africa na kabla na baada ya usuluhishi na maridhiano.
G'Day.
 
Katika yote nakubaliana na wewe ila chadema kuwa kina udini hapo nawaunga mkono hao kina ponda kwa 100% ila mengine wametia chumvi tu na wanatumia ujinga wa baadhi ya waislam wasiojitambua

Tupe hoja za uthibitisho mkuu

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Katika yote nakubaliana na wewe ila chadema kuwa kina udini hapo nawaunga mkono hao kina ponda kwa 100% ila mengine wametia chumvi tu na wanatumia ujinga wa baadhi ya waislam wasiojitambua

Rafiki yangu hata hilo la kwamba CHADEMA kina udini ni uongo mtupu na ni propaganda tu za kisiasa! Udini umetumika na watawala kudanganya wapiga kura ili kupata kura zao kiurahisi.

Utakumbuka wakati CUF ilikuwa tishio kwa CCM mwaka 2005 wananchi waliambiwa ni chama cha kidin-kiislamu na kwamba kilikuwa na mpango wa kufanya nchi hii iwe ya kiislamu pindi watakapochukua madaraka. Hata walisingiziwa Kuingiza silaha toka uarabuni. Na kweli wakristo wengi waliachana na CUF.

Ni janja hii hii imetumika kuwaogopesha waislamu mwaka 2010 ili wasipigie kura CHADEMA na kwa bahati mbaya hii propaganda imeendelezwa hadi leo na kuwekwa vikolezo vya ukabila, udini na ukanda. Na kwa bahati mbaya zaidi kina Ponda wameweka kibwagizo na kuongezea kuwa adui wao ni wakristo-ujinga mkubwa!

Sasa jiulize CHADEMA au CUF ni vyama vya kidini kwa misingi ipi? Soma katiba zao, soma sera zao, angalia wanachama wao kama wanatoka mkoa mmoja au dini moja, hudhuria mikutano yao na hata angalia viongozi wao wakuu je ni wa dini moja? Tena utashangaa viongozi wakuu wa CHADEMA Sita, Kati yao 4 ni waislamu. Niliwahi kuweka orodha yao hapa jf wakati wa kuchangia hoja. Ila ngoja nikuwekee kwa urahisi wa kuliona hili. Ila nakushauri uwe unatafuta taarifa badala ya kusubiri kudanganywa na kina Ponda.

Viongozi wa Kitaifa wa CHADEMA

1. Mwenyekiti Mhe. Freeman Aikaeli Mbowe- Kutoka Hai, Kilimanjaro

2. Makamu Mwenyekiti Bara, Mhe. Said Amour Arfi -Kutoka Mpanda, Rukwa

3. Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Mhe. Said Issa Mohammed-Kutoka Pemba

4. Katibu Mkuu, Mhe. Willibrod Peter Slaa-Kutoka Karatu, Arusha

5. Naibu Katibu Mkuu - Bara Mhe. Zitto Zuberi Kabwe-Kutoka Mwandiga, Kigoma Kaskazini

6. Naibu Katibu Mkuu - Zanzibar Mhe. Hamad Mussa Yussuf-Kutoka Kaskazini Pemba

Nadhani majina yanajieleza.

Unaruhusiwa kuwa mwanachama wa chama chochote lakini usiache kujiunga na chama chochote kwa kudanganywa kwamba ni chama cha kidini. Kwanza kutokana na katiba ya nchi yetu chama chenye udini hakiwezi kusajiliwa na kikigundulika baada ya kusajiliwa kinaweza kufutwa kwa mujibu wa sheria.
 
Nyerere ni Rais pekee hapa Tanzania aliyetafuta fedha na kusimamia ujenzi wa nyumba ya ibada isiyo ya dini yake msikiti wa butiama. Kwa maneno yake alikwenda kwa Gadaff ambaye ni mwislamu na kumwambia kwamba wananchi wake wa dini ya kiisilamu kijijini kwake butiama hawana mahali pa swala Gadaff akajenga msitiki wa kisasa kwa wailsmau.

Hii rekodi bado haijavunjwa na Rais yeyote hapa nchini baada ya Nyerere.

Je waislamu wanahaki ya kubeza matendo yote ya Nyerere

Pia mkapa rais mkristo katoa majengo ya tanesco kuwapa waislam kiwe chuo kikuu na kimeitwa muslim university!
 
Mada hii nimeipenda, imegusia ukweli ambao wengi wanaukwepa huku wakiutambua. Mungu bariki Tz
 
Eee mwenyezi, tuongoze katika njia ya amani, tuepushe na mabalaa, watoto wako daima tusiangamie. Amen. Ndg zangu nani atabaki? Maana vita havina macho!. Nani anahaki zaidi ya mwenzake? Nani kapewa haki ya kuwahukumu wenzake hapa duniani? Kama mtu kakidharau kitabu kitukufu, basi iko siku mwenyezi mungu atamhukumu!.
 
Hongera kwa kujiita muislam poa na mstaarabu @mapogolo. nimekusoma na kukuelewa lakini nimesikitishwa na uelewa wako unaouona ni wa juu na kushindwa kabisa kuisoma hali halisi ya propanganda kwa waislam inayofanywa na Bakwata (waisalamu poa na wastaarabu) kwa kushirikiana na serikali na kainisa. Ikiwa wewe kweli ni muisslam Mungu pekee ndo anaona yaliyovifuani mwa wanadamu atahukum kwa myaliyokifuani mwako.
Unaona la kuuzwa kiwanja cha PSRC kwa METL lkn ya Bakwata kuuza mali za waislamu nchini kote zilizolithiwa kutoka EAMWA kwa maunufaa yao ni sawa kwa kuwa unatutaka tuwe poa na wastaarabu- heri akina ponda wanuchungu na uislam kuliko kuwa poa na mustaarabu.
Ukiona serikali inasiomamia uchanguzi wa chombo cha dini (Bakwata) ujue kuna sababu za makusudi zilizoasisiwa na JK Nyerere na kurithishwa kupitia mfumo wa wakiristo katika sekta zote nyeti za maamuzi, mbona TEC, na vyombo vingine vya wakirstu KAtolik, Lutheran, Anglikana wanachagua viongozi wao kwa uhuru bila serikali kuingilia kati, why Bakwata? kwa sababu inalinda maslahi ya serikali na Kanisa-wanajua wakiingia akina Ponda na wengine wanoaona uchungu na uislam wao waislam waamka kudai haki zao na kusimamia maendeleo yao.
Mungu akulipe kulingana na uono wako-uenda kwa upande wako uko sahihi.
 
If @Nkadabwi you dont have something tangible to talk (discuss) please keep quite-being christian, Muslam -all who dont have followed these religions are called pagan -whether are your g'pa or wathever. When the truth is out and whether it was wrongly done prior to the truth, then to say that the doears were lost is not a sin at all.
 
Nchi yetu iko katika hatari kubwa ya kuingia katika machafuko ya kidini yanayotokana na kufumbiwa macho chokochoko za kidini ambazo zimeanza muda mrefu sasa. Uvumilivu miongoni mwa waumini wa dini kuu chini yaani uislamu na ukristo ambao umekuwepo nchini toka uhuru sasa unatoweka kwa kasi ya ajabu.

Nimesoma kinachoitwa "waraka wa waislamu" nimeweka inverted commas kwa sababu sikubaliani kabisa na title hiyo. Kilichomo ndani ya waraka huo hakina sifa ya kuitwa waraka wa waislamu kwani ni dhihaka na tusi kubwa kwa waislamu wengi ambao ni wastaarabu, wastahimilivu na wasomi. waraka umejaa ujinga mtupu ukisherehesha na matukio ya kubuni ya uongo na ya kiwango cha chini sana ndiyo maana nasema haustahili kuitwa waraka wa waislamu, ungefaa kuitwa "waraka wa ponda kwa waislamu ambao ni wajinga"

Waraka unajaribu kutuaminisha kuwa Mhe Hadji Mponda na Mhe. Mustapha Mkullo walipoteza nafasi zao za uwaziri kwa shinikizo la wakristo bila kujali tuhuma mbalimbali zilizoelekezwa kwao ikiwamo ubadhirifu na kushindwa kumudu majukumu yao. Tunafahamu Mhe Mponda alishindwa kushughulikia ipasavyo mgogoro wa madaktari na serikali, pia ili lazimu awajibike kwakuwa MSD iliyo chini ya wizara yake ililitia hasara taifa la zaidi ya shs 5bilioni kwa kusababisha dawa zenye thamani ya pesa hiyo kuharibika kwa kufikia mwisho wa muda wake wa matumizi(expiry) bila kuzisambaza mahospitalini ambako zilikuwa zikihitajika sana na wagonjwa wakifariki kwa kuzikosa dawa hizo. Pamoja na Mhe Mponda mwingine aliyewajibika katika hili ni Mhe Dr Lucy Nkya aliyekuwa naibu waziri, lakini waraka haumtaji kwa kuwa ni mkristo hivyo hoja ya udini inayojengwa itavurugika.

Mhe Mkulo pamoja na kushindwa kabisa majukumu yake kama waziri wa fedha alikuwa na tuhuma za kuuza kinyemela kwa kampuni ya METL kiwanja mali ya PSRC. Pia Mkulo alishinikiza kuvunjwa kwa taasisi ya CONSOLIDATED HOLDING LIMITED na kuhamishiwa shughuli zake kwa msajili wa hazina. Hapa lengo lilikuwa ni kuwalinda wadaiwa sugu ambao bado hawajamaliza kulipa madeni yatokanayo na ununuzi wa mashirika ya umma. CHL ni mrithi wa iliyokuwa ikiitwa PSRC. Mhe Zitto Kabwe ndiye aliyeibua sakata hili lakini waraka haumtaji kwakuwa ni muislamu ili kujenga dhana kuwa Mkullo aling'olewa kwa shinikizo la wakristo.

Waraka una maelezo marefu lakini yasiyoeleweka juu ya chadema kuwa chama cha kikristo ambacho waislamu tumetakiwa kujiepusha nacho bila kutueleza na kutuelekeza chama cha kukiunga mkono ambacho bila shaka ni cha kiislamu. Jambo lingine ni mali nyingi zinazomilikiwa na makanisa kuwa eti imewezeshwa na mfumo kristo uliopo nchini. Nasema huu ni ujinga na uongo wa mchana kweupe kwani taasisi za kikristo toka kabla ya uhuru pamoja na kuandaa waumini wao kiroho hazipata kuwa nyuma katika kushughulikia huduma za kijamii kwa waumini wao pamoja na wasiokuwa wakristo. Wakristo walimiliki shule na hospitali nyingi ambazo zimehudumia watanzania wote bila ubaguzi. Baba yabgu mzazi ambaye ni mwislamu alisoma katika shule za kikristo yaani st mary na st andrews. Shukrani za pekee kwa baba wa taifa(mkristo) ambaye alitaifisha shule za kanisa ili kuwezesha waislamu kusoma katika shule hizo, pamoja na hatua hiyo ya kizalendo kuna waislamu wenzetu ambao wanamdhihaki mzee huyo kwa udini, huku ni kukosa shukrani kwa kiwango cha juu sana.

Najiuliza bila hatua hiyo ya Nyerere wazee wetu wa kiislamu wangesoma wapi ilhali Mazengo sec schoo, Mkwawa sec. school, Tosamaganga, Musoma alliance, Pugu, Minaki, Malangali, Rugambwa, Forodhani zilikuwa mali ya madhehebu ya kikristo. Narudia kuandika tena kuwa waraka huu ni janga na ni kielelezo kuwa waislamu bado tunasafari ndefu ya kuutokomeza ujinga kama wanaojiita viongozi wetu wa uislamu wanaweza kuandika waraka muflisi kama huu.
NAWASILISHA
hawa akina mapogolo ndo waislam sasa.mnaona hoja zao ee!saafi sana mapogolo kwa kujenga hoja nzuri.wale mnaowaona wanavunja makanisa ni mapoyoyo.mkiwaona tena tiini sheria kikwelikweli tena bila bila shuruti.kwa sababu huwa hata mkisema muwashauri wawasikii kazi jazba tupu.
 
Haifai kutukana kwa namna hiyo blueray ikiwa wewe unasimamia amani timiza wajibu wako wa kushauri si kushangaa- haiwi busdara kwa mtu anayelalamika kulaaniwa bila kufanya juhudi ya makusudi kujua sababu ya kulalamika kwake ikiwa wewe ni muadilifu na si miongoni wa wanaosababisha mtu kulalamika. Ikiwa ni mmoja wapo basi utaona lengo lako limetimia na utajidai kushangaa watu wanaomfuata Sheik Ponda-utamwaona ni mwendawazimu kwa sababu unasimamia dhulma au hujui kwa usahihi kile anachokisimamia na kukitetea kwa sabau ya mazongwe ya kuwamo ktk mfumo huo. Jipe muda tafiti na uliza ueleweshwe -kwa amani kabisa utaujua ukweli then utakuwa na nafasi nzuri ya kuchangia bila kutukana watu. Jenga hoja si matusi ikiwa kweli unauthamini utanzania wako kuliko dini za wazungu
 
Back
Top Bottom