Waislam Wapigwa Stop na Kova

Nasema maandamano yangefanyika yangekuwa yanaidhalilisha sana dini ya kiislam,viongozi wake,waumini wake,kitabu chake[Quran] na Mtume wake Muhamad SAW kwasababu zifuatazo.

[1] Waislamu wanataka kuandamana kwasababu serekali ya CCM imeshindwa kuanzisha mahakama ya Kadhi.Ukweli ni kwamba Serekali ya CCM imewaruhusu waislam waanzishe na kuiendesha mahakama ya kadhi wenyewe kwasababu ni sehemu ya ibada yao [waislamu].Ni ajabu kubwa kuona wanazuoni tena waliobobea kuendelea kudai mahakama ya kadhi ilihali serekali imesharidhia kuanzishwa kwake.

[2] Waislamu wa Tanzania wanajua wazi CCM imekuwa ikiwadanganya wananchi kwa muda mrefu katika mambo mabali mbali,inashangaza sana kusikia viongozi wa waislam hawakuona haja ya kuandamana wakati mabilioni ya EPA,Meremeta,ununuzi wa radar,ndege ya rais,mikataba ya madini na ufujaji wa fedha kwenye maidara ya serekali ukifanyika.Akili yangu inakataa kuamini kwamba viongozi wa waislamu leo hii wanagundua CCM ni waongo kwasababu tu wameshindwa kuvunja katiba ya JMT kwa kuingiza mahakama ya kadhi.Viongozi wa aiana hii kamwe hawataweza kuwakomboa waislam kwasababu wanashindwa kuwaeleza ukweli waumini wao kwamba mahakama ya kadhi inaweza kuanzishwa na waislamu wenyewe bila kutegemea fadhila za serekali.

Umeongea pointi tupu ndugu yangu! Haya mambo ya kulazimisha Serikali "ifuge ndevu, kuvaa kanzu na kuvaa kibaraghashia" hayafai kabisa kwa nchi yetu, yatatuletea vurugu huko mbeleni na patakuwa hapakaliki!
 
mbona unajidanganya. Mbona yale ya yesu sio mungu talifanikiwa
then mukawa victorious kwa kitu gani? hivi ninyi nani aliwapandikiza ujinga kiasi hiki? we maandamano ya Yesu si Mungu mlipewa haki na nani ili kuonekana kuwa mmefanikiwa, sikujua kuwa wewe MS akili yako ni shake well kiasi kikubwa namna hiyo
 
You are totally wrong! Hakuna uhuru usiokuwa na mipaka ndugu, hata kama utaubandika jina la demokrasia, uhuru wako unapoishia ndipo na wa mwenzako unapoanzia! Hawa watu wameambiwa waanzishe Mahakama yao wenyewe, bado wamekaa vijiweni kunywa kahawa wakisubiri Serikali iwaanzishie IBADA yao ya KIISLAMU! Upstairs kwa hawa wandugu kunafanya kazi kweli?

Mkuu Buch nilichokuwa namaanisha mimi sio uhalali wa kuanzisha mahakama yao ya kadhi bali ni uhuru wa kuandamana.
Wangeachwa waandamani ili mradi wasivunje sheria.
kuwazuia kuandamana ni kama kuwahofia hasa ukizingatia wanaandamana kwa sababu ya kuhamasisha wananchi wasiichague tena CCM.
 
Hebu tuangalie kwa ufupi Sheria ya Mahakama ya Kadhi Zanzibar (The Kadhi's Court Act, 1985, No. 3 of 1985) inasemaje. Kumbuka kuwa suala la Mahakama (isipokuwa Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania), si la Muungano, kwa hivyo isidhaniwe kwamba Katiba ya JMT inalihusu!
Section 4 (1). "There shall be a Chief Kadhi who shall be appointed by the President. (2) The Chief Kadhi shall not enter upon the duties of his office until he has taken and subscribed the oath of allegiance...as may be prescribed by the House of Representatives. (3) A person shall be qualified to be appointed to hold or to act in the Office of Chief Kadhi if, and shall not be so qualified unless- (a) he professes and follows the Muslim religion; (b) he possess such knowledge of the Muslim law which in the opinion of the President is qualified to be appointed as such."
Kama Mahakama za Kadhi ndio zinatakiwa Rais awe anamteua CHIEF KADHI na pia maoni yake kuhitajika KWENYE MAMBO YA KIDINI, sasa hiyo nchi sio ya Kiislamu? Anyway, kwa Zanzibar, Waislamu ni wengi, lakini Wakristo nako wapo, Je, akishika madaraka Mkrito atamteua Kadhi? Very confusing indeed!
 
Mimi huwa sipendi kujadili udini, kwani naamini hakuna mwenye haki kuliko mwingine kusema dini yako si ya ukweli ilihali hajui ukweli wa dini hiyo! Lakini kwa mawazo kama ya MS na wenzie ndio maana kila mara waislam huonekana kama watu wasiosoma! Unawezaje kusema eti " tulifanikiwa katika maandamano ya YESU si MUNGU" kama alivyosema Anyisile, nini kipimo cha mafanikio hayo? maana kuanzia wakati huo hadi sasa na hadi mwisho wa dunia bado wakristo wataendelea kuamini kuwa YESU ni MUNGU, na hilo hakuna wa kuwabadilisha hata kama waislam watawawekea mtutu wa BUnduki au kuwachoma moto kama wale mashahidi wa Uganda, kwao itabaki hivyo hiyo kuwa YESU ni MUNGU! kwani nini MS na wenzio wasikubali tu kuwa " Wao wana dini yao, nanyi mna dini yenu!, mnachoabudu ninyi sio wanachoabudu wao" Mbona wakristo wameisha kubali hilo! MS kuwa mstaarabu udini hauna nafasi katika karne hii!
 
wamepigwa changa la macho, nitafurahi kama hamta ichagua sisiemu/ccm, chagueni chama cha upinzani na hilo halina haja ya kujitangaza au kufanya mayowe yoyote, fanyeni kimyakimya tu.
 
Mkuu Buch nilichokuwa namaanisha mimi sio uhalali wa kuanzisha mahakama yao ya kadhi bali ni uhuru wa kuandamana.
Wangeachwa waandamani ili mradi wasivunje sheria.
kuwazuia kuandamana ni kama kuwahofia hasa ukizingatia wanaandamana kwa sababu ya kuhamasisha wananchi wasiichague tena CCM.

Sasa hapo sio kuingia tena kwenye siasa ndugu? Na msingi wa maandamano hayo ni upi hasa ukizingatia kwamba Mahakama za Kadhi zimeruhusiwa kuanzishwa na waislamu na kuendeshwa na waislamu wenyewe kwa gharama zao?
 
Kova na wenzake na hata wakubwa zake wanaweza kudhibiti maandamano. Kama kweli waislamu wamedhamiria kuinyima usingizi CCM mwaka huu wanazo njia nyingi mno. Someni kwanza mazingira ya adui yako na ndipo mtengenezee silaha itakayommaliza kiulaini. Nyuki hana nia mbaya kwa binadamu na viumbe wengine, lakini wakidhamiria kumdhibiti adui yao hapakaliki japo pia wanao uwezo kukupatia asali. Tamu na chungu vyote wanavyo.

Waislamu wamemzoeza CCM kumpa asali miaka yote, sasa kama wanataka kumwondoa jengoni pia wano uwezo huo wakitaka kweli.
 
So far katika nchi hii hakuna maandamano ambayo yamekuwa na productivity!...Wastage of time at the peak tune!
Maandamano ya wanafunzi wa chuo kikuu huwa ni productive. Maana huko haki huwa haipatikani bila maandamano.
 
Sasa hapo sio kuingia tena kwenye siasa ndugu? Na msingi wa maandamano hayo ni upi hasa ukizingatia kwamba Mahakama za Kadhi zimeruhusiwa kuanzishwa na waislamu na kuendeshwa na waislamu wenyewe kwa gharama zao?

Unajua kuna makubaliano ambayo CCM ilikubaliana (kipindi kile cha harakati za Jk kuingia madarakani) na waislamu juu ya kuanzishwa kwa hii mahakama.
Pengine walikubaliana hiyo mahakama itaanzishwa kama waislamu walivyotaka na sio kwa hivi serikari ilivyotaka sasa.
Wa kumlaumu hapa ni CCM ambayo iliwaahidi waislamu kabla hawajaingia tena madarakani 2005, na sasa wamepata tena madaraka, wameenda kinyume na makubaliano yao
LEKANJOBE yupo sahihi kama waislamu wanataka kuiadhibu CCM wanaweza wakakubaliana wenyewe kuwa siku ya uchaguzi wasiichague tena CCM kwa sababu iliwadanganya.
 
Ndugu zangu, waislamu hii habari ya dini ya nini sasa.Mkuu wa Kaya hawezi kubali hii kitu la sivyo hatashindwa kwenda ulaya kuomba misaada. Mzungu anaweza sema unafuga al qaeda nchini mwako
 
Malaria Sugu,
Mkuu unaanza kunishtua vitu ambavyo sikuwa navitazama hapo zamani!
 
Unajua kuna makubaliano ambayo CCM ilikubaliana (kipindi kile cha harakati za Jk kuingia madarakani) na waislamu juu ya kuanzishwa kwa hii mahakama.

Hivi Mahakama hiyo ikianzishwa na kuendeshwa na waislamu wenyewe bila kuingiliwa na Serikali inakuwa SIO MAHAKAMA YA KADHI? Mbona imeng'ang'aniwa kwamba Serikali iliahidi, Serikali iliahidi, Serikali iliahidi..........Serikali iliahidi! Ni kweli iliahidi kulitafutia UFUMBUZI suala la uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi! Serikali HAIKUTOA ahadi kwamba "Itaanzisha na kugharamia Mahakama za Kadhi!" Mbona mambo rahisi yanataka kufanywa kuwa magumu kama chuma cha pua
 
waislamu kuandamana sio suala la demokrasia bali ni utamaduni wao hata kwenye nchi zote za kiislamu ni maandamano kwa kwenda mbele...yaani ni kupinga kupinga....yaaani hawa wa2 wa ajabu sana...wanafikiria shari tu wakati wote.............
''TUWAOMBEE KWA YESU AWAPONYE''.......baadhi ya wale wabishi waliishajisalimisha.
Ninavyoona mimi kuandamana kwa amani kahuna tatizo ni haki ya wananchi.
Serikali inaogopa nini? au inahofu wananchi watahamasika na kutoichagua CCM?
Swala sio udini, ni demokrasia.
 
Hebu tuangalie kwa ufupi Sheria ya Mahakama ya Kadhi Zanzibar (The Kadhi's Court Act, 1985, No. 3 of 1985) inasemaje. Kumbuka kuwa suala la Mahakama (isipokuwa Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania), si la Muungano, kwa hivyo isidhaniwe kwamba Katiba ya JMT inalihusu!
Section 4 (1). "There shall be a Chief Kadhi who shall be appointed by the President. (2) The Chief Kadhi shall not enter upon the duties of his office until he has taken and subscribed the oath of allegiance...as may be prescribed by the House of Representatives. (3) A person shall be qualified to be appointed to hold or to act in the Office of Chief Kadhi if, and shall not be so qualified unless- (a) he professes and follows the Muslim religion; (b) he possess such knowledge of the Muslim law which in the opinion of the President is qualified to be appointed as such."
Kama Mahakama za Kadhi ndio zinatakiwa Rais awe anamteua CHIEF KADHI na pia maoni yake kuhitajika KWENYE MAMBO YA KIDINI, sasa hiyo nchi sio ya Kiislamu? Anyway, kwa Zanzibar, Waislamu ni wengi, lakini Wakristo nako wapo, Je, akishika madaraka Mkrito atamteua Kadhi? Very confusing indeed!

Mkuu, kuna habari nilisikia Somalia wanaume wanalazimishwa kufuga mindevu na wanawake kuvaa hijabu. Hivi ndiyo matokeo ya kuwa na mahakama ya Kadhi? Mimi naigopa sana ikianzishwa kama taasisi ya kiserikali (ikiwekwa kwenye Katiba)! Baada ya mahakama ya Kadhi, kitakachofuata ni kupiga wanaotuhumiwa wamezini mawe hadi kufa na pengine kutakata mikono ya wanaotuhumiwa wameiba. Nikiona jinsi nchi yetu ilivyojaa na vilema, kwa sababu baadhi yao ni wale waliopata ajali, na halafu tuongeze wengine wasio na mikono, in the long-run tutakuwa taifa tegemezi kabisa! Yaani, tutakuwa na idadi kubwa ya watu tegemezi (wao wenyewe na watu wanaowategemea).
 
Hivi Mahakama hiyo ikianzishwa na kuendeshwa na waislamu wenyewe bila kuingiliwa na Serikali inakuwa SIO MAHAKAMA YA KADHI? Mbona imeng'ang'aniwa kwamba Serikali iliahidi, Serikali iliahidi, Serikali iliahidi..........Serikali iliahidi! Ni kweli iliahidi kulitafutia UFUMBUZI suala la uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi! Serikali HAIKUTOA ahadi kwamba "Itaanzisha na kugharamia Mahakama za Kadhi!" Mbona mambo rahisi yanataka kufanywa kuwa magumu kama chuma cha pua

Kuna msemo unasema: 'Nimekupa mkono wewe umeshika bega!' Hawa ndugu wakifanikiwa kwa moja utaona jinsi watakavyofanikiwa kwa yote... CCM ingejidanganya kujihusisha, ingekosa uhuru. Maana wangetakiwa kila mara wafanye kile kinachopendwa na hao ndugu. Sasa nani ataweza hayo?
 
Back
Top Bottom