Waislam msiende liliondo- redio kheir

Jana kulikuwa na mjadala na kuwataka waislam kuacha kwenda liliondo. walisema hio ni dawa ya kiini macho. walisema kama kuna mtu amepowa kwa dawa hiyo ajitokeze waziwazi kabla ya kupoa akiuumwa nini na sasa apime aonyeshe kwamba kama kweli amepoa.
waliwataka waislam kuachana na kabisa dawa hiyo wanayoita ni DECI

waache kwenda kwani kuna aliyewalazimisha kwenda? Babu hana taimu na mtu wala hahitaji mtu, na hao tunaopiga nao kitimoto pale kigogo wakatazwe maana wanasababisha bei ya kitifire ipande . wao waende kwenye ngoma, ramri na madogori huko kuna uponyaji
 
Mie nawaunga mkono kwa asilimia 100 kwani kama Waislamu watasikiliza ushauri huo wa wivu utatupunguzia foleni ya kupata kikombe cha uponyaji sisi tulie na imani ya kuponywa.
 
Kuna watu wanataka kuwalazimisha wengine watangaze hali zao za afya,suala la afya ni suala la mtu binafsi.
Kikwete ameanguka zaidi ya mara tatu na hakuna tulichoambiwa kuhusu tatizo la afya yake,tuanze kumshinikiza rais atangaze kwanza kinachomsumbua,wafuatie viongozi kisha ije zamu ya raia,kwa taarifa yenu kikwete kanywa kikombe cha babu na amepona ila hajapenda kutangaza
 
Jamani hakuna aliyelazimishwa kwenda loliondo manake naona swala hili watu wanalijadili kidini na wengine wanahofia kuhamwa na waumini wao jambo hilo si kweli.
Mimi binafsi ni mkristo na naamini ile dawa inawasaidia watu na mimi mwenyewe nina baba yangu mzazi alikua anasumbuliwa na kisukari na amepona hajatumia dawa huu ni mwezi sasa na soda anakunywa sasa bila wasiwasi wowote.
Kwa waislamu nawashauri wenye matatizo waende wasiogope ile dawa haichagui dini ya mtu ila ni wewe uwe na imani tu utapona usiende pale kujaribu hutapona natoa angalizo.
Dunia nzima itakuja arusha naomba kuwasilisha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom