Mwawado
JF-Expert Member
- Nov 2, 2006
- 993
- 252
Tusipokuwa waangalifu Taifa letu litaingia pabaya sana kwa kuangaliana kwa majina yetu....Ukiitwa Mohamed utakosa haki ya kusaidiwa na kushirikiana na Richard,Tukimaliza hapo tutaangaliana kwa rangi,Yule Sabogo,Rostam au Abood hatokuwa na haki sawa na kina Mwasakafyuka,Rwegasira au Ntagazwa..Sumu hiyo ni mbaya na tuikemee,inaanza kama Utani lakini matokeo yake ni mabaya sana.
Jirani zetu Kenya walianza kulaumiana kwa ubaguzi wa kimakabila,na baadaye kila uteuzi wa Mzee Kibaki ukatafsiriwa kuwa ni njia ya kuimarisha kabila moja na kudhoofisha mengine,Katiba ikabadilishwa kumuondolea Rais uwezo wa kuteua bila kuulizwa,kwani sasa teuzi zote lazima zipitie kwenye Bunge.Juzi kwa kuondoa hali hiyo ya kupigiana kelele kwa makabila Rais kamteua Jaji Mkuu Mkenya mwenye asili ya kihindi.Hali hiyo imesababisha kero kubwa,kwani Bunge limekutana na kujadili kwamba Rais amekiuka utaratibu wa Katiba kwa kutomshirikisha Waziri Mkuu katika Uteuzi huo.Inawezekana kwamba kuna ukweli kwamba Rais alipindisha utaratibu,lakini ukiangalia nyuma ya pazia Ubaguzi wa kikabila ndio umekuwa uchochezi mkubwa katika siasa za jirani zetu
Tuogope Tatizo hilo la kubaguana kwa kuangalia Udini,Rangi au makabila...Katika Katiba yetu mpya kuwepo na pendekezo la kutoshirikisha namna yoyote ya Ubaguzi wa namna hiyo na Utendaji wa Serikali,kwani Serikali haina dini.Katika Kipindi hichi cha Uongozi wa Awamu ya Nne kumekuwa na malalamiko mengi ya Teuzi kuegemea Upande wa dini moja zaidi,tuondoe mawazo hayo ili tujenge Taifa lisiloendeshwa kwa mashinikizo ya kidini.
Waislamu wa Kigoma wamekuwa wakali,kwa sababu tu watendaji wao wakuu kiserikali Mkoani wote ni Wakristo.Tuwaelimishe wananchi hao,ili waangalie Utendaji kazi wa mtumishi na si dini yake.hapa chini naorodhesha baadhi ya watendaji wa Serikali Mkoani kigoma
1); Mkuu wa Mkoa - Joseph Simbakalia.
2);Mkuu wa Wilaya Kigoma - John Mongela.
3);Mkuu wa Wilaya Kibondo - Danhi Makanga.
4);Mkuu wa Wilaya Kasulu - Betty Machangu.